Live Updates: Azam FC v Mtibwa Sugar FC - 11/02/2015

Dak ya 34 mtibwa wanapata goli, Azam 2-1 Mtibwa.
 
Mikia msimu ujao mnaenda kuungana na Polisi Dodoma,Rhino na wengineo.
 
mkuu angalia table kwa makini mtu wa kwanza kampita simba points 8 ni mechi 3 hizo mbona inawezeka tena bila miujiza ukizingatia ndo kwanza round ya 2 imeanza. Simba ndo bingwa bila kumung'unya maneno

mwambie huyoo!!!!! mpira utadunda tuu!
 
Wakata miwa wanapigwa la 3. Azam 3-1 Mtibwa.
 
wenye soka wapo tuliii,! simba my club normally to win!!!!

rage wahurumie mashabiki wa mikia jina ulilowapa nikama uliwalaani maana wanaishi maisha ya ndotoni ya kulta umejenga nyumba angani ukiamka upo kwenye nyumba ya tope
 
Wamechukua chao nini, mbona wanafungwa kirahisi hivi?

Yawezekana walitumia nguvu nyingi kwenye mchezo dhidi ya yanga, wanaweza wakapigwa mpaka 5. Acha wapigwe tu ili siku nyingine waache tabia ya kuikamia yanga wajue ligi hii inashirikisha timu nyingi sio yanga pekee.
 
mkuu angalia table kwa makini mtu wa kwanza kampita simba points 8 ni mechi 3 hizo mbona inawezeka tena bila miujiza ukizingatia ndo kwanza round ya 2 imeanza. Simba ndo bingwa bila kumung'unya maneno

Tangu ligi imeanza mko huko huko chini mkishika nafasi ya 11, mlipocharuka mlishika nafasi ya 7 mkaporomoka tena hadi nafasi ya 9 mlipo sasa hivi. Kuna miujiza gani unayoitegemea kuifikisha Simba kileleni?
 
Yawezekana walitumia nguvu nyingi kwenye mchezo dhidi ya yanga, wanaweza wakapigwa mpaka 5. Acha wapigwe tu ili siku nyingine waache tabia ya kuikamia yanga wajue ligi hii inashirikisha timu nyingi sio yanga pekee.

Nakubali.
 
Hili ndio tatizo la mashabiki wa Yanga, kwa nini usiseme kwamba timu ya Azam ni nzuri kuliko ya kwenu? Na huo ndo ukweli Azam kwa sasa wana timu nzuri kuliko timu zote za ligi kuu na wasipojisahau au kupata majeruhi wana asilimia kubwa sana ya kutetea ubingwa.
 
Sema Azam ni bora kuliko Mtibwa na Simba, Yanga ni habari nyingine Mkuu.
 
Sema Azam ni bora kuliko Mtibwa na Simba, Yanga ni habari nyingine Mkuu.
Tatizo ndo ninalolisema, nyie mnaamini kila msimu timu yenu ni nzuri kuliko timu zote na mkifungwa hamtaki kukubali kwamba mmezidiwa ila mnaamini huwa mnafungwa kwa hujuma au ujanja ujanja mwingine lakini ndugu yangu Makoye Matale nikuambie tu kwa msimu huu Azam wako vizuri kuliko timu yoyote ya ligi kuu.

Kuna vitu viwili vinachangia kupata ushindi, uwezo wa timu pamoja na bahati siku inapotokea Azam wamekosa ushindi ni kwa sababu tu wamekosa bahati lakini kiukweli hata ukichukua mchezaji mmoja mmoja Azam wana wachezaji wazuri wengi tu na ndo hicho kinafanya timu yao iwe nzuri kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…