Sasa kama uongozi wa Nyerere kulikuwa hakuna kiongozi tajiri au mwenye mali basi hata raia nao walikuwa wamekondeana.
Hivi sasa raia wengi wanamiliki nyumba nyingi tu na pia tunakaribia kila nyumba kuwepo na gari ,na uwezo wa wananchi pia unaoenekana kuongezeka ,karibu kila mtu hivi sasa anamiliki simu ya mkononi na karibu wanafunzi na watoto walio chini ya miaka kumi na nne nao watamiliki simu za mukononi ,hivyo kuwajadili wabunge ambao mishahara yao ni minono na inajulikana itakuwa hamuwatendei haki ,maana japo wana mishahara minono inategemea akili ya mtu inavyofanya kazi na uwezo wa kutumia na kupanga matumizi ya hela anayoipata. Au kwa msemo wa kibiashara vipi ataekeza hela anayopata ili izalishe hela zaidi ,ni uwekezaji tu ndio unaoweza kumuinua mtu yeyote yule ,hebu fuatilia story za mabilionea uone ,walivyoanza na mtaji ambao ukipewa wewe haumalizi mwezi hela yote umetafuna. Watu wanajua kufunga mkaja ,msione vinaelea jamani ,huu ni msemo wetu katika lugha.