wabongo tuna tatizo moja, tunadhani Simba alipofikia na kupapongzwa na kuandika vichwa vya habari eti "Simba yafa Kiume" huu ni upuuzi ambao tunao miaka nenda rudi, juzijuzi kuna mdau mmoja wa Simba (sijui kama ni mdau kweli wa wa kibiashara) anaitwa Azim Dewji alikua akilaani simba kukataliwa ombi lao la kuhairishiwa mechi na kagera sugar, akaenda mwali na kusema simba na yanga bila wao TFF haipo. Huyu mtu aliuza mechi ya fainali ya Stella na Simba baada ya kuona atatakiwa kutoa KIA kwa timu nzima, leo hii anajidai anamchungu na kuipenda club na sisi mashabiki tunamshadadia, hii sio sawa. Soka la bongo haliwezi kukuzwa na simba na yanga pekee, Dewji alipaswa na anapaswa kupuuzwa, soka letu linahitaji kuangaliwa kwa mapana yake...tutabakia na heading za kujipa matumaini but hamna kitu tunaangamia, toka enzi ya mwinyi tulikua kichwa cha mwenda wazimui na tutabaki kuwa hivyo mapaka pale tukakapo amua club haziwexi songa mbele kwa kutegemea friends of simba, Dewji, Gulamali (R.I.P), bakhresa, manji na wengineo. Soka inatakiwa kufikiriwa beyond that, tatizo letu tunaruhusu club zitawaliwe na wanachama ambao hawana maono ya wapi wanataka kwenda na ndo maana simba kumfunga yanga au yanga kumfunga simba ni Big deal, hatutafika hata kidogo, soka ni biashara na asiyejua aangalie mataifa ya watu, tutaishia kusema brain washed but the truth is there