Listening Audio Booth:John Malecela: Alichoongea

Mjue John Samwel Malecela.
Akiwa Waziriwa Mawasiliano na Uchukuzi, jibu lake kwa waliolalamikia usafiri wa gari moshi ulikuwa, "you can go te hell" akiwa na maana waende kuzimu.

Aliwakasirisha Wagogo wenzake alipowakandia kwa kuwa ombaomba Dar es Salaam na majibu yao kwake ilikuwa ni kumkataa aliporudi kwao kuwaomba kura ya ubunge.

Akiwa Waziri Mkuu kwenye serikali ya Raisi Ali Hasan Mwinyi, jibu lake kwa wastaafu wa iliyokuwa EAC ilikuwa ni, "walie tu, hawapati kitu ng'o"

Akiwa Waziri Mkuu, jibu lake kwa waliodai mfumo wa vyama vingi ilikuwa ni kuwafananisha na sisimizi huku Waziri wa Mambo ya Ndani Augustino Lyatonga Mrema, akiwaita hamnazo. Bila Mwalimu vyama vingi vingebakia ama ndoto Tanzania au vingepatikana kwa damu.

Akiwa Makamu wa Mwenyekiti wa CCM aliwahi kudai kuwa wanaoipinga CCM wangeachwa kwenye mataa.

Akiwa mgombea wa Uraisi baada ya jina lake kuachwa kwenye mataa, wengi tunajua alivyolalama kwa pembeni na kichini chini.

Leo hii anathubutu kuwabeza wanaokemea UFISADI ndani ya CCM na kutaka magazeti yathibitiwe - hana jipya, analinda maslahi.

Huyu ndiye Malecela ambaye baada ya kushiriki katika mchakato wa ugawaji mali za EAC, aliteuliwa kuwa balozi Uingereza ilikotunzwa mafao ya wastaafu. Baada ya hayo mafao kutafunwa chini ya awamu ya pili na baada ya Mwalimu kung'atuka uenyekiti CCM, alimegewa jimbo aweze kugombea mwaka 1990 na baadaye kuteuliwa Waziri Mkuu. Hivi sasa si ajabu kumsikia akianza kampeni zile zile za mwaka 47 - hivi tujiulize kitu gani kinamsukuma safari hii.
 

“Nyawabhisa bhisa bhurwae ekiriro kirimubhura.” J.K. Nyerere
 
Lugha za kibantu zinafanana, ona hapa

Nyawabhisa bhisa bhurwae ekiriro kirimubhura
Anayeficha ficha ugonjwawake kilio kitamuumbua

Just a lucky guess based on phonetics.
 
Naomba source ya hicho kitu ulicho kinukuu!

Na, tafadhali kije kama ulivyo kinukuu.

FMES kaomba Wazanaki waandike kwa Kizanaki, sasa mkuu unajuaje kama si mmoja wa wazanaki wanaoingia hapa?
 
FMES kaomba Wazanaki waandike kwa Kizanaki, sasa mkuu unajuaje kama si mmoja wa wazanaki wanaoingia hapa?

Okay,

Kwa hiyo source ni wewe mwenyewe kwa sababu wewe ni Mzaneki.

Maana yake nini huo msemo?
 
Okay,

Kwa hiyo source ni wewe mwenyewe kwa sababu wewe ni Mzaneki.

Maana yake nini huo msemo?

Mficha ficha ugonjwa/maradhi kilio kitamuumbua.

**Kwa upande mwingine maana ya moja kwa moja ya neno kubhura ni kushitaki au waswahili wanasema kusemea kwa mfano nilikubhura-nitakushitaki/kusemea.
 
Last edited:
Nadhani tafsiri ni yake,ila hapo kwenye source kuwa yake wakati aki mquote mwalimu bado ni lazima iwe kwamba Icadon alikuwepo wakati wa hotuba hiyo ili kuweza ku justify hilo...Kwenye tafsiri kuwa yake pia itabidi tuamini kuwa na yeye ni Mzanaki ama anazungumza kizanaki.
 
