Live Updates: FC Platinum vs Simba SC, Uwanja wa Taifa - Zimbabwe

Kama kuna mechi ambayo haijanipa pressure ni hii ya leo ya Platinum 1 - 0 Simba hadi dk 90'. Vyura wenyewe wanajua kuwa tayari Simba anaenda kuingia makundi.

Huu uzi tuutunze kwa ajili ya ukumbusho wa baadaye. Waitress fanya fasta 🍺 nijipongeze kabla ya kuwaua Platinum na Vyura hapo January.
 
.... jipeni moyo tuuu, labda muingie makundi ya WhatsApp....
 
Simba wamecheza mpira sana lakini wamekosa mbinu za ushindi. Platinum wamecheza kidogo lakini walikuwa na mbinu bora kabisa na mpango kazi wao umefanya kazi vizuri. Waliwaacha Simba wacheze "square pass" kwenye nusu yao kisha wao walikuwa wanavamia Simba inapovuka mstari wa katikati kisha wakiupata mpira wanaenda kwa kasi kwenye goli la Simba. Pasi nyingi za Simba zilikuwa hazina madhara makubwa kwa sababu walikuwa muda mwingi wanacheza kwenye nusu ya kwao. Na mbaya zaidi viungo wa Simba walipopata mipira walikuwa wanageukia nyuma kwenye goli lao badala ya kugeukia mbele kwa kasi.

Simba lazima wajifunze mbinu ya kushambulia kwa kasi na kushtukiza pale wanapomnyang'anya adui mpira. Waache kukariri kuwa mpira lazima uanze nyuma kwa mabeki wote waugusue halafu wanampa kiungo wakati huo adui anajipanga upya watu saba mpaka nane nyuma ya mpira. Mara nyingine wanapaswa wapeleke mipira kwa washambuliaji wao haraka ili wawalazimishe mabeki wa timu pinzani wafanye makosa. Inasikitisha kwakweli mpira umebaki dakika 15 uishe bado timu inang'ang'ania kucheza "square pass" kwenye nusu yao.

Na ni muda muafaka sasa Simba ivunje benki ili ipate walau beki mmoja wa katikati wa kuaminika wakati huo huo wakianza kumwamini na kumpa majukumu Ame. Na ijiandae kisaikolojia kucheza bila ya Wawa kwani akili yake inataka lakini mwili wake umeanza kumgomea.
 
Good point
 
Umeongea point mzee baba hili limekuwa gonjwa sugu Sana kwa Simba
 
Uko sahihi, pia Simba inatakiwa kusajili striker kijana mwenye uwezo mkubwa na iachane na usajili wa wazee.
 
Sawa Ambangile wamekuelewa. Na yule tajiri yao alivyo na mkono wa birika. Atavunja kweli benki?
 
Pia kwanini anachukua kocha wa bei rahisi kwa sababu yule kocha kiukweli ni wa bei ya chini
Mo ni bahiri wakati anataka mafanikio ndani ya timu, haiwezekani. Anataka timu ifike nusu fainali wakati ndani ya timu hakuna mchezaji ambaye amewahi kuisadia timu yoyote kufika kilele cha mafanikio kwenye mashindano ya Champion League.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…