Live from TEMTL HQ DSM: Hafla ya utoaji tuzo za via za usalama barabarani kwa shule za msingi za totalenergies kwa ushirikiano na karibu art space.

Live from TEMTL HQ DSM: Hafla ya utoaji tuzo za via za usalama barabarani kwa shule za msingi za totalenergies kwa ushirikiano na karibu art space.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Mimi mwanabodi mwenzenu, niko mitaa ya Masaki kwenye Makao Makuu ya Kampuni ya Mafuta ya TotalEnergies, kuwaleta live hafla ya utoaji wa Tuzo za VIA za TotalEnergies kwa ushirikiano na Karibu Art Space kwa shule za msingi za jijini Dar


View: https://www.youtube.com/live/coYQ8VfN2qs?si=Klm3XDbUpTH3TJLm
Karibuni.

Background
Kampeni ya VIA Creative Project kuhamasisha usalama barabarani, inayoendeshwa na kampuni ya mafuta ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, kwa ushirikiano na Nafasi Arts Space, kuhamashishaji usalama barabarani kwa njia ya sanaa kwa shule za msingi za jijini Dar es Salaam, inazidi kuchanja mbuga kwa wiki hii kuzitembelea shule mbili za jijini Dar es Salaam.

Meneja Mawasiliano wa TotalEnergies, Anita Bulindi, amesema kampeni hiyo ina lengo la kuwafikia wanafunzi 600 kwenye shule 6 za Msingi za jijini Dar es Salaam, kwa kuanzisha vilabu vya usalama barabarani na kuhamasisha mambo ya usalama barabarani kwa watoto tangu wakiwa shule za msingi.

Bulindi amezitaja shule hizo ni Shule ya Msingi Makuburi iliyopo Ubungo, Shule ya Msingi Uzuri iliyopo Manzese, Shule ya Msingi Buza iliyopo Temeke, Shule ya Msingi ya Ugindoni iliyopo Kigamboni, Shule ya Msingi ya Jangwani Beach iliyopo Mbezi Beach na Shule ya Msingi ya Ubungo iliyopo Ubungo.

Bulindi amesema kampeni hiyo inawafundisha wanafunzi wa shule za msingi usalama barabara, kuwahamashisha kuwa mabalozi wa usalama barabarani kwa wenzao kwa kuanzisha vilabu vya usalama barabarani mashuleni, na inakwenda sambamba na uhamasishaji utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti, miti 500 inatarajiwa kupandwa kwenye shule hizo.

Shindano hilo linahusisha kuhamasisha usalama barabara kwa kutumia sanaa na picha za kuchora za watoto kuhusu usalama barabarani, wakati wakiyafanya hayo, watarekodiwa picha na video, kisha kisha picha zao na video hizo na picha hizo zinashindanishwa na za watoto kutoka nchi mbalimbali, washindi watatangazwa mwezi October na kuiwakilisha Tanzania kwenye shindano la kimataifa la dunia.

Mwezeshaji kutoka Nafasi Arts Space, Michael James Kid amesema, watoto wanavipaji mbalimbali vya sanaa, na wanapenda picha, hivyo ukiwafundisha kitu kwa kutumia sanaa za picha na michoro, kunawajengea hamasa na ari zaidi kujifunza usalama barabarani.

Watoto hao mabalozi wa usalama barabarini wa shule ya Msingi ya Uzuri, Jamal Ali Kingazi na Phibi William Christopher, na mabalozi wa usalama barabarani wa Shule ya Msing ya Jangwani Beach, Sarah Masanja na Farhia Hashimu, walizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo na kuwashukuru TotalEnergies Tanzania na Nafasi Art Space kuwapatia mafunzo hayo.

TotalEnergies Tanzania ni kampuni ya mafuta ya petroli inayoongoza Tanzania kwa kuwa na vituo zaidi ya 100 nchini Tanzania na iliingia nchini Tanzania tangu mwaka1969. Biashara ya TotalEnergies inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na

bidhaa za mafuta, ambayo ni kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta na pia katika idara maalum ndani ya wake shirika hilo.

Paskali
Rejea
 
Ni kitu kizuri sana, nadhani na baadaye waende mbele zaidi n akuwapa motivation hata wanaosaidia kuvusha watoto barabarani kwenye sehemu zilizo busy sana kama Tegeta kwa ndevu kuna mzee mmoja huwa anajitolea sana kuanzia asubuhi mpaka jioni
 
Back
Top Bottom