Mashamba Makubwa Nalima
JF-Expert Member
- Mar 19, 2024
- 4,978
- 2,411
pamoja mkuuNitakuwa na Dr. Slaa na Ndg. Lyatonga Mrema kwenye matangazo ya mchana kwenye "Mwanakijiji Live" usikose!!!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
pamoja mkuuNitakuwa na Dr. Slaa na Ndg. Lyatonga Mrema kwenye matangazo ya mchana kwenye "Mwanakijiji Live" usikose!!!!
Watakua wamefanya jambo la maana if really we need reforms lazima tuanzie huko mafisadi wote warudishe hela ya serikali na wale ambao kwa macho ya kawaida hawaonekani wakatwe mikono
Hili Kaburi limefikuliwa kwa sababu gani?😄😃😆😀pamoja mkuu
Tangu tutangaze orodha ya mafisadi pale viwanja vya MwembeYanga, mjadala mkali sana umetokea katika taifa. Mara baada ya kutangaza orodha hiyo siku ya jumamosi tarehe 15 Septemba, waliotajwa wengi walikaa kimya bila kujibu chochote wakiamini kuwa vyombo vya habari havitataja majina yao. Ni kweli takribani vyombo vyote vya habari havikutaja majina yao.
Wiki iliyopita ikabadili kabisa mjadala huu ambao ulikua umeanza kulala. Gazeti la MwanaHalisi lilitaja Mafisadi wote kwa majina na kwa vipi wamehusika. Hapo ndipo waliotajwa walipoanza kujibu mmoja baada ya mmoja.
Najua kuwa Mkuu wa Kaya aliagiza kupitia Waziri Marmo kuwa kila mtu ajibu tuhuma zake. Waziri Mkuu alikuwa ni mmoja wa watu waliogomea agizo hilo la mkuu wa kaya ya kwamba kila mtu ajibu tuhuma zake mwenyewe. Aakamtuma Mzee Kingunge ajibu. Haikutosha na pia mwungwana akahimiza kupitia kwa Waziri anaepata nguvu za ajabu hivi sasa ndugu Marmo. Karamagi akaanza!
Majibu ya Karamagi na yale ya Mgonja, ambae alifuatia yanafanana sana. Mtindo wao wa kujibu ulikua ule ule.
Hata hivyo, majibu ya Patrick Rutabanzibwa, mmoja wa wasomi wazuri sana katika Taifa hili yamenifanya nitake tujadili, tumjadili kwa kina yeye na ufisadi wake na ikibidi humu humu totoe 'verdict'. Wale walio karibu nae wamwombe aje humu katika mjadala huu. Kwa nini yeye?
Angalau yeye amejibu baadhi ya tuhuma zake katika mkutano wake na waandishi wa habari. Wakati Karamagi na Mgonja wametishia tu kwenda mahakamani, Rutabanzibwa yeye kasema ni masuala gani hahusiki nayo na yepi anahusika nayo. Kasema kwa kina ni vipi hahusiki na IPTL lakini kakubali kuwa katika bodi ya TANGOLD na pia kuwa na hisa za kampuni hii. Wengine wote isipokuwa Chenge wamechenga kusema chochote. (Chenge kakubali kuwa na hisa katika TANGOLD).
Nilikutana na Ruta kwa mara ya kwanza mwaka 2003 nikiwa pale Chuo Kikuu cha Dar. Nilikua kiongozi wa DARUSO na tuliandaa mjadala kuhusu Netgroup Solution, kwanini nchi iingie katik mkataba huu (NETGROUP ulikuwa ni mkataba mbovu pia). Tulifanya mjadala pale Council Chamber, alijenga hoja na kutuacha wote hoi licha ya kujindaa kweli kweli.
Tunaambiwa Ruta ni mmoja wa Bureaucrats wenye uzalendo wa hali ya juu na alie tayari kulinda maslahi ya nchi kwa gharama yeyote. Tunaweza kukubali kuwa Ruta alipinga IPTL, lakini IPTL bado ipo na nchi inafujwa.
Kakubali kuwa na hisa katika TANGOLD, kwa niaba ya serikali. Uchunguzi unaonesha kuwa TANGOLD ni monster. Kampuni hii imehusika moja kwa moja na wizi wa fedha za umma katika Benki Kuu. Mzalendo Ruta anakaa katika bodi ya kampuni hii. Anasemaje juu ya hili.
Rafiki yangu mmoja aliniambia, jamani mmekosea kumtaja Ruta. Ni mwadilifu! Dkt. Slaa, hana tatizo lolote binafsi na watu waliotajwa. Ametimiza wajibu wake na alitoa mwezi mzima kwa serikali kuact, wakadharau. Orodha iliyotolewa ni orodha iliyofanyiwa kazi vya kutosha na wala haikuwa na lengo la kumwonea mtu. Rutabanzibwa, ambae anaonekana kutetewa na watu wnegi sana hapa nchini, ni vema aseme ni vipi ahusishwe na uporaji wa nchini.
Ikumbukwe kuwa katika orodha hii kuna mafisadi wa moja kwa moja na wale waliotumia mamlaka yao ya umma.
A. USHIRIKI WA MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI
Katika kundi hili wamo viongozi na/au maafisa wa umma na/au mawakala na/au washirika wao katika sekta binafsi ambao kwa namna mbali mbali wameshiriki katika kupora utajiri na/au fedha za umma na hivyo kulisababishia taifa na umma wa Watanzania ufukara na/au umaskini mkubwa.
B. USHIRIKI KATIKA KUTOA MAAMUZI YA KIFISADI
Katika kundi hili wamo viongozi wa umma ambao kwa kutumia nyadhifa na/au vyeo vyao katika utumishi wa umma wamefanya maamuzi ambayo kwayo taifa limepoteza mapato na/au utajiri na rasilmali zake na kuwaneemesha raia na/au taasisi za kiuchumi na/au za kibiashara za kigeni. Kwa mfano, viongozi wa umma walioshiriki katika kusaini mikataba mibovu katika sekta za madini na/au nishati na/au maeneo mengine yenye umuhimu mkubwa kwa maisha ya taifa na jamii ya Watanzania.
Patrick Rutabanzibwa atajwa kama ntu aliyetumia madaraka yake vibaya kuingia mikataba mibovu na kushindwa kuizuia. Ruta aweza kuwa safi, lakini analo la kujibu kwa Watanzania.
Tumjadili Patrick Rutabanzibwa, Katibu Mkuu wa zamani (1997-2006) wizara ya nishati na madini na Katibu Mkuu wa sasa wa Wizara ya Maji.
Lissu ndie alieandaa list hiiHili Kaburi limefikuliwa kwa sababu gani?😄😃😆😀
hatari sanaLissu ndie alieandaa list hii
Watanzania tu wajiga kweli, pamoja na ufisadi wao bado tunawashangilia