Live streaming kutoka Bukoba: Mapokezi ya Mwili wa Ruge Mutahaba

Huyu jamaa kama angejua watu wanampenda hivi asingegombanaga na watu huku dunian

Sent using Jamii Forums mobile app

hajagombana na mtu yeyote ila alikuwa anawanyoosha wasanii waliokuwa hata hawatambuliwi hata na BASATA,hawaeleweki mbele ya wazazi,mbele ya jamii,kila kona kuna makundi ya wahuni,mkiwa wasanii wa arusha kama weusi mkienda mwanza mnafanyiwa fujo kwenye matamasha na makundi ya wavuta bangi kama dudu baya.Kuna kipindi fulani makundi ya hawa wauni akina lord eyes walishawahi kukodi costa kutoka arusha kwenda dsm na kuzunguka mitaani wakienda kufanya fujo.yani ukihudhuria matamasha na demu wako asiposhikwa makalio mbele yako ujue mkojo mtarushiwa,msanii fulani akipanda jukwaani unashangaa wahuni wamemwibukia na kuanza kumshushia kipigo,kwa kusema machache mpaka nitakapokuja na uzi maalumu msanii analewa na kula bangi anapanda jukwaani amechelewa au hatokei kabisa.Kwa hiyo malicious marketer,Ruge ,kwa maana ya jina lake ''MSIMAMIZI''alipotaka kunyoosha mambo na kuondoa takataka ndani ya tasnia ya burudani ,ili aweze kujenga uaminifu kwenye jamii na wadhamini ,kutengeneza ''muziki kazi''muziki pesa''ndipo alipojipata katika kutengeneza maadui.
Na kwa sababu alikuwa ni mdau mkubwa sana na alitambulika hivo ndani na nje,hivyo kukosana nae ilikuwa upate shida mjini,maana ni kama dreva wa basi la abood amtukane boss wake halafu akaombe kazi shabiby,bila kujua wote hawa ni ndugu kibiashara,wana umoja wao wa mabasi.Na kama udereva ni last option huna plan B,utajuta kuzaliwa mjini.R.I.P Rugemalira Mutahaba.(Msimamizi wa wanaotaka kupotea mpaka wanyooke).
 
Mmekuelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakumbuka dudu baya alimpiga Mr Nice akafungiwa,Kala pina nae alishawahi fungiwa kwa vurugu zake
 
manaa ya neno mutahaba ni MSITOKE KWENYE NJIA
 
Hii nairusha hapa akielezea kuongelewa vibaya na Jaydee

Duh kumbe.. huyo mwanamke ajionee aibu

Aibu gani , aliyoyasema Jide ni ukweli mtupu acheni UNAFKI

Sent from my Iphone using Tapatalk
 
Hapa ndipo ambapo mwili wa mpendwa wetu, Ruge Mutahaba utapumzishwa kwenye makazi yake ya milele, Kijijini kwao Kiziru-Kabale, Bukoba, kesho Jumatatu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…