Live Updates: Vodacom Premier League, Lipuli FC Vs Yanga SC uwanja wa Samora Iringa

Live Updates: Vodacom Premier League, Lipuli FC Vs Yanga SC uwanja wa Samora Iringa

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara (VPL), kuanza kutimua vumbi leo kwa viwanja tofauti.

Mabingwa watetezi ya Yanga SC kuanza ugenini katika dimba la Samora mkoani Iringa, Azam FC watakuwa Chamazi Complex wakipimana ubavu na Ndanda SC huku Singida United wakiwaalika Mwadui FC uwanja wa Namfua mkoani Singida. Ambapo mchezo ulikuwa wa mapema kwa siku ya leo umekwisha, Singida United 3-2 Mwadui FC.

Kaa nasi kukuletea yatakayojiri uwanja wa Samora mkoani Iringa, sambamba na viwanja tofauti.

Vikosi vya timu zote zimetoshana nguvu kati ya Lipuli FC dhidi ya Yanga SC tukianza na wenyeji;
b94e71c229f5bc90fd0d67569323e4f8.jpg
Na upande wa wageni Yanga SC;
ceab41d5f481e4f5a43adbb02f161adb.jpg


Timu zote zimeingia uwanjani kupasha misuli moto, ili kujiweka tayari kwa mtanange.

Naam mpira ameanza Lipuli FC dhidi ya Yanga SC 0-0


Goooooooooaal, 18 ' Papy Tshishimbi anaandika bao la kwanza upande wa Yanga SC

Lipuli FC 0-1 Yanga SC

45' za kipindi cha kwanza za mchezo zimemalizika hapa uwanja wa Samora Iringa.

Wenyeji wakiwa nyuma ya bao moja dhidi ya Yanga SC

Mpira umeanza kipindi cha pili, na hakuna mabadiliko kwa wachezaji pande zote

46' Lipuli FC 0-1 Yanga SC

Go goooal 56 ' Butswita anaipatia goli la pili Yanga SC

Lipuli FC 0-2 Yanga SC

90' Naam mpira umekwishaaaaaaaaaaaaa Yanga wameibuka na ushindi wa goli mbili bila majibu dhidi ya Lipuli FC.
Asanteni sana. Ghazwat
 
5' za mchezo katika uwanja wa Samora Mjini Iringa

Lipuli FC 0-0 Yanga SC
 
Gadiel anapiga gooo laaaa, golikipa anadaka bila wasiwasi wowote.
 
15 ' Lipuli FC 0-0 Yanga SC
 
Wakuu Kwa Mwenye Kuujua Huu Uwanja vipi sio Mdogo Huu uwanja?? Manake Naona mipira inapigwa goli moja mpaka inaanguka goli la upande Wa pili.!!!
 
Golikipa Rostand yuko chini mpira umesimama, matibabu yanaendelea hapa uwanjani
 
Goooooooooaal, Papi Kabamba anaandika bao la kwanza mpira uliochezwa vibaya na golikipa baada Emmanuel Martin kupiga kichwa mpira wa kona na kuhesabu goli la kwanza upande wa Yanga

Lipuli FC 0-1 Yanga SC
 
Back
Top Bottom