Live: Mkutano wa CHADEMA Arusha, ni kuhusu Rasimu ya Katiba

Live: Mkutano wa CHADEMA Arusha, ni kuhusu Rasimu ya Katiba

Chadema walipendekeza serikali tatu, lakini saizi wanapiga tena hawafahamu wanapigania kitu gani.

Hata sasa CHADEMA wanapendekeza kuwe na serikali tatu yenye wabunge 314 badala ya idadi ya sasa ya wabunge 438 kwenye mfumo wa serikali mbili.
Hapo utaona mfumo wa serikali tatu una gharama nafuu kuliko mfumo wa sasa

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Maoni yangu kwenye Rasimu ya katiba Wabunge wa viti maalum,wanapopitishwa kwenye vyama vyao ,baada ya vyama kuwapitisha warudi majimboni au mikoani ili kupigiwa kura na wanawake walioko ktk majimbo yao ,kwani wanapochaguliwa na vyama hawawaheshimu wanawake kwenye majimbo ,ila wakichaguliwa na wanawake heshimu itakuwepo kwa wanawake.zaidi sana vifutwe visiwepo
 
Chadema walipendekeza serikali tatu, lakini saizi wanapiga tena hawafahamu wanapigania kitu gani.

Pilipili usiyo ila yakuwashia nini???? Mbona huongei mambo ya magamba? ???
 
Kuna kijana moja amependekeza mtu mwenye umri wa miaka 18 agombee urais, umati wote umemkataa.
Huyo kijana alivuta bangi za "zzk" na januari "ma-rope" kuwa kila mtu anaweza kuwa rais.
 
Kama vijana ndo wengi na katika marekebisho ya daftari la wapiga kura ni wazi kabisa watakao ingia kwenye orodha mpya ya wapiga kura ni vijana, nina uhakika wakimua Rais ajaye atakuwa nani na wa kada ipi! Wakiamua awe kijana atakuwa japo sio wa miaka kumi na nane! Tusewabeze vijana.
 
Maoni yangu ninayoyapendekeza katika Rasimu ya Katiba Mpya ni haya yafuatayo:
1] Iundwe Tume huru ya Uchaguzi
2] Bunge lipewe Mamlaka ya kuwaidhinisha Wateule wa Rais
3] TISS iwajibike kwa Bunge (Kamati ya Usalama ya Bunge)
4] Vyeo vya Ukuu wa Wilaya na Ukuu wa Mikoa waondolewe
5] MaGavana warejeshwe na wachaguliwe kwa njia ya sanduku la kura
6] MaMayor pia wachaguliwe na Wananchi
7] Kuwepo na Vikao vya Wabunge na Madiwani ngazi ya Majimbo
8] Kuwepo na Vikao vya Wabunge na Madiwani ngazi ya Taifa
9] Itikadi za Vyama zitambuliwe rasmi katika Katiba ijayo
10] Taifa lijitambue rasmi linafuata mrengo gani wa kisiasa na kiuchumi ili kuondokana na mikanganyiko inayotukabili kama ilivyo sasa.
11] Katiba ijayo iweke mipaka rasmi ya kimamlaka na kimaamuzi kati ya Serikali na Sekta Binafsi.Sekta Binafsi inahitaji kupumua sasa maana imezongwa sana na Serikali.
12] Katiba ijayo ikuze uhuru wa vyombo vya habari na kuvifanya muhimili mwingine wa Dola
13] Process ya kumuajibisha Rais Bungeni anapopwaya kutawala ubadilishwe
 
13] Process ya kumuajibisha Rais Bungeni anapopwaya kutawala
 
Back
Top Bottom