Litre ya diesel

Litre ya diesel

majiyashingo

Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
44
Reaction score
2
Jamani waungwana hapa jamvini nimerudi tena.

Hivi juzi juzi nimenunua lorry la tani 10 ambalo linafanya kazi zake kuanzia saa moja asubihi hadi saa 12 jioni? Huwa linapumzika mchana tu pale dereva anapopata kifungua mchana mimi kwa kifupi sina utalaamu sana na magari nimepata dereva ila namuona mjanja mjanja kidogo Je disel ya shilingi 75,000/-anaweza kuitumia siku nzima?

Na kidogo humu kuna wataalamu wa mambo hayo je ili anitunzie gari yangu fresh mnahisi mshahara gani nimpatie kutokana na maisha yetu hapa ili mimi wala yeye tusinungunike.

Natanguliza shukrani
 
Mkubwa kweli maji ya shingo yamekufika kama jina lako, dereva mjanja na wewe uko gizani kwenye magari :A S 13:!!! Ila all in all unywaji wa mafuta wa magari unategemea vitu vingi sana... kwa ufupi tu upya na ukubwa wa engine ya gari lako; kama inatembea tupu au ina mzigo na uzito wa mzigo wenyewe; umbali unaotembea; spidi linalotembelea; hali ya barabara linalotembelea n.k. Mkuu kweli kama huna kabisa idea ya magari huwezi kukwepa kulizwa na huyo dereva wako... cha msingi jaribu kukaa nae muelewane vizuri ili kila mmoja afaidike kwa upande wake lakini kumbana dereva wakati wewe haujui chochote kuhusu magari ni ngumu kidogo!!!!
 
Kaka nadhani maelezo ya gari haya hapa gari ni mpya

Chassis model
 
EQ5140KLJ1
Real volume
T
15
Total mass
Kg
14490
Curb mass
8000
Rated mass
6295
Vechicle size
mm
 
8650×2480×3100
Wheelbase
5000
Tyre size
10.00-20
Displacement/power
ml/ps
5900/140
Engine
Diesel engine
Max speed
 km/h
85
 
Mkuu! Fahamu kuwa kiasi cha 75000 ni kununua lita karibu 40 za diesel. Kwa wastani magari makubwa (kulingana na tonnage) husafiri km hadi 6 kwa lita. Hapo ni kwa mwendo wa 80km/hr na kwenye barabara isiyo na milima akitumia gea ndogo. Kwa hivyo utaona kuwa km 6/ltr ni mwendo wa km240 endapo kanunua lita 40! Depending wapi anaekwenda na ukubwa wa gari, kwa siku utamaliza lita hizo. Mfano, kawaida magari mengi reserve yake ni litre 10-15 hasa makubwa. Kwa hiyo endapo tank ni tupu, ina maana dereva anakuwa na litre 25 tu za kufanyia kazi! Hizi zita-cover km 150 tu
 
Back
Top Bottom