List za biashara au fursa

k
Una simu ya smart phone ya 250,000 afu unasema tatizo mtaji na wakati wengine walianza na mtaji wa elfu 20, jitazame kwanza unaresource gani na apo ndio pa kuanzia
ama arithishwa je? usiseme kitu usicho kijua.
 
ngoja ni reply ili nikipata pesa nirudi huku kuchagua biashara maana nimesoma zipo nyingi hadi nimesahau mtaji wa kwanza umeandika ni upi?
 
 
Asante sana Mleta mada, umetoa mwanga kwa watu wengi sana humu JF.
Kuna baadhi ya watu wanasema tatizo kwao ni kupata mtaji wa kuweza kuanzisha hizo biashara, sasa ngoja nitoe ufafanuzi kuhusu hilo.

MTAJI.
Ni kitu chochote kile kinachoweza kutumika kama dhamana ya kuanzishia biashara. Kitu hicho sio lazima iwe ni Pesa iliyopo mfukoni mwako. Narudia tena kusema, Mtaji sio lazima iwe ni Pesa iliyopo mfukoni mwako. Mtaji unaweza kuwa Muda, Watu, Fursa, Dhamana, Akili, Uaminifu, Kufahamiana na Watu(Connection), Mkopo, Kiwanja, Gari, Nyumba, Elimu, Akaunti ya Benki, Ajira, Kipaji, Marafiki, Imani, Vyeti, Nguvu, Simu ya mkononi, Kompyuta, Samani, shamba, Luninga nk.

Watu wengi wanaopenda sana kusingizia kuwa hawana Mitaji ya Pesa ya kuanzishia biashara basi ukichunguza vizuri utagundua haya...
1/Hawajahi kufanya biashara kabisa.
2/Ni waoga wa Fursa.
3/Ni wachaguzi wa fursa tu(Wanafirikia biashara nzuri ni ile inayovutia masikioni mwa watu na kupata sifa).
4/Wanawaza mambo makubwa tu wakati haiwezekani kwa wao kuyafikia mambo hayo kirahisi au kwa muda mfupi.
5/Wanaamini kuwa kufanikiwa kwa biashara ni matokeo ya kuwa na mtaji mkubwa wa Kipesa.
 
Sijaweza kuzipitia fursa zote. Ila nilipotumia teknolojia kusearch 'Dalali' sikupata results... Kwa taarifa yako, hakuna biashara inalipa kama Udalali. Pia nimesearch kubet, sijaona kama umeiorodhesha. Kubet inaonekana kuwa ni fursa nyingine...
 
nafundisha tuition hapa, aisee natumia masaa mawili tu per day kupata mshahara wa doctor.
 
Sijaweza kuzipitia fursa zote. Ila nilipotumia teknolojia kusearch 'Dalali' sikupata results... Kwa taarifa yako, hakuna biashara inalipa kama Udalali. Pia nimesearch kubet, sijaona kama umeiorodhesha. Kubet inaonekana kuwa ni fursa nyingine...
Kubet fursa ya wavivu wa kiutendaji na hata kufikiri...
 
Safi saana kaka kwakutokuwa na ubaguzi wowote kwa maelekezo yako mazuri, ubarikiwe Sana, give up
 
Zipo poa sana...
 
kama una malengo na duka la vifaa vya simu watafute hawa jamaa wanajiita Jumlasupply blog wanauza mtandaoni kwa jumla tu,unachagua bidhaa unajaza cart yako kisha unaprocess invoice,unatumiwa muda huo huo wanakuletea ulipo
Wanaitwa je?
 
Aiseee umeweka list vizuri.Kuanzia mwezi huu,naweka tai pembeni na vyeti nafungia kabatini nakamata 120.Ngoja sasa hivi nielekee misitu kujua taratibu za vibali,subirini mrejesho.
Mwisho mwezi wa 7 mkuu kuanzia hapo ni magenɗo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…