Na iwe hivyo kwa Freeman Mbowe...
Ukweli wa kudumu unaosimama milele na milele ni huu:
DHULUMA, UOVU NA UONEVU HAUJAWAHI KUISHINDA HAKI...!
Unaweza kuichelewesha tu hiyo HAKI lakini haiwezekani KUIZUIA isifuate mkondo wake kuelekea kwa mwenyewe....
Hopefully, hizi ndizo dalili za mwisho mwisho za udhalimu na utawala wa mashetani ktk nchi hii...
Wiki chache zilizopita niliandika mada humu yenye kichwa kisemacho;
"..Rais Samia Suluhu Hassan ndiye Rais wa kwanza mwanamke Tanzania, alama ya mwisho ya siasa na utawala wa CCM Tanzania..."
Unabii huu unasimama imara LEO, KESHO na MPAKA utimie kwa ukamilifu wake na mchakato (process) yake ya kutimilika ndiyo hii, taratibu udhalimu unajizika wenyewe, ukombozi na haki itachukua nafasi yake katika nchi hii tuliyopewa na Bwana Mungu baba muumba....!
Shetani kwa kuwatumia wenzetu wachache kwa kuwapa madaraka ya kiutawala hawawezi kuwashinda watoto na watu wa Mungu halali na wamiliki wa nchi hii...
Tuendeleeni kuwaombea, kuwatia moyo na kuwa sapoti front liners wa vita hii ya ukombozi. Mahubusu au magereza hiyo ni njia tu ambayo ni lazima baadhi yetu wapitie hapo na kwenda tunakotaka tuende. MSIOHOPE wala MSIHOFU...