Live Updates: SIMBA Sports Club vs TP Mazembe

unajua mechi ya AFC na Mtibwa ilipata kiasi gani kama walifikisha 200,000 nitashangaa...angalia mechi ya AFC na Simba walipata mil ngapi kama ni chini ya TZS 20,000,000 nitashangaa...hicho ndicho alicho kuwa anaimanisha Dewji..
 
Hivi hiyo Nguvu kubwa iliyowekwa ktk mechi moja tu dhidi ya TP Mazembe tena yenye ahadi za mamilioni ya pesa kwanini wasiwekeze kwenye kuiandaa timu????

Watanzania ni watu wa kupenda sana shortcut. Na kamwe hatutafanikiwa kwa hiyo njia
 
Jumamosi nilituma post hapa hapa, nikasema lazima mnyama angechinjwa na Kaluyituka...........ndivyo ilivyokuwa! Tatizo ni maandalizi! Sikuwa na nia mbaya ila jinsi magazeti na 'wadau' mbalimbali wa mpira walivyoi-under rate TP Mazembe badala kuhamasisha maandalizi, hata kama Simba ilicheza vizuri, mwisho wa siku mpira ni magoli na si porojo! Kama walivyosema wengine, nami naungana nao kuwapa pole watani zetu wa jadi! Msijali, mwakani si mtatuwakilisha tena kwenye michuano ya kimataifa! Anzeni maandalizi sasa, maana mnaweza kupangiwa tena mabingwa watetezi!
 
Hawa maembeee waliharibu kabisa wikiendi yangu....
Invizibo hebu watwange ban hawa wanaoendelea kuiharibu....
 
Lol............
 

Attachments

  • 200515_215270141821424_100000153207127_1005878_2719420_n.jpg
    15.2 KB · Views: 68
Huu sio uzalendo aisee....

Ni kweli si uzalendo...........hivi ni vijimambo tu vya utani wa jadi babu...........Usichukulie serious kiviiiile

Kwani TPM si kampakata Simba jana?
 
Ni kweli si uzalendo...........hivi ni vijimambo tu vya utani wa jadi babu...........Usichukulie serious kiviiiile

Kwani TPM si kampakata Simba jana?

Infakti naandaa muswada wa kuifungia ile pub....!
 
Ila na majina ya timu jamani yanatisha, mtu kabla ya kuingia uwanjani unahisi umeshafungwa. we timu inaitwa TOUT POUISANT MAZEMBE ENGLEBERT utatoka kweli?
 
lakini jamani si michezo tu sisi Wabongo tumezigi majigambo na maneno mengiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii vitendo 0.5% halafu mwisho wa siku tunatafuta mchawi au mamluki.
 
Hivi hiyo Nguvu kubwa iliyowekwa ktk mechi moja tu dhidi ya TP Mazembe tena yenye ahadi za mamilioni ya pesa kwanini wasiwekeze kwenye kuiandaa timu????

Watanzania ni watu wa kupenda sana shortcut. Na kamwe hatutafanikiwa kwa hiyo njia
Si kwamba Simba hatukujiandaa, tulijiandaa kadiri ya uwezo wetu na kwa aina ya timu na wachezaji tuliokuwa nao. Tunajua kuwa ni kazi ngumu kuitoa mashindanoni timu kama ile, lakini si vibaya kujaribu kama tulivyojaribu, hizi porojo za akina nanihii ni mambo yanayotawala vijiweni na kwa vile mpira wetu unaendeshwa kutokea vijiweni, porojo ni kitu cha kawaida sana.

Kwa hiyo ukiangalia hata wale anti-Simba wanavyotoa comments zao humu, ni muendelezo tu wa porojo zilizojaa katika mfumo wa uendeshaji wa timu zao. Mazembe wametusaidia kujijua tulipo na namna gani tutoke hapo na kusonga mbele, kwa watani wamewasaidia kujisahau na kuendeleza porojo, shangaa jinsi walivyonunua jezi ya mazembe kuliko hata wanavyonunua bidhaa za club yao,hiyo yote ni porojo tu kwa vile wangeweza kuishangilia Mazembe hata kwa kuvaa jezi yao na kuinunua kwa wingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…