Live Kutoka Mbinguni/ Welcome back to Heaven

Leta ushaidi na uthibitisho wa uwepo wa huyo Mungu.

Nakwambia hivi [emoji116]

Mungu hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
We subiri kiberiti acha kutusumbua akili hata siku za sodoma na gomora na kipindi cha gharika kulikuwa na watu kama wewe..kwa kifupi tumewazoea
 
Kuna mtizamo ninao uona katika hili la kuharibika au tuseme kutoa mimba.
Kimsingi mtu ana aina tatu za miili katika hali tofauti.
1-mwili wa damu na nyana(kutoka kwa mama)
2- mwili wa roho kutoka kwa Mungu
3- Mwili wa roho uliotengana na ule wa flesh teofania( mzimu)
4 -Mwili uliotukukaglorified body huu ni ile teofani itakapo chukua ule wa flesh ulio kaburini na kuchukua state mpya ya kutukuka.
Huu wa kutukuka ni mfano wa ule wa Yesu aliofufuka nao kaburini tofauti na watakatifu wengine wote miili yao ipo bado makaburini wakisubiria. Hapa ndipo penye kuondoa utata wa swali nguli la ikiwa wapo wanaodai kuwa watu hawafi na kwamba wapo mbinguni au kuzimu vyovyote tunavyoweza kuita ni kwa nini basi kuwe na ahadi ya kufufuliwa wafu siku ya mwisho? Jibu ni kwamba mwili wa roho uliotengana na fleshi upo katika hali ya teofani au mzimu ambapo hauwezi au sio wa kushikika ni kama upepo huwezi kupeana mikono au kushiriki kula na wapendwa wao. Lakini wakiisha rudishiwa ule wa flesh katika kutukuzwa kwake wanarudi kuwa watu(binadamu) maana ndivyo tulivyo umbwa.
Yesu baada ya kufufuka na kuuchukua ule wa flesh alipowatokea aliwaambia wanafunzi wake leteni kitu nile au nishikeni kwa kunipapasa mjue ni mimi na sii mzimu(roho).
Nikirudi kwa mada ya mimba, mtoto hakamiliki kuwa mtu hadi azaliwe maana pindi tu anapozaliwa ndipo ule mwili wa kimbingu(nafsi hai) huungana na huu wa baba na mama kufanya hiyo nafsi iwe hai.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usitumie akili zako finyu kibinadamu kuelewa mambo ya kiroho.

Mimba ikishatungwa, Roho unakuwa tayari, Si mimba tena ,ni mtu tayari ndani ya tumbo.

Roho Ile ni mtu kamili, Roho zote ni sawa.

Atakuwa kana wengine, ila katika Roho utaweza kutambua Hali aliyokuwa nayo kabla ya kufa.

Uwe mtu wa Roho ndipo uelewe ya Rohoni, tofauti na hapo utajikuta unakufuru Kwa kuongea usichojua.

Nawe ubarikiwe.
 
Mtumishi unaposema mtu hakamiliki Hadi azaliwe ndio awe NAFSI hai unakosea pakubwa.

Rudi kurekebisha ulichoandika au Rudi kwenye Imani na mafundusho hayo mapotofu uliyopokea.

Kwa maana ingine unasema mtu akitoa mimba, Hana kosa lolote sababu mtu anakuwa hajakamilika.

Hii Si Kweli.

Mbinguni Roho za watoto waliotolewa mimba ni HALISI kabisa kama watu waliokufa wakiwa watu wazima.

Roho hizo zinasema, na zinamlilia Mungu muda wote zikidai kisasi Kwa wazazi walioshiriki kitendo Cha uuaji wa mtoto, na Si mimba!!
 
kwaiyo ww ukifariki tusemeje ebu acha wosia kabisa ili tuandike pale kwenye kabur lako kuzaliwa mwaka 1994 na kijitenga na mwili 2023 mwezi wa 11 saa 5 usku🤣😅😆😁😄😃😀
anacho kisema yuko sawa msikie
 
Ni kwa andiko lipi unaweza kulisimamia kutetea hoja ya roho za mimba kabla ya kuzaliwa kulilia kisasi?
Na je kuna mahali mimi nimetamka kusema kuwa kutoa mimba sii kosa?
Unaposoma hoja ya mtu jaribu kuweka itikadi pembeni ili kuruhusu uhuru wa akili kufanya kazi kwa haki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mara zote unatakiwa kujua hamna swali la kijinga ila majibu ya kijinga, joking aside.... hoja zako hazina uambatano na mafundisho ya dini za abrahamic.
 
