MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Tayari tupo msibani huku kwenye jumba la kifalme kama picha niliyopost inavyoonyesha. Muda mchache uliopita alifika mzee wa ukoo na tayari kikao cha wanandugu kinaendelea. Ila jana tayari walishamchagua mrithi wa malkia... kuna mtoto wa Malkia anaitwa Charles ndo kachaguliwa.... wenyewe huku kwao naona wengi wanamwita CHALII.
Majirani siwaoni kabisa msibani. Ila jirani mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mzee Smith ndo kasema kwamba majirani wameususia msiba kwasababu Eliza alikuwa hahudhurii misiba ya wenzake. Pia Mzee Smith anadai yeye ndo alimuuzia kiwanja Marehemu Eliza akajenga nyumba inayoonekana pichani. Ila kitu kilichonishangaza zaidi eti Eliza hakuwa na kadi ya bima afya ndo maana matibabu yake yalisuasua... inasikitisha.
Nitazidi kuwajuza zaidi maana watu tuko hapa toka jana usiku.... watu kwa sasa wapo wapo tu. Ukitazama picha utaona vyakula vinaendelea kupikwa... mimi niko na wazee wengine wa hapa, Mzee Fergusson, Al Fayed, na wengine tunacheza karata... he! ngoja kwanza 😰😡!!!... kuna watu kama watatu karibu yetu toka wamekuja hawaongei ila ghafla wameanza kubishana kwa kikwao nimeambulia maneno machache.. wanataja sana Nchemba & tozo. Nimeambiwa ni kabila moja na Eliza. Msibani mambo ni mengi sana.