Kwa upande wangu sijaona jambo la maana ambalo mzee malecela ameongea.
Sana sana ametaka umaarufu wa kuwaita waandishi wa habari.

Malecela kwa umri aliokuwa nao, uzoefu na usomi wake amekimbia kuongelea jambo la msingi badala yake ametoa vitisho na amri kama tuko jeshini. Sikutegemea kusikia upuuzi kama ule toka kwa mkongwe wa siasa.

Amekubali kwamba kweli kuna tatizo la viongozi kutupiana maneno kwa kupitia vyombo vya habari. Angejaribu kulielezea tatizo lenyewe kiundani na chimbuko lake then ndipo angekuja na solution nini kifanyike kutatua tatizo hilo. Huwezi kuanza moja kwa moja na solution bila kujua tatizo nini na limetokana na nini. Malecela amesema malumbano yakome, sasa ni malumbano gani?, yameanzia wapi?, kwanini yameanza nk.

Baba unapokuta watoto wako wawili wanapigana ndani ya nyumba pamoja na kuamulia ugomvi wao ni lazima utafute chanzo cha ugomvi wao, nani mchokozi, kwanini alichokozwa/chokoza then unaweza kupata mwanga mzuri wa kutatua ugomvi huo ili hata huko mbeleni watoto wasije kupigana tena.

Alichofanya Malecela ni sawa na kuchukua kitambaa na kufunika jipu lililoiva ili lisitoe usaha. Dawa ni kukamua jipu hilo kwanza, kupaosha kidondani then unaweza kufunika ili inzi wasiweze kukupa taabu.

Ukweli anaujua vyema lakini anajaribu kuficha ukweli ili suala hili liishe haraka vichwani mwa Watanzania.

Ni mtanzania gani asiyejua kama CCM ya leo imetekwa na wenye pesa?. Ukitaka kupata madaraka kwa haraka na unazo pesa basi peleka pesa yako CCM na madaraka utayapata mara moja. Inasikitisha sana kuona kwamba CCM imebakia jina tu kwenye ganda (jarida la kitabu) lakini kitabu chenyewe ndani si CCM (hapa nina maana kwamba ni sawa na kuwa na jarada la kitabu linaonesha kwamba ni kitabu cha Biology, kumbe ndani ni kitabu cha methali za kiswahili).

Watanzania wenzangu tunategemea kitu gani kipya kwa watu kama Malecela ambaye amekuwa madarakani miaka nenda miaka rudi na hakuna chochote cha maana alichofanya?. Nchi imefika sehemu mbaya na mchango wa malecela pia upo katika kutufikisha hapa tulipo.

Tunadanganywa na kauli ya "Tanzania ni nchi ya amani". Tusiwe wajinga nchi inaliwa na inaibiwa vibaya sana na kundi la wachache kwa kivuli cha CCM. Wananchi wengi ni masikini na watumwa ndani ya nchi yao. Tuamke kwa pamoja na kudai haki yetu bila kuona haya kuwaonea haya wahusika.

Ni mtanzania gani mwenye akili timamu atapenda tununue mitambo ya Dowans?, kampuni ambayo ni kivuli?.

Hivi ni kweli tunaweza kukubali kwamba wahusika wa KAGODA hawajulikani?. Inawezekana vipi ukachota bilioni 40 na kumpa mtu asiyejulikana?.

Malecela amenipandisha hasira zaidi pale alipomsifia kikwete na safari zake za kuomba kuomba nchi za nje. Sisi si masikini hivyo mpaka raisi wetu azunguke na bakuli kuomba kuomba. Tunachokihitaji ni usimamizi mzuri wa mali zetu ama kile tukipatacho na tuwe na vipaumbele.

Unakwenda kuomba $200m za kuchimba kisima cha maji na wakati huohuo unatumia $800m kuwanunulia viongozi magari ya kifahari (mashangingi), what is wrong with us?. Na mzee malecela bila aibu anasifia kitendo kama hicho?. Ama kweli mgogo kuomba jadi yake.
 
