Live Kutoka Mbinguni/ Welcome back to Heaven

Ndugu mwandishi naona una ujumbe mzuri ila ubora wa uwasilishaji wako upo partial .. mfano,hujaeleza namna ulivyokutana na Yesu bali unasema ukamuuliza Yesu hatujui umekutana naye vip na umemjuaje ni Yesu?
Ubarikiwe.

Rudia kusoma tena, nimeandika japo ni Kwa uchache, endelea kuwepo maana Uzi huu hautaisha Leo Wala kesho,

Ni wa Milele.

Amen
 
Ubarikiwe.

Mtu ni ROHO, vazi ni mwili.

Roho zetu zilikuwapo Mbinguni ndani ya Mungu kabla ya kutuleta duniani Kwa KAZI maalumu.

Duniani tu wapitaji.

Amen

Na tumfanye mtu kwa sura na mfano wetu huo umilele wa mwanadamu unautolea wapi
 
Sema kaka, cha kuongeza, Mbingu sio choo so sio kila mtu ataingia.

Hakuna jambo gumu duniani kama kutaka kuingia mbinguni.
 
Sema kaka, cha kuongeza, Mbingu sio choo so sio kila mtu ataingia.

Hakuna jambo gumu duniani kama kutaka kuingia mbinguni.
Ni Kweli, Mungu katuweka hapa tuvipige vita Ili kuingia Mbinguni.

Mwanadamu hakuumbiwa moto,

Ingawa pia ni Kweli, imeandikwa njia ya Mbinguni ni nyembamba na waionao ni Wachache.


Mimi nawe na mwingine tuwe kati ya hao Wachache watakarudi tena heaven.

Ubarikiwe. Amen
 
Kwa hiyo umelala,umeota rangirangi za kuvutia ukajua ndio mbinguni?mbi
 
Katika uumbaji,vitu vyote vinataja viliumbwa siku Fulani,Fulani ila sijaona kuumbwa Kwa jehnamu,he iliumbwa lini?
 
Kwa hiyo umelala,umeota rangirangi za kuvutia ukajua ndio mbinguni?mbi
Nawe ubarikiwe.

Niliyekuwa pale na uzuri niliouona ndiye ninayejua nilikuwa wapi,

Hukusoma imeandikwa Mbinguni hakuna jua, hakuna usiku ni Nuru tu?

Nakuombea nawe ukutane naye Kwa wakati na njia ya kipekee.

Amen
 
Katika uumbaji,vitu vyote vinataja viliumbwa siku Fulani,Fulani ila sijaona kuumbwa Kwa jehnamu,he iliumbwa lini?
Eneo unalotaja, halijaumbwa Bado.

Leo na mada hii itajikita kuhusu habari kuhusu Mbinguni pekee,

Kuna mengi yanakuja hayajaandikwa Bado.

Ubarikiwe. Amen
 
Mbinguni malaika wanapika chakula? Watu wanakula matunda.

Maana tunafundishwa huku na wachungaji kuwa hatutakua na njaa wala hakuna kula
 
Ni maombi yangu Kwa Mungu,

Wote watakaosoma Uzi huu, Mungu awasaidie wote waingie Mbinguni.

Aaamen
 
Mbinguni malaika wanapika chakula? Watu wanakula matunda.

Maana tunafundishwa huku na wachungaji kuwa hatutakua na njaa wala hakuna kula
BIBLIA ni Pana sana.

Unamhitaji Roho mtakatifu akufunulie,

Hukusoma Yesu akiwambia wanafunzi wake kuwa wasubiri hapo atakapokunywa divai Mbinguni na baba yake?

Yesu asema, ikiwa ninawasimulia ya Duniani hamsadiki, vipi nikiwasimulia ya Mbinguni?

Hukusoma kuhusu maji ya Uzima, hukusoma juu ya bustani ya Mbinguni?

Uzuri wa Mbinguni hauelezeki.

Mbinguni ziko nyumba za WATAKATIFU na Kila mtu ana kwake, nyumba Yako imefikiwa hatua Gani?

Ubarikiwe. Amen
 
Unaijua asiri yako? Nani aliweka sukari kwenye nanasi? Ni Baba yako Mzee Mang'ombe?
Ubarikiwe.

Yesu anatutaka tuwapende na kuwahubiri INJILI wote hata walioasi katika Dhambi.

Tukiwaelewesha Kwa Upendo na kuwaombea bila kuchoka,

Yesu atawapa neema ya Wokovu na wote wataingia Mbinguni.

Ni maombi yangu, wote wasomao Uzi huu ,waokolewe na waingie Mbinguni siku ya HUKUMU.

Aamen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…