Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Hivi sasa, Lithuania inafanyika uchaguzi mkuu, na uhusiano na China umekuwa moja ya masuala muhimu katika kampeni za uchaguzi. Kwa mujibu wa matokeo ya duru ya kwanza ya upigaji kura, Nauseda aliongoza kwa kupata asilimia 44.19 ya kura zilizopigwa, huku Waziri Mkuu Ingrida Simonyte akishika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 20 ya kura. Tofauti kubwa zaidi kati yao ni kwamba Nauseda anataka kuboresha uhusiano na China, lakini Simonyte anataka kuendelea na sera isiyo sahihi katika suala la Taiwan. Matokeo ya duru hiyo ya uchaguzi yanaonyesha vya kutosha kwamba watu wa Lithuania wana maoni gani katika suala hilo. Kwa kuwa hakuna aliyepata kura zaidi ya asilimia 50, duru ya pili ya uchaguzi itafanyika tarehe 26 mwezi huu.
Mbali na uchaguzi, sababu kuu ya Nauseda kuboresha uhusiano na China ni ya kiuchumi.
Mwaka 2021, bila kujali upinzani mkali wa China, serikali ya Lithuania ilitangaza kuruhusu mamlaka ya Taiwan kuanzisha kile kinachoitwa “ofisi ya uwakilishi” huko Vilnius, mji mkuu wa Lithuania, ikitumia jina la Taiwanese, badala ya “Taipei” ambalo linatumiwa na nchi nyingine. Kutokana na kitendo hicho cha kudai Taiwan ni nchi huru, China ilishusha moja kwa moja kiwango cha kidiplomasia na Lithuania, na kusitisha ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya nchi hizo mbili.
Katika miaka mitatu iliyopita, wanaviwanda nchini Lithuania wamekuwa na wakati mgumu sana kutokana na makosa ya serikali ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Lithuania, sio tu makampuni ya nchi hiyo hayawezi kuuza bidhaa zao kwa China, bali pia bidhaa zilizo na vipuri vilivyozalishwa nchini Lithuania pia haziwezi kuuzwa nchini China. Licha ya hayo, wakulima pia wameathirika. Mwaka 2022, Idara Kuu ya Forodha ya China ilitangaza kusimamisha kushughulikia maombi ya kuagiza nyama ya ng'ombe kutoka Lithuania. Jambo hili limeathiri maslahi ya moja kwa moja ya zaidi ya watu 400,000, ambapo jumla ya wananchi wa nchi hiyo ndogo ni zaidi ya milioni 2 tu.
China ina watu wengi na soko kubwa, na ni nchi kubwa zaidi duniani kwa ukubwa wa biashara na viwanda. Kwa hiyo, baada ya China kufunga mlango wake wa kibiashara kwa Lithuania, mauzo ya bidhaa za Lithuania kwa nje yalipungua mara moja kwa asilimia 70. Mbali na biashara, kampuni nyingi za kimataifa zilizowekeza nchini Lithuania zina wasiwasi wa kuathiriwa na mzozo kati ya Chian na Lithuania, na zimeamua kupunguza au kuondoa uwekezaji wao kutoka Lithuania.
Ikiwa nchi ndogo yenye idadi ya watu milioni 2.8 tu, hivi sasa Lithuania inabeba mzigo mzito wa madeni ya nje kiasi cha dola bilioni 47 za Kimarekani, na hata inashindwa kumudu riba ya madeni hayo. Marekani ambayo ilichochea mzozo wa Lithuania na China, haikutoa chochote ila mkopo wa dola milioni 600 za Kimarekani, lakini mkopo huo unahitaji kulipwa pamoja na riba. Wakati huohuo, Taiwan, ambayo iliahidi kuagiza bidhaa zote za Lithuania zilizoachwa na China sasa imebaki kimya.