 

- DK. Malecela, amesema anamtaka Rais wa sasa Kikwete aendelee na urais, na wewe sasa sema kwa nini humtaki Rais Kikwete na kwamba unamtaka mgombea mwingine, mimi, wewe, na yeye kama wananchi wa Tanzania wote tuna haki sawa ya kusema wazi mgombea urais tunayemtaka, kama unaweza pingana na hoja yake lakini umri wake hauna anything to do na chaguo lake la nani awe rais.

- Acheni kujishusha hadhi na hoja finyu, huu ni uwanja wa great thinkers ambao hatutafuti njia za mikato na matusi na kejeli kwa wazee eti kwa sababu ni wazee, ndio maana wananchi wa Tanzaania mpaka leo wanaogopa sana upinzani kutokana na hoja kama hizi, sasa kama mimi ni mpiga kura mzee ninmeingia hapa unafikiri kweli nitatoa kura kwa upinzani badala ya upande wa mzee mwenzangu Malecela?

- Sometimes muwe mnafikiri japo kidogo effect ya maneno mnayoandika hapa kuwa yanafika mbali sana kuliko mnavyofir, mimi sio member wa CCM sasa nitakoseshwaje usingizi na mambo ya dnani ya chama ksichokuwa changu?

Wazee wa sauti ya umeme FMES!

 
Ni afadhali hata sijaweza kuisikiliza hotuba hiyo,based on the scripts ni wazi mafisadi wanatumia watu flani flani kujaribu kwa kila namna kujisafisha.....Hilo halina ubishi,ama kweli mpambano huu ni mgumu na tutaona mengi sana,karata ya mzee sidhani kama itafanya kazi na hawezi kuplay za ubaba wa Taifa kwa mtiririko huu,ukisoma kwa makini utagunduwa mzee ameongea kama amekurupushwa flani hivi licha ya kwamba anajaribu kuwa above the frey kama Mwalimu,bado yuko na mafisadi pamoja,kauli kwamba udaku na magazeti viemezidi bongo bila ku acknowledge kuwa vyombo vya habari vimetusaidia kupambana na ufisadi wa ccm yenyewe na bado mpambano unaendelea ni ukosefu wa fadhila kwa wazalendo wapenda Taifa lao ambao hawajashiriki kutufikisha kwenye jalala tulilomo....Ni wapi hapo aliposifia juhudi hizo za kupambana na ufisadi? Sana sana ametumia lugha nyepesi na mchosho kuwa ni lazima wafikishwe mahakamani na si kutuhumiwa kwenye vyombo vya habari...Sasa hizo tuhuma za kwenye vyombo vya habari anavyoviponda si ndizo ziliwafikisha baadhi ya mafisadi mahakamani na pia kuepelekea mijadala mikali bungeni? Ama alikuwa analala wakati wa mijadala na hata mkewe alipokuwa mkali kuhusu mizengwe?

Kaahidiwa nini na JK huyu mzee? Mimi kaniudhi sana huyu mzee,kwanza maneno aliyoyazungumza tayari mkewe mama Kilango alishayazungumza,sasa na yeye ni mzee wa ku copy and paste ama anadharau kazi za mkewe kwamba hakusikilizwa ama hasikilizwi?

Alichosema mkewe juzi ni kuwa habari hizo za kina Mwakyembe zirudishwe bungeni na si kwenye chama,yeye kaja karudia yale yale at the same time akionekana kuwa alijiamkia zake asubuhi na kuamua na yeye akazungumze,na alichosema kina prove beyond imagination out of touchness....Kuzi group habari za udaku na zile za ufisadi na kuzi categorize kuwa ni upuuzi kumepelekea mimi kuona kuwa ccm wasipokuwa makini wataliingiza taifa hili matatani....Ni blind politics zinazosababishwa na recklessness,missjudgements,out of touchness na carelessness....Eti watakao chukuwa fomu watakuwa wamepoteza muda wao na pesa kwasababu yeye hachajukuwa...What a dissgrace.

Malecela: Ni Kikwete tu 2010

2009-03-26 12:38:03
Na Joseph Mwendapole

Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, John Malecela, amesema kuwa mwanachama yeyote wa CCM atakayejitokeza kuchukua fomu kupambana na Rais Jakaya Kikwete katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, atakuwa anapoteza muda wake.

