Live Updates: FC Platinum vs Simba SC, Uwanja wa Taifa - Zimbabwe

Da Gladiator

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2020
Posts
1,641
Reaction score
2,646
CAF CHAMPIONS LEAGUE QUALIFICATIONS.

Raundi ya kwanza, mkondo wa kwanza.

(Oooh, Ataepita mikondo(aggregates) yote miwili ataingia hatua ya makundi moja kwa moja. )

10:00 JIONI: FC Platinum, Zimbabwe v Simba SC, Tanzania

UWANJA: Uwanja wa Taifa, Harare- Zimbabwe.

ITAONESHWA MUBASHARA: Azam Sports HD 1.

Na. Da Gladiator.

Patashika ya ligi ya mabingwa Afrika kufuzu hatua ya makundi, raundi ya kwanza, mkondo wa kwanza, kuendelea leo Jumatano 23, Disemba 2020. Leo zitapigwa mechi kifutu katika viwanja mbalimbali. Lakini katika uwanja wa Taifa Harare-Zimbabwe kuna bonge la mechi kati ya Simba SC, Tanzania na FC Platinum, Zimbabwe.

Hii ni baada ya mnyama huyo mkali mwituni Simba SC kuwaondosha kwa aibu raundi ya awali, mabingwa wa nchi bora, kubwa na maarufu kisoka Plateau Utd FC ya nchini Nigeria na Luis Miquisson kuibuka mchezaji bora wa mechi zote mbili na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo.

Mkondo wa kwanza.
Plateau Utd FC 0-1 Simba SC,
Goli: C C Chama, 59'.

Mkondo wa pili.
Simba 0-0 Plateau Utd FC.

Je, Simba SC ama FC Platinum kuibuka mbabe? Kaa nami/nasi usikose ukahadithiwa. Kumbuka mtanange ni kuanzia saa 10:00 jioni.

Nyongeza;

Usisahau kuwa UTO leo wanacheza mchezo wao wa kimataifa, Uwanja wa Sokoine-Mbeya, wamesafiri usiku kucha kwa basi maana mbeya ni mbali, na sidhani kama watatoka salama, maana si kwa yale madera yao .

"Kulitaka mwana, kulipewa mwana".
#SimbaNguvuMoja.
#AnotherLevel.

Karibuni kwa michango yenu.
View attachment 1657649
 
CAF CONFEDERATION CUF QUALIFICATION.
2nd round

(Ataepita hapa, atacheza 'round' moja ya mwisho.)

1700Hrs: Namungo FCTanzania, v Al Hilal , Sudan Rep.

Venue: Azam Complex
 
SIMBA SC, KUWAKOSA WATANO(5) LEO KIMATAIFA.
SIMBA leo Desemba 23 ikiwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya FC Platinum ya Zimbabwe kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza itawakosa nyota wake watano.

Nyota hao ni pamoja na :-Bernard Morrison yeye yupo Bongo akiendelea kupata matibabu kwa kuwa hakuwa fiti kiafya. Charlse Ilanfya pia yupo Bongo akiendelea na programu ambayo amepewa na Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck.

Kipa namba moja Aishi Manula yeye alikaa langoni kwenye mechi mbili zilizopita za kimataifa dhidi ya Plateau United anasumbuliwa na majeraha baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya KMC, Uwanja wa Mkapa.

Kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu Bara alitumia dakika 45 wakati Simba ikishinda bao 1-0 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na Meddie Kagere.

John Bocco nahodha wa Simba naye pia aliumia kwenye mchezo dhidi ya KMC ulikuwa ni wa Ligi Kuu Bara. Kwa mujibu wa Kocha Mkuu, Vandenbroeck hawa watakosekana kwenye mchezo wa leo.

Thadeo Lwanga, ingizo jipya ndani ya Simba, kwa mujibu wa Barbara Gonzalez ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Simba alisema kuwa kumekuwa na ugumu wa kupata vibali vyake.

Salehjembe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…