Niliposoma hiko kitabu cha uongo kwa kina nimebaini ni stori za uongo Mtupu
1. Mungu gani huyo anayebebwa na shetani mpaka kilimani?
2.Ni nani aliyekuwa anarekodi wakati huyo Mungu anaumba Dunia?
3.Hivi jua liliumbwa siku ya ngapi na kabla ya kuubwa Jua mwanga gani uliokuwepo?
4.Yesu alivyokwenda Mlimani kusali peke yake muandishi wake alikuwa nani mpaka mazungumzo yake na Mungu yawe kitabuni?
5..Eti ukiwa na Imani unaweza ukaamuru mti ng'oka na utang'oka lakini Yesu huyo huyo akasaidiwa kubeba msalaba tu maana aliushindwa ili akatundikwe.
6.Hivi inakuaje mnatembea kwa mguu km1400 kwa usiku mmoja lakini km 700 tu miaka 40 Hao wanaIsrael na Mussa wao
7.Imani yako inasema Umerithi zambi za Adam na Eva lakini kituko kwani Hamjarithi Utajiri wa Suleiman
8. Eti Nuhu alijenga Safina sababu ya Gharika kuu na akapakiza viumbe jike na dume swali linakuja (i)Taarifa ilifikishwa vipi Afrika,Ulaya,Amerika kusini? na Australia ?(ii)Simba alikula nini kipindi chote cha gharika ndani ya Safina(iii) Watu walikula nini baada ya mafuriko hayo makali maana ardhi ilikuwa tupu mazao yamekaisha na mafuriko? (i)Kangaroo alisafiri vipi mpaka Australia
7.Baada ya kula Tunda huko bustani ya Eden Mwanamke Eva akasema Atazaa kwa Uchungu Swali hawa ng'ombe wetu hapa Tarime mbona wanazaa kwa Uchungu wametenda kosa gani?
8.Kwenye Sodoma na Gomola tunaambiwa Mke wa Ruthu aligeuka Mwamba wa Chumvi swali ni hili nani aliyemuona kwamba amegeuka Mwamba wa Chumvi wakati walipewa taarifa kuwa ni marufuku kugeuka?
9.Hivi ni Mungu gani huyo aliyevumilia miaka 400 ya utumwa tuliofanyiwa na kuuzwa mnadani kama maembe halafu ataniadhibu kwa kutokumuamini?
10.Eti msamehe Mtu 7x70 kwa makosa aliyotenda Lakini huyo Mungu kashindwa Kumsamehe Adam na Eva kwa kula Apple moja?
11.Samson alimuua Simba kwenye jangwa la Palestina aaahaaaa Toka lini simba anaishi kwenye jangwa?.

Hakika ninakuambia kama kungekuwa na Nguvu kwenye jina la Yesu hao Wazungu wangeficha kama inavyofichwa Teknolojia ya Nyuklia.

Heshimu sana Babu wa Mababu zako maana wao ndiyo wenye DNA zako wewe umetoka kwao Dini ni tamaduni ndani ya tamaduni kuna mila ndani ya Mila kuna Imani na Imani ndiyo Wageni wakaita Dini hakika nakuambia Imani ya Kiafrika wala haina Masharti magumu na Inafanya kazi kwa Ubora wa juu sana na Ibada zake ni kwa Mwaka mara moja au mbili lakini Imani zingine lazima ufanye kila muda kila wakati lakini Matokeo 0.

Heshimu Afrika heshima maadili na mila ulizoachiwa..

Unaweza sema Uongo Kanisani Unaweza sema Uongo Msikitini na hakuna kinachoweza tokea usije sema Uongo kwenye Mizumu au kwenye Kilinge cha Mganga utakwenda na Maji .Toa ahaadi ya Pesa ya sadaka kanisani na Msikitini usipotoa hakuna kitakachotokea Usije thubutu Kwa Mganga au kwenye Mizimu hutoamini macho yako. KILINGE HAKITANIWI WALA HATUSEMI UONGO .
 
Ameutelekeza uzi
Si Kweli,

Follow me, thread hii ITAENDELEA......

Lakini Pana thread zingine nyingi nimeandika zitakazokujenga sana Ili ujue zaidi kiroho amen.


Soma: Kasri tupu la Mfalme Suleiman katika Jiji la walioachwa - Rabbon
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…