Yeye binafsi ameweka msimamo wake wazi kuwa hatajitokeza kuchukua fomu kugombea kiti cha urais mwakani tofauti na alivyofanya mwaka 1995 na mwaka 2005 na jina lake kuondolewa na vikao vya Kamati Kuu (CC) ya chama hicho.

Alisema mwanachama wa CCM mwenye fikra hizo ni vyema akazifuta mapema na atumie fedha ambazo angetumia kwenye kampeni za urais kuendeleza familia yake.

Aliyasema hayo jana nyumbani kwake Sea View, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari vya IPP.

Alitoa jibu hilo baada ya kuulizwa iwapo atawania urais mwaka 2010 baada ya jina lake kuchujwa katika kinyang`anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

``Rais Kikwete ameifikisha nchi sehemu nzuri sana, hakuna wa kumpiku, ametuendesha vizuri tangu tumpe usukani mwaka 2005 na lazima wananchi na wanachana wa CCM wajue kuwa mwaka 2010 ni kituo tu Kikwete hajafika mwisho....mwisho wake wa urais ni 2015,``alisema na kuongeza kuwa yeye hatagombea urais badala yake ataendelea kuwania ubunge katika jimbo lake la Mtera, mkoani Dodoma.

Alipoulizwa kuhusu dhamira yake kutokana na kuondolewa na Kamati Kuu (CC) ya chama hicho katika kinyang`anyiro cha urais mwaka 2005 na kuamua kukata rufaa Halmashauri Kuu (NEC), alisema hadi sasa hana kinyongo.

Alikemea malumbano yaliyotokea hivi karibuni baina ya Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz, na Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe, kuhusu mjadala wa ununuzi wa mitambo ya Dowans.

Alisema wakati huu wa hali mbaya ya kiuchumi, viongozi wanapaswa kuweka mikakati ya kumsaidia Rais Kikwete ambaye amekuwa akiizunguka dunia kutafuta misaada ya Tanzania, badala ya kuendekeza malumbano.

Alisema badala ya kulumbana hadharani, wanapaswa kupeleka masuala hayo katika Bunge, Serikali au katika chama.

``Kwa kweli tumechoshwa na malumbano haya, hakuna sababu ya kuendeleza malumbano kwani kama suala linahusu serikali kwanini lisipelekwe huko likajadiliwa?

Kama ni la Bunge, kwanini lisipelekwe bungeni? na kama ni la chama kwanini lisipelekwe kwenye chama mpaka watu wanasutana katika magazeti,`` alihoji Malecela ambaye pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais kuanzia mwaka 1990 hadi 1995.

Alisema lipo kundi la watu wanaojidanyanga kuwa ipo siku CCM itameguka endapo watajitoa katika chama na aliwataka kufanya hivyo haraka iwezekanavyo.

Alisema hata wakiondoka chama kitabaki imara na hakitatetereka.

``Baba wa Taifa aliwahi kusema kuwa bila CCM imara nchi itayumba, lakini hakumaanisha kuwa chama hiki kitameguka, sasa hao ambao wamekuwa wakitoa vitisho kila kukicha kitameguka ni heri waondoke tumechoka na vitisho vyao,`` alisema.

Alisema CCM haitakubali watu wachache waruhusiwe kuiyumbisha nchi kwa sababu wanazojua wao.

Vile vile, Malecela alisema kamwe CCM haitaruhusu matajiri kuongoza chama hicho na kwamba wanaojaribu kufanya hivyo wanajidanganya.

Alisema chama hicho kitaendelea kuwa chama cha wanyonge na wafanyakazi.

Kuhusu mjadala wa Dowans, Malecela alisema ni sawa na kuchapa bakora mzoga kwani suala hilo lilishajadiliwa na kumalizwa na Bunge.

Alisema anayeona mjadala huo unamaana tena anaweza kuwasilisha hoja yake bungeni.

