Live Updates: FC Platinum vs Simba SC, Uwanja wa Taifa - Zimbabwe

Live Updates: FC Platinum vs Simba SC, Uwanja wa Taifa - Zimbabwe

CAF CHAMPIONS LEAGUE QUALIFICATIONS.

Raundi ya kwanza, mkondo wa kwanza.

(Oooh, Ataepita mikondo(aggregates) yote miwili ataingia hatua ya makundi moja kwa moja. )

10:00 JIONI: FC Platinum, Zimbabwe v Simba SC, Tanzania

UWANJA: Uwanja wa Taifa, Harare- Zimbabwe.

ITAONESHWA MUBASHARA: Azam Sports HD 1.

Na. Da Gladiator.

Patashika ya ligi ya mabingwa Afrika kufuzu hatua ya makundi, raundi ya kwanza, mkondo wa kwanza, kuendelea leo Jumatano 23, Disemba 2020. Leo zitapigwa mechi kifutu katika viwanja mbalimbali. Lakini katika uwanja wa Taifa Harare-Zimbabwe kuna bonge la mechi kati ya Simba SC, Tanzania na FC Platinum, Zimbabwe.

Hii ni baada ya mnyama huyo mkali mwituni Simba SC kuwaondosha kwa aibu raundi ya awali, mabingwa wa nchi bora, kubwa na maarufu kisoka Plateau Utd FC ya nchini Nigeria na Luis Miquisson kuibuka mchezaji bora wa mechi zote mbili na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo.

Mkondo wa kwanza.
Plateau Utd FC 0-1 Simba SC,
Goli: C C Chama, 59'.

Mkondo wa pili.
Simba 0-0 Plateau Utd FC.

Je, Simba SC ama FC Platinum kuibuka mbabe? Kaa nami/nasi usikose ukahadithiwa. Kumbuka mtanange ni kuanzia saa 10:00 jioni.

Nyongeza;

Usisahau kuwa UTO leo wanacheza mchezo wao wa kimataifa, Uwanja wa Sokoine-Mbeya, wamesafiri usiku kucha kwa basi maana mbeya ni mbali, na sidhani kama watatoka salama, maana si kwa yale madera yao .

"Kulitaka mwana, kulipewa mwana".
#SimbaNguvuMoja.
#AnotherLevel.

Karibuni kwa michango yenu.

Tupo hapa tunafatilia
 
Leo nawai mapema sanaa nakaa mbele kabisa

Ila suluhu itakuwa poa sana kuliko kufungwa goli zaid ya moja.

Tusiende na matokeo mfukoni
Simba SC wengi ni wanamichezo, hivo sidhan kama kuna mtu ataenda na matokeo mfukoni

"Nasema uongo ndugu zangu ???!"
 
Powered by facebook.
Ona.
IMG-20201223-WA0006.jpg
 
Nguvu moja leo ushindi lazima tutampiga hapo hapo kwao huyo Platinum.

Kikosi kikiwa hivi itakuwa bora Sana

1 Beno Kakolanya
2 Shomari Kapombe
3 Zimbwe JR
4 Onyango
5 Wawa
6 Erasto Nyoni
7 Hassan Dillunga
8 Jonas Mkude
9 Made Kagere
10 CC Chama
11 Luis Miqussion.

Hapo tutalinda zaidi hasa eneo la katikati (makosa ya mdhamiru na Ndemla yatatugharimu kwa ugenini Kama wakicheza).
Pia tutaweza kushambulia zaidi kwa kutumia mawinga hao wawili Luis na Dillunga wakisaidiwa na mabeki wa pembeni Shom K na Zimbwe JR .
Eneo la kati kati Jonas Mkude na Nyoni wanaweza kumchezesha Chama pale juu ambaye anaweza kuwa hatari zaidi akitokea katikati huku mbele yake kukiwa na MK14 kwenye box mtu hatari sana.

Pia Nyoni atakuwa na faida zaidi kwa kuwalinda mabeki wa kati Wawa Onyango ( uzoefu utawabeba )

Simba nguvu moja.
 
Nguvu moja leo ushindi lazima tunpiga hapo hapo kwao huyo Platinum.

Kikosi kikiwa hivi itakuwa bora Sana

1 Beno Kakolanya
2 Shomari Kapombe
3 Zimbwe JR
4 Onyango
5 Wawa
6 Erasto Nyoni
7 Hassan Dillunga
8 Jonas Mkude
9 Made Kagere
10 CC Chama
11 Luis Miqussion.
Mkuu, kati ya Bocco au Manula aidha watacheza wote au atacheza mmoja.

Kumbuka taarifa inasema kucheza kwao ni 50/50.
 
Nguvu moja leo ushindi lazima tunpiga hapo hapo kwao huyo Platinum.

Kikosi kikiwa hivi itakuwa bora Sana

1 Beno Kakolanya
2 Shomari Kapombe
3 Zimbwe JR
4 Onyango
5 Wawa
6 Erasto Nyoni
7 Hassan Dillunga
8 Jonas Mkude
9 Made Kagere
10 CC Chama
11 Luis Miqussion.
So far, kikosi cha kibabe sana mkuu.
 
Nguvu moja leo ushindi lazima tunpiga hapo hapo kwao huyo Platinum.

Kikosi kikiwa hivi itakuwa bora Sana

1 Beno Kakolanya
2 Shomari Kapombe
3 Zimbwe JR
4 Onyango
5 Wawa
6 Erasto Nyoni
7 Hassan Dillunga
8 Jonas Mkude
9 Made Kagere
10 CC Chama
11 Luis Miqussion.
Umepanga kikosi[emoji38]

Mzamiru lazima aanze chaguo la kocha

Ngoja tusubiri Kocha atakujaje?
 
Back
Top Bottom