Live Updates: Azam FC v Mtibwa Sugar FC - 11/02/2015

Makoye Matale

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2011
Posts
6,491
Reaction score
2,104
Leo tarehe 11/02/2015 majira ya saa 10 jioni kutakuwa na kipute cha aina yake pale Azam FC Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara watakapowaalika wakata miwa wa Mtibwa kutoka Manungu, Turiani mkoani Morogoro. Mchezo huo utafanyika katika uwanja wa Azam Complex Jijini Dar es Salaam.

Azam FC inaingia uwanjani ikiwa na kijeraha cha kutoa sare na Polisi Morogoro ya bao 2-2 na Mtibwa Sugar itaingia uwanjani ikiwa na jeraha la kufungwa bao 2-0 na timu ya Wananchi.

Kwa vyovyote vile, huu ni mchezo mgumu kwa timu zote, yafuatayo ni mavuno ya timu hizi kama yanavyoonekana katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015 hadi sasa:-

PositionTeamPWDLGAGFGDPoints
2
Azam FC

[TD="colspan: 10"]
PARTIAL VPL STANDING TABLE
[/TD]

[TD="width: 30, bgcolor: transparent"]
12
[/TD]
[TD="width: 35, bgcolor: transparent"]
6
[/TD]
[TD="width: 31, bgcolor: transparent"]
4
[/TD]
[TD="width: 28, bgcolor: transparent"]
2
[/TD]
[TD="width: 38, bgcolor: transparent"]
10
[/TD]
[TD="width: 38, bgcolor: transparent"]
17
[/TD]
[TD="width: 40, bgcolor: transparent"]
7
[/TD]
[TD="width: 59, bgcolor: transparent"]
22
[/TD]

[TD="width: 78, bgcolor: transparent"]
6
[/TD]
[TD="width: 114, bgcolor: transparent"] Mtibwa Sugar [/TD]
[TD="width: 30, bgcolor: transparent"]
12
[/TD]
[TD="width: 35, bgcolor: transparent"]
4
[/TD]
[TD="width: 31, bgcolor: transparent"]
6
[/TD]
[TD="width: 28, bgcolor: transparent"]
2
[/TD]
[TD="width: 38, bgcolor: transparent"]
9
[/TD]
[TD="width: 38, bgcolor: transparent"]
13
[/TD]
[TD="width: 40, bgcolor: transparent"]
4
[/TD]
[TD="width: 59, bgcolor: transparent"]
18
[/TD]

Hakuna shaka Azam FC itashangiliwa kwa nguvu na 'MIKIA' na Mtibwa Sugar itapata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wa timu ya Wananchi. Mashabiki wa Azam watapata ahueni pale Steve Azam atakapopata ruksa ya kukaa jukwaa la mikia kwa siku ya leo.

Pamoja na majigambo lukuki kutoka kwa mnenaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, dakika 90 pekee ndizo zitaamua mshindi katika mchezo wa leo.

Makoye Matale
anazitakia kila la heri timu zote katika mchezo huo.
==============================

20' Goaaaaaal: Dakika ya ishirini Azam wanaandika bao la kwanza, Kipa anautoa mpira cm chache baada ya mstari hivyo kuhesabika goli.

27' Goaaaaaal: Dakika ya ishirini na saba Azam wanaandika bao la pili, Domayo anafunga bao jingine. Pasi nzuri kutoka winga ya kushoto na Domayo bila papara anaingiza wavuni.

34' Goaaaaaal: Mussa Mohammed wa Mtibwa anarudisha bao moja kwa timu ya Mtibwa baada ya Azam kutofanya marking yao vizuri

40' Goaaaaaal: Kavumbagu anaiandikia Azam bao la tatu baada ya pasi nzuri kutoka kwa sure boy

*Timu zinaenda mapumziko Azam ikiwa inaongoza kwa mabao 3 dhidi ya moja la Mtibwa

*Timu zimerudi kutoka mapumziko na mambo yanaendelea hapa uwanja wa Azam complex


Full Time: Azam 5-2 Mtibwa Sugar.
 

