Elections 2010 Live From TV's: Upigaji wa kura, matokeo na yatokanayo

Mpaka naondoka kituoni hali ilikuwa kama hivi:




 

Attachments

  • DSC00008.jpg
    48.9 KB · Views: 232
  • DSC00009.jpg
    40.5 KB · Views: 228
Damn so wht were they doing for all these dayz???????????? With all the technology that the promised kwa nini isiwe kwamba unaandika sms with your reg no and then inakupa kituo cha kupiga kura! Kma mambo ndiyo hivi kupiga kura nje ya nchi mpaka 2050!
 
wakuu TBC is already biased... stinky television
 
Wakati naondoka kituoni saa 1:45 asubuhi hali ilikuwa hivi:

 

Attachments

  • DSC00010.jpg
    37.5 KB · Views: 204

mimi katika kituo nilichoenda huku Tegeta bahari beach utaratibu ulikuwa hivi:

  1. ukifika kituoni unapanga mstari mita kama 20 toka maafisa wanaoendesha upigishaji kura walipo.. wanaume mstari wao, wanawake mstari wao
  2. Afisa wa Polisi anaigiza wanawake 7 na wanaume 7..
  3. kwa kuwa kituo changu kilikuwa na sehemu 7 za kupigia, ukiingia either unaenda direct kwenye sehemu yako (kama ulifika kabla ya leo na kunakiri namba ya sehemu ya wewe kupigia --- naamanisha namba 1 mpaka 7) kama hujui unatakiwa uende sehemu majina yalipobandikwa na kutafuta jina lako na namba ya kituo.. KUMBUKA MAJINA YAMEPANGWA ALPHABETICALLY
  4. ukishajua NAMBA YA sehemu unayotakiwa kupigia kura, karani mwongozoji atakuelelekeza wapi pa kwenda
  5. ukifika sehemu ya kupiga mstari.. utapanga mstari.. kama utakuta kuna wengine mbele yako
  6. zamu yako ikifika unaenda kwa karani wa kwanza ambaye unampa kadi yako, anahakiki jina lako kwenye rejister, na kisha anataja kwa sauti ambapo mawakala wa vyama nimeona wanaandika kumbukumbu kwenye writing pad zao (ila mmoja nimeona kama anasinzia)..
  7. ukitoka hapo unaenda kwenye karani mwingine ambaye anaandika namba yako kwenye karatasi ya rejester (kipande kinachobaki kitabuni) na kisha kukuchania katarasi za kupigia kura
  8. then, unaenda kwenye kibanda cha kupigia kura
  9. ukishamaliza kupiga unatumbukiza kwenye box kwa kuzingatia rangi-- bluu ya raisi, nyeusi mbunge na nyeupe diwani
  10. ukishatumbukiza, karani mwingine anakuwekea wino mweusi
  11. baada ya hapo unaondoka kituoni
huo ndo utaratibu nilipitia... ila kasheshe moja nimeona kwa wasio jua kusoma.. nimeona kuna uwezekano mkubwa kudanganywa... kwa sababu wanaambiwa chagua mtu yeyote (minogoni mwa wapiga kura kama utakuwa hujaenda na mtu wa kukusaidia)

habari ndio hiyo!!
 
Wakati naondoka kituoni hali ilikuwa hivi:

 
Ule uvumi kwamba ukiweka Tick kwa Slaa na baadaye ukikunja karatasi ile Tick inaamia kwa JK hakika si za kweli.

Mpangilio wa majina katika karatasi na hata karatasi yenyewe baada ya kuitafiti kwa muda haikuwa na na mwelekeo wa ukweli wowote.

Kitu kimoja ambacho nime-observe ni kuwa wasimamizi wote ni vijana wadogo sana na baada ya kuwahoji wawili watatu nimejiridhisha kuwa wengi Elimu yao inaweza kuwa haifiki ile ya Chuo.
 

nilisahau hili..

ukienda kupiga kura hakikisha karatasi yako ya kupigia kura inapigwa muhuri sehemu ya nyuma.. muhuri unapigwa mbele yako,, isiyopigwa kura inaharibika
 
Baada ya briefing ya hapo juu, sasa naamia katika TV's kuwapa updates: ITV wako Live wanaohoji waandishi sehemu mbalimbali, , TBC pia wanarusha matangazo; , Channel 10 nao wako hewani na Star TV pia.

. . . . . . .
 
Baada ya briefing ya hapo juu, sasa naamia katika TV's kuwapa updates: ITV wako Live wanaohoji waandishi sehemu mbalimbali, , TBC pia wanarusha matangazo; , Channel 10 nao wako hewani na Star TV pia.

. . . . . . .


 
hivi TBC wanaumwa????? what a scrap? yaani wakati ITV wapo mitaani wanafuatilia mambo yanavyoendelea ... eti TBC wapo studio wanajadili jinsi vyombo vya habari vilivyokuwa vinaripoti na jinsi wagombea walivyokuwa wanatoa ahadi..... jamani leo ni upigaji kura kwa nini vyie TBC msiende mtaani.. si mnatumia kodi zetu jamani.. wewe MHANDO unafanya nini hapo... mbona uzoefu wa kufanya kazi BBC hausaidii hapa...

hongera ITV hongera STARTV...
 
According to ITV, vituo vingi vya Kigamboni mambo ni shwari. Kuna amani na utulivu.
 
Baada ya briefing ya hapo juu, sasa naamia katika TV's kuwapa updates: ITV wako Live wanaohoji waandishi sehemu mbalimbali, , TBC pia wanarusha matangazo; , Channel 10 nao wako hewani na Star TV pia.

Thanks Superman

Acid kasema TBC1 wapo biased.....ni kweli? wapo biased Kivipi?
 
Singida mambo shwari ila kuna kituo kimoja ambacho kuna wapiga kura hawajaona majina yao. Na kuna mzee anaojiwa anasema asaidiwe apate haki yake ya kupiga kura.
 
Thanks Superman

Acid kasema TBC1 wapo biased.....ni kweli? wapo biased Kivipi?

TBC1 yuko Lusingi na analyst wawili wanachambua tu Uchaguzi kwa ujumla lakini hakuna LIVE toka vituoni kama ITV
 
Baadaye leo tutashirikiana na BongoRadio kurusha matangazo ya ITV online!!!! sijui saa ngapi.. naenda kulala maana kuna kukesha kesho au maandalizi ya safari!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…