List ya sanamu ndefu zaidi hapa duniani

List ya sanamu ndefu zaidi hapa duniani

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Orodha hii ya sanamu ndefu zaidi inajumuisha sanamu zilizokamilishwa ambazo zina urefu wa angalau 100 m. urefu katika orodha hii hupimwa hadi sehemu ya juu zaidi ya kielelezo cha binadamu (au mnyama), lakini haijumuishi urefu wa msingi wowote (plinth), au jukwaa lingine la msingi pamoja na mlingoti, au muundo wowote unaoenea juu zaidi.

download.jpeg


Hii inaitwa statue of unity ipo India ina Mita 240.. Huyo anaitwa Patel
Spring_Temple_Buddha_picturing_Vairocana,_in_Lushan_County,_Henan,_China.png


Hii ya pili ni spring temple Buddha ina urefu wa mita 208 iko China. Laykyun_Setkyar_01_(cropped) (1).jpg

Huyu wa tatu ni buddha mwingine yuko mynamar ina urefu wa zaidi ya mita 129..

Vishwas_Swaroopam_after_completion_of_work.jpg


Huyu ni Shiva anafahamika na wengi India hiyo mita 120
Ushiku.jpg



Ushiku wa japan ana karibia mita 120.

Статуя_богини_Гуаньинь_в_Чанше.jpg



Guishan wa China katengenezewa material ya shaba ana mita 99

MOTHER_OF_ALL_ASIA_-_TOWER_OF_PEACE.jpg


Anafuata bikra Maria huko ufilipino ana mita km 90.
Phra_Buddha_Maha_Nawamin_Sakayamuni_Sri_Wisetchaichan.jpg


Kuna hili great Buddha wa Thailand nalipenda limerembwa kwa kupakwa dhahabu..


images (2).jpeg


Sendai wa huko japan nalipenda hilo sanamu Lina mita zaid ya 100

List ni ndefu ila hayo ndo maarufu zaidi.
 

Attachments

  • download.jpeg
    download.jpeg
    7.6 KB · Views: 1
  • images (14).jpeg
    images (14).jpeg
    35.9 KB · Views: 2
  • images (13).jpeg
    images (13).jpeg
    7.1 KB · Views: 3
Huko yaliko ni mapambo tu ya maeneo hayo au yana matumizi mengine? Ufafanuzi.
 
Huko yaliko ni mapambo tu ya maeneo hayo au yana matumizi mengine? Ufafanuzi.
Kwani sanamu la Askari wa posta Lina matumizi gani.. Hizi ni kama symbol tu ila hayo makubwa pia utalii wanaingia watu mpaka ndani ya sanamu
 
Hapo sawa. Nilidhani ni miungu au kuabudia. Otherwise it's ok.
Sijui kwa upande wa Buddha au yale ya kihindi huenda wanayaabudu me Sina uhakika ila ht km kuyaabudu yatakuwa yale madogo yaliyopo kwenye temple zao
 
Sijui kwa upande wa Buddha au yale ya kihindi huenda wanayaabudu me Sina uhakika ila ht km kuyaabudu yatakuwa yale madogo yaliyopo kwenye temple zao
Ok. Ila lugha uliyotumia kwa sanamu boresha kidogo. Mfano "anaitwa"; "ana urefu"; "yuko"; etc. hivyo (and similar ones) ni viwakilishi vya nafsi hai au zilizowahi kuwa hai usually binadamu na wanyama.

Sanamu linawakilishwa na "i"; "li"; e.g. iko/liko India; i/linaitwa; etc. Tuienzi lugha yetu.
 
Cleopatra ?
Ile ya Mwalimu Nyerere aliyochonga yule bwanamdogo sijaiona pia.
 
Back
Top Bottom