Live Updates: FC Platinum vs Simba SC, Uwanja wa Taifa - Zimbabwe

Live Updates: FC Platinum vs Simba SC, Uwanja wa Taifa - Zimbabwe

Simba wamecheza mpira sana lakini wamekosa mbinu za ushindi. Platinum wamecheza kidogo lakini walikuwa na mbinu bora kabisa na mpango kazi wao umefanya kazi vizuri. Waliwaacha Simba wacheze "square pass" kwenye nusu yao kisha wao walikuwa wanavamia Simba inapovuka mstari wa katikati kisha wakiupata mpira wanaenda kwa kasi kwenye goli la Simba. Pasi nyingi za Simba zilikuwa hazina madhara makubwa kwa sababu walikuwa muda mwingi wanacheza kwenye nusu ya kwao. Na mbaya zaidi viungo wa Simba walipopata mipira walikuwa wanageukia nyuma kwenye goli lao badala ya kugeukia mbele kwa kasi.

Simba lazima wajifunze mbinu ya kushambulia kwa kasi na kushtukiza pale wanapomnyang'anya adui mpira. Waache kukariri kuwa mpira lazima uanze nyuma kwa mabeki wote waugusue halafu wanampa kiungo wakati huo adui anajipanga upya watu saba mpaka nane nyuma ya mpira. Mara nyingine wanapaswa wapeleke mipira kwa washambuliaji wao haraka ili wawalazimishe mabeki wa timu pinzani wafanye makosa. Inasikitisha kwakweli mpira umebaki dakika 15 uishe bado timu inang'ang'ania kucheza "square pass" kwenye nusu yao.

Na ni muda muafaka sasa Simba ivunje benki ili ipate walau beki mmoja wa katikati wa kuaminika wakati huo huo wakianza kumwamini na kumpa majukumu Ame. Na ijiandae kisaikolojia kucheza bila ya Wawa kwani akili yake inataka lakini mwili wake umeanza kumgomea.
Mkuu ubarikiwe.
 
Sio kweli mkuu , walikuwa bora kwa lipi ?!
kulikua na wachezaji hatari Kama vile Thabani Kamusoko, Donald Ngoma,Aubrey Chirwa


Lkn nilivyoangalia kikosi Cha Jana labda yule chikwende ndo msumbufu


forward yenu ndio imewanyima ushindi Simba mna'mic Script wachezaji wenu Kuna muda wanatembea uwanjani....BTW maliza mchezo home tinga 16 bora. Nafasi unayo mbele ya mashabiki wako elf 30
 
Wanakuja lini tukawapokee

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Tarehe hii,
IMG-20201224-WA0001.jpg
 
Back
Top Bottom