Kuhusu madai ya wizi wa fedha za umma zinazomwandama Mbunge wa Bariadi (CCM), Andrew Chenge, Malecela alisema hizo ni tuhuma tu na kwamba Mahakama pekee ndiyo yenye uwezo wa kumtia hatiani.

Alisema mtu yeyote anaweza kutuhumiwa hivyo haoni ajabu kwa yanayosemwa kuhusu mwanachama huyo wa CCM.

``Watuhumiwa wako wengi hapa nchini na hata wewe unaweza kuwa mtuhumiwa wakati wowote tu na kisheria mtuhumiwa hana hatia mpaka Mahakama itakapomwona na hatia,`` alisema.

Wakati huo huo, Malecela, ameishauri serikali iyafunge magazeti ambayo yamekuwa yakiandika uongo na mambo binafsi dhidi ya watu mbalimbali.

Alisema magazeti hayo yanakosa habari na badala yake yanaandika uongo na uzushi.

``Imefika wakati sasa serikali ifanye kazi yake...magazeti haya sasa yamekuwa mengi mno na yamefikia hatua mbaya ya kuandika mambo ya uongo,`` alisema Malecela.

Aliongeza kuwa serikali isiendelee kuyafumbia macho na kwamba lazima ionyeshe kuwa haikubaliani nayo kwa kuchukua hatua madhubuti ikiwa ni pamoja na kuyachuja.

Alisema mpaka sasa ripoti zinaonyesha kuwa Tanzania ina magazeti mengi kuliko nchi yoyote barani Afrika.

``Imefikia wakati yanaingilia mambo ya watu binafsi ya ndani kabisa na kuyachapisha..lazima tujiulize haya yanafanyika kwa faida ya nani?`` alihoji.

Aidha, alisema kuwa anaamini vyombo vya habari vimeanzishwa kwa ajili ya kuelimisha umma na si kuandika uongo na kuendeleza malumbano.

Alitahadharisha kuwa hali hiyo ikiendelea, wananchi wanaweza kudhani kuwa uhuru wa vyombo vya habari ni watu kutukanana na kukashifiana.

Hivi karibuni, kumeibuka kundi la magazeti ambayo yamekuwa yakishambulia watu wanaopambana na ufisadi.

Magazeti hayo yamekuwa yakiandika habari za uongo na za kutunga dhidi ya watu wanaomuunga mkono Rais Kikwete katika kupambana na vitendo vya ufisadi.
  • SOURCE: Nipashe
Tuma Maoni Yako
 

Mkuu FMES nilikuwa namheshimu sana mzee Malecela lakini amenikatisha tamaa kabisa especially kutumia heshma yake na kujaribu ku neutralize vita ya ufisadi..Mkuu mzee huyu alikuwa kimya sana,lakini sasa anatokeza na kuwatetea watuhumiwa wa ufisadi na kuviponda vyombo vilivyofichua ufsiadi simply because kuna habari nyingine anazoziita binafsi zimechapishwa na kwamba eti ni tuhuma tu...Mkuu what is that? Ni mara mia aachie vijana kazi sasa apumzike.
 

- Hakutetea ufisadi unless tumesikiliza sauti tofauti, ametoa maoni yake na wewe unaweza kutoa ya kwako, wewe ukiona kuna ufisadi CCM sio lazima na mimi niuone huo ufisadi especially kama hakuna ushahidi kama alivyosema.

- Ishu ya Lowassa na bunge mapka leo bado ni tatizo kwamba ameonewa na kuna valid arguments hapa Jf kila siku kuhusu hilo, sasa ndio maana watu makini kama yeye wanakuwa carefully na wanachokisema maana bila ushahidi tena mtu kama yeye itakuwa aibu mkuu.

- Ni haki yako kutoa maoni yako as nani unataka awe rais next kama yeye alivyo nayo au kwa kuwa yeye ni mzee hatakiwi kuwa nayo? hivi kwani bado ni kiongozi wa taifa? Au unawazungumzia wananchi wa jimbo lake na wewe ni msemaji wao?
 

