Elections 2010 Live From TV's: Upigaji wa kura, matokeo na yatokanayo

Hii ni hali halisi niliyoikuta saa 12.00 asubuhi nilipowasili kituoni:

 

Attachments

  • DSC00001.jpg
    50.8 KB · Views: 238

Jamni viongozi wetu heshimuni bas sehemu mnayopatia ajira:A S angry::A S angry:
 
Nikilinganisha na Uchaguzi wa Mwaka 2005 naona kuwa kwa muda wa saa 12.00 asubuhi waliojitokeza ni wengi.

Katika sub-vituo vyote 9 katika kituo chetu, wasimamizi wa uchaguzi walikuwepo wakati huo na askari wa kutosha: Police, Magereza na Askari wa Jiji. Hakika kwa hili wamejiandaa na wanastahili pongezi walau kwa wakati nilipowaona.


Hii ni mfano wa karatasi ya Kura ya Urais:

 

Attachments

  • DSC00003.jpg
    27 KB · Views: 254
  • DSC00002.jpg
    38.9 KB · Views: 258
  • DSC00004.jpg
    27.3 KB · Views: 257
Hii ni Mfano wa Kura ya Ubunge:

 
Na hii ni mfano wa Kura ya Madiwani:

 
Na haya ni maelekezo kwa wapiga kura:

 

Attachments

  • DSC00007.jpg
    51.7 KB · Views: 227
  • DSC00006.jpg
    38.6 KB · Views: 221
na mimi nimetoka kupiga kura sasa.. saa kumi na mbili na robo nilikuwa kituoni huku Tegeta Bahari beach... ilipofika saa moja kamili juu ya alama watu wakaanza kuingia kupiga kura!!!!! mpaka naondoka kituoni hali ilikuwa shwari,... watu walikuwa watulivu... na askari walikuwa wametulia na kuelekeza vizuri.. hii ni taarifa mpaka naondoka kituoni... sijui yatakayojili baada ya hapo....
 
Na haya ni maelekezo kwa wapiga kura:


maelezo Namba 3 inatoa taarifa isiyo sahihi.. BOX lipo sehemu ya kulia na siyo chini.. nashindwa kuelewa kwa nini tume imetoa taarifa isiyo sahihi
 
Tunaomba wenye habari za maendeleo ya vituoni waturushie!
 

Thanx Superman...Hope hii itaendelea mpaka watakapoanza kutoa matokeo....Mungu akupe Afya na nguvu...Kila la kheri...
 
So far Hali ikoje??? Hasa maeneo ya Buguruni (Sheli, Mnyamani, Madenge,Rozana, Ghana na Malapa??)
 
Nilipiga Kura yangu saa 1.30 asubuhi nikiwa mtu wa 5.

Uhakiki wa wapiga kura unachua muda:

Ofisa wa Kwanza wa NEC anapokea kadi ya mpiga kura na kuangalia kama jina lako lipo.

Ofisa wa pili anaangalia kama uko katika daftari ya wapiga kura. Akiona jina anaoanisha na picha na kisha mawakala wa vyama nao wanashuhudia. Baada ya hapo anasoma namba yako na niliona mawakala wa CUF, CCM na CHADEMA wananakili namba ya mpiga kura.

Baada ya hapo unaenda kwa msimamizi wa kituo, anakagua kadi yako na kisha anaisoma kwa sauti na mawakala wanahakiki. Kisha anakupa karatasi tatu. Ya blue nyuma - Urais, Nyeusi nyuma - Ubunge na nyeupe nyuma - Madiwani. Anazikunja na kisha kugonga mihuri miwili kwa nyuma katika kila karatasi. Kisha anakupatia.

Kisha unaenda katika sehemu iliyoandaliwa kupiga kura kuna pen hapo, unakunjua karatasi zako na kuweka vema kwa mgombea unayemtaka na kisha unazikunja.

Ukimaliza: Blue-Urais unatumbukukiza katika sanduku la kura za Rais, Black-sanduku la Ubunge na Nyeupe sanduku la mwadiwani.

Ukimaliza hapo kuna mdau wa NEC anakupaka wino katika kidole kidogo kisha unaondoka.
 


ITV kweli wanafanya kweli! Nawapa BIG-UP kwa sana! Yaani matokeo yanakuja live, kituo kwa kituo, TANZANIA NZIMA! Picha ni za Dar es Salaam, lakini wanaongea kwa njia ya simu. Safi sana! HII ndio maana halisi ya TEKNOHAMA!

Hongereni sana ITV!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…