Kwakweli Yanga ilicheza vizuri sana kipindi cha kwanza,na cha pili kidogo. Ila haikuweza kuzitumia nafasi zao vizuri. Ndiyo maana timu imekosa nafasi nyingi sana za wazi za magoli.
Kwa mchezo wa mtoano,nafasi ilizopoteza,itazijutia. Kwani kule Cairo hata kama uwanja hautakua na mashabiki,fitna zitatawala.
Licha ya kucheza vizuri,kilichotakiwa kutoka kwa Yanga ni ushindi. Hivyo matokeo ya 1 - 1 ni ushindi kwa Zamalek.
Tusianze kutafuta visingizio kwamba kutakuwa na fitina kwenye mechi ya marudiano, wote ni mashahidi wa mpira ulivyokuwa, yanga wamecheza vizuri labda walikuwa na hofu tu kwani walipaswa kutumia nafasi walizozipta vizuri, ila Zamalek ni timu nzuri hata bila fitina na hizi timu zinajua jinsi ya kutumia advantage ya kucheza nyumbani sio timu zetu za simba na yanga.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.