Mathayo 7:1 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.
Luka 6:37 Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa.
Yohana 7:24 Basi msihukumu hukumu ya macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki.
1 Wakorintho 4:5 Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.
Barikiwa. sana sana wasaidie wafike mbinguni kwa kuwaombea.