Live Updates Kagera Sugar vs Simba kwa huzuni kubwa sana baada ya kupata msiba

Live Updates Kagera Sugar vs Simba kwa huzuni kubwa sana baada ya kupata msiba

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Mnyama leo anaingia uwanjani akiwa amenyong'onyea sana baada ya kupoteza wanachama wake kadhaa katika ajali ya basi iliyotokea jana jion. wachezaji na viongozi wa simba wanaingia uwanjani wakiwa na huzuni kubwa sana hasa katika kipindi hiki kigumu.
hata hivyo tutawaletea live updates kati ya Kagera Sugar vs Simba kwa unyonge na huzuni kubwa sana.


MECHI IMEHARISHWA KUTOKANA NA UWANJA KUJAA MAJI . TUTAKUTANA TENA WAKATI UJAO
 
Daaaa niliumia sana kuwapoteza mashabiki wa ukweli ila Simba inasonga mbele
 
wachezaji wana huzuni na kuna wengi wameomba kama mech ingehaiishwa ili wakashiriki katika shughuli za mazishi au pengine tu kuhuzunika pamoja na wanachama wengine wa simba. ki ukweli wanaingia uwanjan kutimiza tu wajibu ila morali haipo kabisa
 
Na mvua iliyonyesha Shinyanga toka asubuhi,kuna mchezo hapo?
 
Simba wametoa kafara watu wake. Mtabaki na makombe yenu yale tu.

Unakumbuka walichinjwa uwanja huohuo na mateja wa stand united? wameamua kutoa kafara washinde bahati mvua imenyesha. tusubiri siku ya kurudiana sijui watamtoa nani
 
Kwa Kafara ya jana kisha leo mvua naweza amini Simba anachukua ndoo
 
pole sana watani, comment ni moja ya utani pia be strong SIMBA JIKE utazaa soon!!!
 
Kwa hiyo mechi ya Kagera Sugar na Simba inachezewa Shinyanga? Kwa nini?

Tiba
 
Kwa hiyo mechi ya Kagera Sugar na Simba inachezewa Shinyanga? Kwa nini?

Tiba

Ndio uwanja wao wa nyumbani; Miaka yote walikuwa wanatumia uwanja wa Kaitaba ulioko Bukoba kama uwanja wa nyumbani lakini mwaka huu uwanja ule unafanyiwa matengenezo makubwa (ukarafati), wakati uwanja wa Kaitaba ukiwa kwenye matengenezo makubwa ilibidi wahamie uwanja ulio karibu na Bukoba na wao wakachagua kuhamia CCM Kirumba ulioko Mwanza baada ya kuutumia ule uwanja kwa mechi tatu na kufungwa zote waliona CCM Kirumba hapawafai hivyo wakaamua kuhamia uwanja wa Kambarage ulioko Shinyanga na ndo unaotumia kama uwanja wao wa nyumbani.
 
Back
Top Bottom