Wakuu zangu mbona hawa wagombea wote wanajibu jinsi wanavyopfikiria wao yaani kipi kibaya au bora kimetendeke au kingetendeka?. Kwa nini wasizungumzie mipango ambayo tayari wanayo wao kuhusiana na hoja iliyowekwa.
Kwa mfano Utalii:- Wazungumzie mfumo uliopo chini ya Utawala wa CCM kwa mapungufu yake kadhaa ambayo ni haya blaa blaa blaa na yamepoleta athari hizi na zile. Hivyo Wananchi wakinipa kura zao chama changu kina mipango hii na hii. Nitafanya yafuatayo, kwanza blaa blaa blaa ambacho tunategemea kutumia kiasi kadhaaa zitakazo toka sehemu kadhaa ili kuboresha sekta hiyo kwa muda wa miaka kadhaa. Kwa kufanya hivi tutaikuza sekta hiyo kutoka makusanyo ya pato kiasi kadhaa hadi kufikia kiasi kadhaa na pia wananchi wataweza kufaidika hivi na vile..
Yaanii mjadala mzima uwe kama picha a Blueprint ya chama na mgombea wake wanataka kufanya nini tofauti pindi wakipewa dhamana ya kuongoza badala ya kusema tu barabara inayopita mbugani haifai inakimbiza wanyama. Wewe ukipewa utafanya nini zaidi ya kuifunga ikiwa swali ni kuongeza utalii Arusha..