Live Score-Twiga Vs Zimbabwe

Live Score-Twiga Vs Zimbabwe

xlarge.jpg
 
12821599_818537368251587_6156325638566954747_n.jpg
12821599_818537368251587_6156325638566954747_n.jpg
 

Attachments

  • 12821599_818537368251587_6156325638566954747_n.jpg
    12821599_818537368251587_6156325638566954747_n.jpg
    14.9 KB · Views: 37
TANZANIA, Twiga Stars imejiweka katika mazingira magumu ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake baadaye mwaka huu Cameroon, baada ya kufungwa mabao 2-1 nyumbani na Zimbabwe jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Tanzania sasa itabidi ishinde ugenini kwa tofauti ya mabao mawili, au 2-1 ili mshindi aamuliwe kwa mikwaju ya penalti.
Katika mchezo wa leo uliohudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, Twiga Stars walianza vyema baada ya kutangulia kupata bao kupitia kwa kiungo wake mahiri, Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ dakika ya 17 kwa shuti kali la mbali baada ya kupokea pasi ya Asha Rashid ‘Mwalala’.

Stumai Abdallah wa Twiga Stars akimdhibiti Emmaculate Msipa wa Zimbabaw leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam

Iliwachukua dakika mbili tu Zimbabwe kuchomoa bao hilo baada ya Erina Jeke kusawazisha kwa shuti la mbali dakika ya 19.
Mwanahimisi Gaucho alikaribia kufunga dakika ya 39 kama si shuti lake kutoka nje na dakika 45 za kwanza zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1.
Kipindi cha pili, Twiga Stars inayofundishwa na Nasra Juma ilirudi ikiwa dhaifu zaidi na kuwaruhusu wageni kutawala mchezo.
Zimbabwe ‘waliwakera’ mamia ya Watanzania waliojitokeza Uwanja wa Chamazi baada ya kupata bao la pili dakika ya kwanza tu ya kipindi cha pili, mfungaji Erina Jeke aliyefumua shuti akimalizia krosi ya Majory Nyauwe.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Fatuna Omary, Stumai Abdallah, Maimuna Khamis/Fatuna Khatib dk73, Fatuma Issa, Annastazia katunzi, Donisia Minja, Happinnes Mwaipaja, Amina BIlali, Shlder Boniphace/Fatuma Makusanya dk21, Asha Rashid ‘Mwalala’ na Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’.
Zimbabwe; Chido Dzingirai, Felistus Muzingodi, Eunice Chibanda, Sheila makoto, Nobhule Majika, Luntet Mutokuto, Daisy Kaitano/Rejoice Kapfuvuti dk75, Emmaculate Msipa, Majory Nyauwe, Erina Jeke/Mavis Chirandu dk79 na Rudo Neshamba/Patience Mujuru dk90.
 
TWIGA YASHINDWA KUTAMBA NYUMBANI BAADA YA KUCHAPWA NA DADA ZAKE KAMUSOKO


Pamoja na kuwa nyumbani, Twifa Stars imeshindwa kuonyesha ujuzi baada ya kukutana na kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Zimbabwe.
Kinadada wa Zimbabwe wameonyesha wanaweza kama sifa ambazo amekuwa akipata kaka yao, Thabani Kamusoko anayekipiga Yanga.

Kwani pamoja na Twiga Stars kujiandaa vilivyo, imeshindwa kuwazuia kinadada hao wa Zimbabwe ambao walionyesha soka safi katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.
Kipigo hicho kinaifanya Twiga Stars kuwa na wakati mgumu kwa kuwa italazimika kucheza na kushinda katika mechi ijayo ikiwa ugenini.

Zimbabwe ni kati ya timu tano bora kabisa barani Afrika kwa upande wa soka la wanawake na Twiaga Stars ilikuwa na kazi ya kuuangusha mbuyu huo lakini ikashindikana.
 
Back
Top Bottom