Attachments

  • Azam.png
    14.2 KB · Views: 1,432
  • Mtibwa Sugar.png
    13.6 KB · Views: 1,424
Last edited by a moderator:
Mkuu tupo majukwaa JF yapo mengi huku na majukumu ya ujenzi wa Taifa yanasubiri. Bado ibada nazo zinasubiri saas kwa kuwa huku hakukuwa na tukio tumeona tujikite huko.

Hata hivyo leo Mwenye kiti chake anakalia maana chakuazima hakisitiri makota...
 
Ningefurahi sana kama wangetoshana nguvu kwa kutoa sare tena ya bila kufungana.
 
Mkuu tupo majukwaa JF yapo mengi huku na majukumu ya ujenzi wa Taifa yanasubiri. Bado ibada nazo zinasubiri saas kwa kuwa huku hakukuwa na tukio tumeona tujikite huko.

Hata hivyo leo Mwenye kiti chake anakalia maana chakuazima hakisitiri makota...

Unaota wewe!!!! Azam ndo aliazima kiti sasa ameamua kurudisha kwa mwenyewe. Yanga ndo bingwa mpya 2014/2015.
 
Unaota wewe!!!! Azam ndo aliazima kiti sasa ameamua kurudisha kwa mwenyewe. Yanga ndo bingwa mpya 2014/2015.
Endelea kuota ikishindikana weka na mbolea ya minjingu....Ubingwa wenu ni kuongoza ligi mwezi wa pili tu na kuchukua mbao ya hisani pekee ambao hata pesa hakuna.

Kuongoza ligi siyo ishu hata Mtibwa aliongoza tena kwa muda mrefu kuliko nyingi wa kubahatisha leo hii yuko wapi?
 

Haya sasa wacha tuseme ubingwa utakuwa wa mikia, wazee wa mabonanza. labda utaridhika
 
Unaota wewe!!!! Azam ndo aliazima kiti sasa ameamua kurudisha kwa mwenyewe. Yanga ndo bingwa mpya 2014/2015.

Kombe hilo ni la Yanga wengine huwa wanalipora tu, vivyo hivyo hata kiti cha uongozi wa ligi ni wa Yanga hao Azam na Mtibwa pamoja na mikia ni waporaji tu. Endapo Azam atashinda kwa tofauti ya goli moja, ataongoza kwa kutumia herufi A dhidi ya Y ya Yanga. Wakitoka sare kwetu sisi itakuwa ni furaha tele kwani vita vya panzi ni furaha ya kunguru.
 

Tena iwe sare ya kutofungana.Iwe hivi; FT Azam 0-0 Mtibwa.
 
Soka lina watu wake nyie angaikeni lakini mwisho wa siku Simba ndo atakuwa bingwa msimu huu
 
Soka lina watu wake nyie angaikeni lakini mwisho wa siku Simba ndo atakuwa bingwa msimu huu

Kwani huu ni msimu wa ngapi hamjawahi hata kushika nafasi ya pili!!! Wewe jidanganye tu, Eti simba ndo atakuwa bingwa msimu huu!! Hivi wewe ni mzima kweli??
 
Lambalamba 1-0 wakata miwa. Mtibwa sijui kwanini imekubali kuwa underdog mbele ya azam!!?
 
Kwani huu ni msimu wa ngapi hamjawahi hata kushika nafasi ya pili!!! Wewe jidanganye tu, Eti simba ndo atakuwa bingwa msimu huu!! Hivi wewe ni mzima kweli??

mkuu angalia table kwa makini mtu wa kwanza kampita simba points 8 ni mechi 3 hizo mbona inawezeka tena bila miujiza ukizingatia ndo kwanza round ya 2 imeanza. Simba ndo bingwa bila kumung'unya maneno
 
Tobias Kifaru mjinga sana huyu jamaa pamoja na Mexime wake, wao wanaiandaa timu yao kwa ajili ya kupambana na yanga tu, Acha wapigwe tu hata ikiwezekana wale 5-0.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…