omutimbasafi
JF-Expert Member
- Oct 17, 2017
- 609
- 770
Huyu jamaa kama angejua watu wanampenda hivi asingegombanaga na watu huku dunian
Sent using Jamii Forums mobile app
hajagombana na mtu yeyote ila alikuwa anawanyoosha wasanii waliokuwa hata hawatambuliwi hata na BASATA,hawaeleweki mbele ya wazazi,mbele ya jamii,kila kona kuna makundi ya wahuni,mkiwa wasanii wa arusha kama weusi mkienda mwanza mnafanyiwa fujo kwenye matamasha na makundi ya wavuta bangi kama dudu baya.Kuna kipindi fulani makundi ya hawa wauni akina lord eyes walishawahi kukodi costa kutoka arusha kwenda dsm na kuzunguka mitaani wakienda kufanya fujo.yani ukihudhuria matamasha na demu wako asiposhikwa makalio mbele yako ujue mkojo mtarushiwa,msanii fulani akipanda jukwaani unashangaa wahuni wamemwibukia na kuanza kumshushia kipigo,kwa kusema machache mpaka nitakapokuja na uzi maalumu msanii analewa na kula bangi anapanda jukwaani amechelewa au hatokei kabisa.Kwa hiyo malicious marketer,Ruge ,kwa maana ya jina lake ''MSIMAMIZI''alipotaka kunyoosha mambo na kuondoa takataka ndani ya tasnia ya burudani ,ili aweze kujenga uaminifu kwenye jamii na wadhamini ,kutengeneza ''muziki kazi''muziki pesa''ndipo alipojipata katika kutengeneza maadui.
Na kwa sababu alikuwa ni mdau mkubwa sana na alitambulika hivo ndani na nje,hivyo kukosana nae ilikuwa upate shida mjini,maana ni kama dreva wa basi la abood amtukane boss wake halafu akaombe kazi shabiby,bila kujua wote hawa ni ndugu kibiashara,wana umoja wao wa mabasi.Na kama udereva ni last option huna plan B,utajuta kuzaliwa mjini.R.I.P Rugemalira Mutahaba.(Msimamizi wa wanaotaka kupotea mpaka wanyooke).