Live Clouds TV: Ujinga wa Watanzania kwa Pastor Eubert Angel

Live Clouds TV: Ujinga wa Watanzania kwa Pastor Eubert Angel

Huihui2

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
7,021
Reaction score
11,475
Kinachoendelea Clouds TV kutoka Leaders club ni aibu tupu. Pastor Mzimbabwe anayeishi London anawaburuza kama kawaida yao. Nawakunbusha kidogo utapeli wake wa zamani hapa.

Kama alivyo prophet Alfa Lukaku, mzaire , nani ya Johannesburg. Alifanya muujiza wa kumfufua mtu. Aliyejifanya kafa, ndani ya geneza, lililoletwa toka mochwari, straight kanisani. Akamfufua mtu. Watu wakapinga na kumlaani.

Baada ya siku chache, alikwenda kwenye TV kuomba msamaha. Bado anaendelea kuhubiri mpaka kesho. Na hilo tukio la kumfufua mtu you can google.

Eubert Angel alishikwa anafanya training na watu wakufanyiwa/kupokea muujiza, kwa malipo. Na alikiri. Walishikwa na police waki recruit watu wajifanye wanavilema, kwa malipo.

Walikuwa wanawapa nguo maalumu za kuvaa. Walikuwa wanawapanga ukumbini. Baada ya ibada walikuwa wanawalipa kwa kushuhudia uponyaji.

Na ukichunguza, ibada zao wanapendelea usiku wa kiza kiza. Baada ya kushikwa, walikuwa paraded na palisi, televisions kuwaonyesha. Na wale waliotumiwa wali confess kulipwa pesa kusudi wawa deceive umati.

Yote haya yalifanyika wazi television za SABC, Zimbabwe TV, miaka ile.
 
Angel has been critiqued for advocating prosperity theology through his sermons, teachings and writings, or the prosperity gospel, a pseudo-theological belief that the reward of financial and material gain is the divine will of God for all pious Christians.

He has also had multiple controversies surrounding his ministry and charities and has had warrants issued against him. He has been accused of financial fraud and sexual misconduct. In 2023 he was found running a money laundering scheme by abusing his diplomatic privileges. Angel's former congregants have accused him of rape and sexual assault. In 2013 his name was included on a list of people who bought fake degrees from an online degree mill
 
ignorance.png
 
Ni waongo waongo tu , Huyu prophet Joshua tuliwahi kuonana mahali na mafuta yake ya Upako.
Ilikua ni Virgin Olive Oil tu.
Nilienda kwa kazi nyingine.
Nikakuta wamejaa waumini toka nchi mbalimbali na walilipishwa hela Ndefu tu..
Mi nilishikwa mkono tu na dada mmoja nikaombewe.
Fika pale waumini wanaangushwa sijui nini.
Jamaa kaja na bakuli lake la mafuta nikanyanganya
Kanipiga jicho.
Nikatia dole bakulini nikalamba nitest.😁
Aisee uongo mtupu.
Kataka kunipaka usoni nikatoa nje na kuondoka kabisa.
Maana angenisukuma
nidondoke aseme miujiza.
Ni mafuta tu hayo.
 
Wewe achana na ushetani wako ulionao kichwani huwez kufake miujiza yote hiyo
 
Huyo nabii ana shutma za utakatishaji fedha. Pia ana dharau sana na kiburi juu. Nilimuona kwenye Gold Mafia
 
Huyo nabii ana shutma za utakatishaji fedha. Pia ana dharau sana na kiburi juu. Nilimuona kwenye Gold Mafia
Kwenye Gold Mafia mwizi ni nani na nani aliyeibiwa? Mnalishwa matango pori na Aljazeera .Ndio maana hata mwisho wa Documentary Aljazeera waliogopa kuhitimisha kwa kutaja mwizi nani na nani kaibiwa na kuweka ushahidi wa wazi
 
Media inapotumika kuunga mkono utapeli, nchi hii ina wjng wengi sana

Ova
Dini isiyo yako achana nayo hangaika na ya kwako

Kila dini ina wenyewe.Pilipili shamba wewe inakuwasha nini? Usiangalie hata TV waachie wenyewe
 
Kwenye Gold Mafia mwizi ni nani na nani aliyeibiwa? Mnalishwa matango pori na Aljazeera .Ndio maana hata mwisho wa Documentary Aljazeera waliogopa kuhitimisha kwa kutaja mwizi nani na nani kaibiwa na kuweka ushahidi wa wazi
Unajua maana ya shutma? halafu sijataja neno wizi. Wewe ndio unataka kunilisha matango pori.
 
Radio na TV kubwa zote zimetekwa na self proclaimed preachers ambao wengi mkazo ni sadaka na miujiza! Hata mahubiri sehemu kubwa si habari za ufalme bali miujiza ambayo haiokoi mtu.

Zinalipwa fedha nyingi kama commercial program sio kwaajili ya gospel bali kuvuta watu kwake kama mtu pekee mwenye Yesu wa kuwasaidia kwenye shida zao na si habari za wokovu.

Lakini haya yote yalitabiriwa kutokea nyakati za mwisho. Wengi watakimbilia wanachofikiri ndio ukweli yumkini hata wateule kumbe wanajisalimisha kwenye madhabahu za giza kwa hila bila kujua.
 
Wote wanajifanya au wanadhani wana nguvu fulani tofauti na wengine kutoka somewhere ni wajinga tu .
 
Back
Top Bottom