Simba hii haizuiliki, ndivyo waweza kusema.. Na hii ni baada ya leo kuendelea na utaratibu aliojiwekea wa kugawa dozi kwa kila anayekutana nae. Leo ilikua ni zamu ya wakata miwa wa Kagera, na hii ni baada ya kuwatafuna kisawasawa.
Hadi refa anapuliza kipyenga cha kumaliza mpira.. Simba imeibuka mshindi kwa kuwafunga wakata miwa wa Kagera goli mbili kavu. Wafungaji walikua Shiza Kichuya Mabao na Muzamir Yasin.
20.10.2016 itakua ni zamu ya Mbao FC kupimiwa dozi yao katika uwanja wa Kirumba jijini Mwanza.
SIMBA SPORTS CLUB.. NGUVU MOJA