Elections 2010 Live From TV's: Upigaji wa kura, matokeo na yatokanayo

Elections 2010 Live From TV's: Upigaji wa kura, matokeo na yatokanayo

Miye katika kituo changu nilichopigia kura bibi mmoja mwenye umri kati ya 65 na 70 baada ya kupiga kura. Alisema hadharani kwa walio mstarini kwamba kabadilisha kura yake uchaguzi huu na kumpa Slaa na kuwaomba walio mstarini wasiharibu kura zao. Alisema, "Nawaomba sana mumpigie Slaa na watu wake." kisha akaweka alama ya peace mikono yote miwili basi watu wakaangua kicheko kikubwa. 😛eace:😛eace:😛eace:
 
Baadaye leo tutashirikiana na BongoRadio kurusha matangazo ya ITV online!!!! sijui saa ngapi.. naenda kulala maana kuna kukesha kesho au maandalizi ya safari!!!

Asante Mkuu wa kaya ya JF.

Tuko pamoja. Usiku Mwema.
 
Mara hali ni shwari.

Ila kuna baadhi ya viongozi wa kisiasa wameripotiwa wanawabeba wapiga kura kutoka nyumbani na kuwaleta kuja kupiga kura. Inasemekana kuwa baada ya kufika viongozi hao wanalazimisha wapiga kura hao wapiga bila kupiga que.

Wanausalama wanalifanyia kazi hili.

ITV studio one hii:

attachment.php
 
Attachments

  • DSC00002.jpg
    DSC00002.jpg
    30.1 KB · Views: 156
Baadaye leo tutashirikiana na BongoRadio kurusha matangazo ya ITV online!!!! sijui saa ngapi.. naenda kulala maana kuna kukesha kesho au maandalizi ya safari!!!

pleiya kumbe uko d town? Mi nilidhani na wewe umetia timu kama jasusi
 
ITV Na Gondwe: Studio 2:

attachment.php
 
Attachments

  • DSC00004.jpg
    DSC00004.jpg
    31.8 KB · Views: 159
Jimbo la Kinondoni:

Kuna jamaa anahojiwa anadai haenda kupiga Kura kwa sababu CCM wataiba kura. Alopobanwa anadai hata kuna chaguzi moja ya mbunge waliiba. Hata hivyo wengi waliohojiwa katika pub wakipata kinywaji na kucheza pool wanadai kuwa wataenda baadaye mara que zikipungua. Wengi wanaonekana kuwa na hamasa.
 
Miye katika kituo changu nilichopigia kura bibi mmoja mwenye umri kati ya 65 na 70 baada ya kupiga kura. Alisema hadharani kwa walio mstarini kwamba kabadilisha kura yake uchaguzi huu na kumpa Slaa na kuwaomba walio mstarini wasiharibu kura zao. Alisema, "Nawaomba sana mumpigie Slaa na watu wake." kisha akaweka alama ya peace mikono yote miwili basi watu wakaangua kicheko kikubwa. 😛eace:😛eace:😛eace:

Du!, Mkuu hapo si Bibi kavunja sheria? Askari walimwacha?
 
kwenye picha naona ni bendera ya cCM, vipi mlipigia kura kwenye kituo cha CCm?

Haaa haaa, sikuinote hiyo. Nadhani ni ofisi ya Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa. Sijajua kama bendera ya CCM ni sawa kuwa hapo.
 
Zanzibar hali inaripotiwa kuwa ni shwari sana. Haijapata kutokea.
 
Mkuu MJJ, tunashukuru sana kwa kutu habarisha.
Tunakusubiri Bongo radio baadae uendelee kutupa updates za uchaguzi.
 
Haaa haaa, sikuinote hiyo. Nadhani ni ofisi ya Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa. Sijajua kama bendera ya CCM ni sawa kuwa hapo.

au ni bendera ya halmashauri ya Manispaa ya Ilala?
 
Back
Top Bottom