Jospina
JF-Expert Member
- Apr 19, 2013
- 2,421
- 1,395
kindumbwe ndumbwe cha ligi kuendelea tena kesho. Pale mjini tanga ndani ya dimba la mkwakwani watakutana yanga sc na wagosi wa kaya coastal union.
ni moja kati ya mechi ngumu sana kwa timu zote mbili ukiangalia aina ya uchezaji, tension ya mechi na jinsi gani timu zote zilivyo pambana kabla ya mechi hiyo.
coastal union wamecheza mechi 12 , wameshinda mechi 4 na kwenda sare mechi 5 . Coastal wamefungwa mechi mbili. Katika mchanganuo huo imejikusanyia pointi 17.
ukiwatizama yanga sc wao wamecheza mechi 11 huku wakishinda mechi tano tu , sare mechi nne na kufungwa mechi 2 sawa na coastal. Wakati coastal akishinda mechi 4 katika 12, yanga kashinda mechi 5 katika mechi 11. Hapo utaona kimbembe kilivyo katika safu zote za ushambuliaji na ulinzi.
Wakati yanga sc wakipitia msuguano mkali wa kisaikolojia kutokana na timu kutoridhisha kwa kiwango chake hasa eneo la ushambuliaji, coastal wao ni zaidi ya siku tano wamekuwa na muda mzuri wa kujiandaa kutafuta ushindi dhidi ya wakongwe hao wa ligi kuu tanzania bara. Yote kwa yote tunatarajia mchezo mzuri na wa kuvutia kwa sababu timu zote zinatumia mfumo na patterns zinazo shabihana.
All the best coastal union
===========
===========
Matokeo ya Mwisho: Coastal Union 0 - 1 Yanga Afrika

Ligi Kuu ya Vodacom
Raundi ya ** (Kiporo)
Uwanja wa CCM Mkwakwani
Saa 10 Jioni
Coastal Union vs Yanga Afrika