Kama hukumbuki sawa - kusahau si kosa lakini kujaribu ku"spin" ni kitu kingine kabisa !! Usimsingizie Marehemu tafadhali.

- Wagogo omba omba wamekuwa siku zote wakihudumiwa sana na ndugu wawili Balozi Lusinde na DK. Malecela, ingawa Balozi Lusinde ndiye alikuwa akiwasaidia zaidi kutokan na DK, kutokuwepo Dar kwa muda mrefu, akiwa nje na Arusha.

Kwa nini alinyimwa kura ? Waziri mzima !!


Alikuwa anaongelea wagogo kwa ujumla wao, hayo ya Chinolwa ni yako.


Mwaka 1991 wastaafu walipopata angalau uwanja wa kutoa madai yao, tamko la kwanza kabisa la serikali lilikuwa kuwakana. Lilitolewa na Waziri Mkuu, John Samwel Malecela akisisitiza kuwa wastaafu hawakuwa na madai yoyote kwa serikali - rejea matoleo ya magazeti ya mwaka 1991. Serikali ilienda hatua moja zaidi kwa kupiga marufuku mikutano ya hawa wastaafu kama kuzuiwa kukutana Klabu ya Sigara, Changombe (1992) - ikabidi wakutane kisiri siri barabarani karibu na uwanja wa taifa.


Waziri Mkuu, John Samwel Malecela, akiwa kwenye ziara mikoa ya kusini alitamka hadharani kuwa wanamageuzi ni kama sisimizi na akasema serikali ya CCM ingewakanyakanyaga kama tinga tinga. Kama wewe hukumbuki, wengine tuna kumbukumbu nzuri tu - hebu ajaribu kukana. Ni wakati huo huo Mrema naye alidai wehu tu wangeingia upinzani.

- Akimaanisha Mrema, Lipumba, na Seif, ambao toka watoke CCM mpaka leo wameachwa kwenye mataa na urais walioutaka na wanaoutaka bado.

Alikuwa nadhihaki wote wale kama anavyodhihaki sasa hivi wenye nia ya kumeguka. Anachosahau ni kuwa mambo yamebadilika - wakati huu huyo unayesema utamwacha kwenye mataa huenda ndiye kakuacha kwenye mataa.


Maslahi yako guaranteed as long as CCM iko madarakani, period. Utawala wa sheria utakapokuwapo, majizi na mafisadi hayatapata pa kujificha - na mali walizochuma hazitakuwa salama.

- Hapana uongo tena mkuu, baada ya ugawaji mali EAC, alikwenda Commonwelath, baad ya kumaliza alirudi na kuwa RC Iringa, na ndio akaenda kuwa balozi london. Acha uongo mkuu tena ni aibu kwa wewe mtumzima kusema uongo mchana namna hii!

Hebu rudia niliyoandika, alikuja kuteuliwa kuwa balozi wakati wa Mwinyi - sasa uongo wangu u wapi ?


Fedha za wastaafu hazikuwa na mahusiano yoyote na madeni. Fedha za wastaafu zilitokana na makato ya mishahara yao na wala hazikuwa fadhila za serikali ya Tanzania. Serikali ilikabidhiwa hizo hela iwalipe wahusika na sio kuzitafuna kwa majumba ughaibuni.

- Tizama uongo huu, amepewa uwaziri mkuu hata kabla hajwa mbunge, alipokuwa balozi London na kuja kuwa waziri mkuu hakuwa mbunge mkuu, mbona unasema uongo mtupu mkuu na wewe unatetea masilahi gani na huu uongo?

Kama aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu kabla ya kuwa Mbunge 😕..... Hata hivyo ukweli ni kuwa alimegewa jimbo na likaitwa Mtera.

- Wewe unasukumwa na nini na hizi kampeni za uongo wa mchana ndicho hasa tunatakiwa kujiuliza! Next time mkuu tafuta facts, badala ya kudnika uongo wa kitoto kama huu!

Mimi nawaachia wengine waamue maanake nikianza kukuita muongo sitatofautiana sana na wewe.

Respect
FMES wazee wa sauti ya umeme. [/SIZE]

Kazi njema katika utetezi - lakini ufisadi ulianza zamani tu.
 

