Lisu Kutia Nia, Kwa Nini Kelele Za Kuchanganyikiwa Zinatoka Zaidi CCM?

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,362
Reaction score
48,879
Jana Tundu Lisu, kwa kutekeleza matakwa, uhuru na haki ambayo chama chake kinatoa kwa wanachama wote, alitangaza nia yake ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Chake Ngazi ya Taifa. Wakati jambo hili ni la kawaida kabisa kwa vyama vyenye demokrasia, huko CCM watu wamechanganyikiwa na kutoa kila kauli ya ajabu dhidi ya nia hiyo ya Tundu Lisu!!

Kwa nini uchaguzi ndani ya CHADEMA, walioonekana kuwashwa na kuchanganyikiwa sana ni CCM na siyo wanachama wa CHADEMA?

Mara kadhaa Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amekuwa akiwakumbusha na kuwaeleza wanachama wa CHADEMA na watanzania kwa ujumla, kuwa CHADEMA siyo ya Mbowe, siyo ya Lisu wala siyo ya Mnyika, ni ya wanachama wote, na watanzania wote. Akimaanisha kuwa kila mwanachama ana haki sawa ndani ya chama, ikiwemo ya kugombea na kuchaguliwa kwenye nafasi yoyote ndani ya chama alimradi ana sifa zinazohitajika.

Ndani ya CHADEMA, hakuna nafasi ya mtu, bali mtu anaweza kushika nafasi fulani ya uongozi ndani ya chama. Lisu ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa chama, hakutangaza kugombea nafasi ya Mbowe. Heche ametangaza kugombea nafasi ya makamu wa mwenyekiti, siyo nafasi ya Lisu.

CCM kwa sababu hawaijui demokrasia, wala hawajawahi kuwa na demokrasia, basi nawaombeni na kuwasihi sana CHADEMA, Mbowe, Lisu na wanachama wote, wafundisheni CCM maana ya demokrasia.

CCM hawajui uchaguzi wa mwenyekiti wa chama, CCM hawajui uchaguzi wa mgombea wa nafasi ya Rais, wao kila mahali wanaprint fomu moja kwaajili kuhakikisha udikteta unakuwa ndiyo desturi na mazoea ya chama. Kwao kinachoitwa uchaguzi ni unafiki mtupu, ubabaishaji na hadaa kubwa kwa wanachama wao. Hili linaweza kuwa ni jibu kwa nini CCM wamehamaki kusikia ndani ya CHADEMA kutakuwa na uchaguzi halisi, walitaka vyama vyote viwe vya kidikteta kama cha kwao.

CHADEMA kutekeleza misingi ya demokrasia kunawanyima CCM usingizi kwa sababu wanaona kuwa CHADEMA itakuwa imepata uhalali mkubwa wa kuusimanga udikteta wa ndani ya CCM. Wangependa vyama vyote viwe na uchafu kama wa kwao katika demokrasia ili vikose uhalali wa kuisema CCM kwa udikteta.

Hongera CHADEMA, hongera Mbowe, hongera Lisu, wafundisheni CCM maana ya demokrasia. Tena waruhusuni hata wanachama wengine wenye sifa kuendelea kutangaza nia ili CCM wazidi kujifunza, wakishindwa kujifunza, basi wazidi kuchanganyikiwa.
 
Kuna wakati CCM walitakaMbowe aachie ngazi!
Walipo muona ni chui wa karatasi wanampigia debe Kwa Nguvu zoote aendelee na Uenyekiti....
 
Front Company ya tisiem imenusa hatari endapo Double Agent ataanguka.
 
Back
Top Bottom