LIVE : maoni ya JF kuhusu katiba mpya

Chama cha siasa kitakachohubiri na kuchochea fujo na vurugu kwa lengo la kufanya Tz isitawalike kifutwe mara moja.
Wewe ni mgonjwa tumeisha elewa lengo lako, lakini katiba tunayotaka ni ya kudumu kwa maslahi ya taifa.
Chama cha siasa kinao muda wa kuishi na kufa kama vile KANU Kenya!!!!
 
mimi nawaomba waTZ wenzangu, tusome katiba za nchi kama US, UK, CANADA, hizi ndo nchi zinazoongoza kwa demokrasia duniani., tukae chini tuona vipengele gani vizuri kutoka kwao, then na sisi tuige.
hivi-hivi hatuwezi jua vipi vizuri katika katiba, na vipi tunapaswa tuwe navyo katika katiba mpya
 
kUNA OFISI ZINAHITAJIKA KUWA HURU KUTOKANA NA UNYETI WA KAZI ZAO:

(I) oFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI (SASA IMEKUWA KAMA NI TAWI LA CCM)
(II) OFISI YA IGP
(III) TAKUKURU
(IV) DPP
(V) JAJI MKUU (MAHAKAMA)
(VI) USALAMA WA TAIFA
(VII) SPIKA
 
spika wa marekani ana chama.Kama hujui mambo uliza kwanza
 
kUNA OFISI ZINAHITAJIKA KUWA HURU KUTOKANA NA UNYETI WA KAZI ZAO:

(I) oFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI (SASA IMEKUWA KAMA NI TAWI LA CCM)
(II) OFISI YA IGP
(III) TAKUKURU
(IV) DPP
(V) JAJI MKUU (MAHAKAMA)
(VI) USALAMA WA TAIFA
(VII) SPIKA
nashukuru umeongelea swala la SPIKA, maana hiki ni chombo muhimu katika kutunga sheria za nchi, mambo yakipindishwa uku nchi nzima inapinda ,
bunge letu limekuwa la kuoneshana ubabe, chama gani ni bora na mambo yanajadiliwa kichama-chama, hata kwenye mambo which needs reality, people stands kutetea ujinga ili kuokoa chama. SPIKA unatakiwa kuwa neutral, ila huyu mama ana stand kwa maslahi ya chama, that is a problem,...anway inabidi tuwe kama-wamerakani, india, canada katika hili, ukitakA kuwa spika, sharti ujitoe katika chama kwanza
 
Yeah......Na chama cha siasa kinachofuga majambazi na kuwafunika huku wakijua ni majambazi kisa kinawafadhili kuendeleza udhalimuna ukibaka wake kifutwe mara moja

Majambazi yakiiba kuku majambazi! Wakiiba milioni 150 kwa mwezi sio majambazi, wakitaka kulipwa 94bilion ni watakatifu!
 
Mie napendekeza kuwepo na Tume huru ya Uchaguzi inayojumuisha vyama vyote na pia mahakama. Na kwenye hii tume mwenyekiti wake asichaguliwe na Rais bali achaguliwe kutoka Bungeni.

Pia Rais apunguziwe madaraka kama kuteuwa wabunge, pia hata wakuu wa mikoa wasichaguliwe na rais bali wapigiwe kura na wananchi ili waweze kutenda haki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…