- Angalau this time umeongea facts tupu, bwa! ha! ha!

FMES.
 
Uchambuzi wa uchaguzi wa mwakani ....kikwete atashunda..,lakini siasa za makundi alizoziazisha mwaka 2005 yeye mwenyewe zitazidi kujionesha dhahiri,kwani hata kampeni kuna uwezekano mkubwa kutengwa ..na akabaki anapigana yeye na mtandao wake mpya....

Kama itakuwa hivyo ni wazi kikwete atakuwa na kazi kubwa na ngumu ambayo inaweza kumshinda ya kuunganisha ccm kwa mwaka 2015......kufikia wakati huo nguzo alizoelekea kuziegemea kwa siku za karibuni zitakuwa zimezama au kukosa nguvu hata ya kusimama,ni wakati sasa wa kikwete kutoa mkono wa suluhu kwa aliokosana nao 2005....kwa faida ya ushindi wa ccm mwaka 2015...kwani ushindi wa kikwete mwaka 2010 hautakuwa na maana yoyote kama ataacha nchi ikiwa na makovu yasiyotibika ...yenye dalili za siasa za chuki,maji taka , na kukomoana!!

KAULI YA MALECELA HAIKUTARAJIWA KWA SASA....na kila mtu atajiuliza kweli huyu ni malecela anamtetea kikwete?????...basi kweli siasa haina fomula!.........lakini huyo ndiye MALECELA HASWAAA....hata mwalimu alikuwa akimpenda sana ...tatizo lake moja tu walilokuwa wakitofautiana na mwalimu ni kuwa MALECELA HUWA HANA MSIMAMO WA KUDUMU!!!!!...BASI!................

na kama malecela ameweza kumsamehe kikwete kwa fitina na siasa chafu alizomfanyia ...basi nampa shahada ya uvumilivu na kusamehe!!!
 

Malecela is a shrewd politician. Anajua kuwa Kikwete kashika mpini na yeyote atakayetaka kwenda against Kikwete, at least in the short term, ana kazi ngumu kwani Kikwete ana dola, na yeyote anayejikombakomba kwa Kikwete anapalilia ustawi wake.

Other than that, he was jsut exercising his "right" to be a senile old man, hajasikika siku nyingi alitaka watu wajue na yeye yupo, hamna chochote worthwile in my opinion alichosema.
 



- Mkuu PM, hapa hutendi haki ni lini wanasiasa waliwahi kuwa na msimamo wa kudumu? Mbona kuna wakati Mwalimu alimtukana sana Kawawa na baadaye akamsifu sana mwishoni akiwa nje ya urais? Yaani kupendwa au kutopendwa na Mwalimu unasema ndio standard ya uongozi bora na kuwa na msimamo kama kiongozi? Sasa what happened to Kingunge aliyekuwa akipendwa na Mwalimu na hakuwahi kutofautina na Mwalimu hata siku moja kama Malecela?

- Malecela anao msimamo mkuu ila labda hutaki kuuona maana kama asingekua nao Lowassa, angekuwa bado ni waziri mkuu kwa mara ya kwanza alimuambia wazi huko CC kwamba atoke, lakini akagoma mwishowe aliishia kutoka tu huku yeye mwenyewe Malecela akimshinikiza rais, against baadhi ya wabunge wenziwe, sasa unasema huu sio msimamo?

- Kuhusu msimamo wake nani awe rais next, ameusema wakati muafaka kama alivyofanya mwaka 2000, pale CCM Lummumba, alipogundua kuwa kuna baadhi ya viongozi wa CCM walikuwa wakifanya mipango ya chini chini kumng'oa Mkapa kabla hajamaliza term ya pili, akasema wazi kwamba anataka Mkapa amalize term ya pili tena wakati kama huu, na this time ameruda tena kwamba anamtaka Rais wa sasa aendelee tena, na wewe unaweza kusema wazi ni nani unamtaka na kwa nini hakuna tatizo hapo mkuu


Wazee wa sauti ya umeme FMES!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…