Live Updates za Chengdu Auto Show 2024 (30 August - 8 September)

Live Updates za Chengdu Auto Show 2024 (30 August - 8 September)

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Wadau na wapenzi wa magari.

Kuna hii show inaitwa Chengdu Auto Show au juna jingine Chengdu International Automobile Exhibition inayochukua siku 10 kila mwaka katika mji wa Chengdu, China.

Kama ilivyo Beijing Auto Show ya mwezi wa nne na tano, tutegemee makampuni mbalimbali ya magari kutoka China na nchi nyingine yakitambiana ubabe katika kutambulisha magari mapya, concepts, technology mpya na pia makampuni mapya ya magari kuibuka.

Tugemee more hybrids na more EV kutoka China.
 
Avatr 07

Kampuni kutoka China, Avatr wameshatambulisha SUV yao ya Avatr 07, wanayosema itakua kati aya $35,000 hadi $50,000 kwa bei.

pixelcut-export-3-1.png

Avatr 07 itakuja na model kuu mbili, moja ni full EV na nyingine ni range-extendend EV.
Avatr_07_revealed_in_China_CNC-4.jpg

Kwa full EV nayo utachagua kati ya RWD ambayo itakua na motor moja au AWD itakayokuja na motor mbili, na zitakua na range ya kilometa 650 kwa RWD na 610 kwa AWD.
pixelcut-export-2-5.png

Option ya pili ndio range extended EV.
Kwa kujikumbusha, REEV ni gari la umeme ambalo pia lina engine, mara nyingi inakua engine ndogo mfano cc 1500 au hadi cc900.
arenaev_002.jpg

Lakini, tofauti na hybrid ambayo engine na battery zote zinatumika kuendesha magurudumu, hizi range extender kidogo zipo tofauti.
Hiyo engine haijaunganishwa na wala haifanyi kazi yoyote kuendesha gari, ila yenyewe inafanya kazi kama genereta. Kwamba, battery likiisha chaji, yenyewe itawaka na kuichaji battery ikijaa au ikifika kiwango flani iyo engine inazima. Nadhani kidogo umenipata.
Tuendelee na REEV..
Hii itakuja na 1.5L engine na utachagua tena RWD au AWD, na ina range hadi ya 1200+
arenaev_003.jpg

Kuhusu design, hawa jamaa wanajua sana. Kuna watu jukwaani mlilamika kwamba hamtanunua Avatr 12 tulioidiscuss wiki iliopita kwasababu taa zake ndogo sana. Na hii pia, taa ova mstari.
pixelcut-export-1-1.png

Kuna double-layer LED daytime running lights ambayo ni style yao ya kujitambulisha pale mbele kama kawaida.

Ndani kuna cockpit yenye four-screen setup (ndio walivyosema kwenye presentation), moja ikiwa ni inch 35 4K, na mbili inch 6 ni side mirrors screen (ikumbukwe hatuna vioo nje ni camera), na moja ni Huawei intelligent control screen.
Untitled-1.png

Kuhusu technology, wao wanatumia Taihang Intelligent Control Chasis ni mpya so hatuna pa kuifananisha napo, wana dual wishbone independent suspension, smart air spring, nk.
avatr 07 huawei.jpg

Pia Huawei wamewapa baadhi ya technology kwenye self driving, kuna LiDAR, parking assist, na collision avoidance system.
 
Kumbe china wanatumia upande wa kushoto kama marekani .
Mwezi July nilikutana na BYD CROSSOVER COMPACT imepaki pale kamata ni IT ya Congo lkn usukani upo kushoto
 
Chery Fulwin E05
Cherry wamezindua Chery Fulwin E05 ambayo itakua sedan exclusive kwa China tu, sisi tukiitaka itabidi tuwaagize Silent Ocean. Itakua na option ya EV na REEV, na itauzwa $22,000 tu.
Screenshot-2024-08-31-102630_1725125235268-scaled.jpeg

Hii ni Sedan ila unaweza sema ni fastback, inamuonekano mzuri kwa mtazamo wangu. Mfano, kwa mbele ina taa zenye muonekano wa kipekee, kwa juu kuna LiDAR kwenye roof, ambayo itasaidia kwenye driving assistance.
image-154.png

Kwa ndani wamejitahidi iwe simple, nadhani kupunguza gharama, kuna infotainment screen katikati na cluster screen ya dereva na huku vents za AC wamezificha.
image-155.png

Kwa ndani huko huko, kuna friji na modes mbalimbali za kuchagua mfano relaxing modes na sleep modes.
Screenshot-2024-08-31-101428.png

Kwa sasa, taarifa za battery, motor na engine hawajaziweka wazi bado
 
Changan CS75 Plus
Changan Mobile wamezindua CS75 plus ambayo tunaweza sema ni second gen ya CS series SUV.

1400x0_1_q95_autohomecar__Chtk2WbRY16AK6zcABaCcihLyrY241.jpg

Hii ni SUV kubwa, kwa mbele ikiwa na grille zimejipanga kwenda chini kwa V-shapped na kuna mkanda wa LED daytime running lights ambao umepita juu ya izo grille mwanzo hadi mwisho.
1400x0_1_q95_autohomecar__ChxkPWbDB46AIH4wAEzcuYxAU4M252.jpg

Kwa ndani kuna screen tatu ambazo zimeteka dashboard nzima. Upande wa abiria kuna infotainment screen, katikati kuna Screen na kwa dereva kuna LCD instrument panel.

Gear-leaver ipo kwenye steering wheel, kwahiyo hapa chini pako empty wameweka wireless charge na cupholders tu.

Pia kuna options ya massage seats, heating and ventilation seats ambazo ni zero gravity (unaweza kulala).
1400x0_1_q95_autohomecar__ChxkPmbDBPyAbhVuACEI3lFixnc342.jpg

Kwa kuanza, gari itakua ICE tu, ikiwa na engine ya 1.5T na 8 gear automatic transmissions.

1400x0_1_q95_autohomecar__ChxkPWbDBFaAOPBCAB4P-RPtw_4331.jpg

Gari itakuja na level 2 driving assistance, ikiwa na lane keeping assistance, parking assist nk.

Hii model unaweza kua haujaisikia, lakini ni moja ya best selling SUV huko China. Mfano mwaka jana zaidi ya gari 250,000 ziliuzwa na takwimu zinasema hadi sasa ni namba 4 best selling SUV ya 2024.
 
Changan CS75 Plus
Changan Mobile wamezindua CS75 plus ambayo tunaweza sema ni second gen ya CS series SUV.

View attachment 3084224
Hii ni SUV kubwa, kwa mbele ikiwa na grille zimejipanga kwenda chini kwa V-shapped na kuna mkanda wa LED daytime running lights ambao umepita juu ya izo grille mwanzo hadi mwisho.
View attachment 3084228
Kwa ndani kuna screen tatu ambazo zimeteka dashboard nzima. Upande wa abiria kuna infotainment screen, katikati kuna Screen na kwa dereva kuna LCD instrument panel.

Gear-leaver ipo kwenye steering wheel, kwahiyo hapa chini pako empty wameweka wireless charge na cupholders tu.

Pia kuna options ya massage seats, heating and ventilation seats ambazo ni zero gravity (unaweza kulala).
View attachment 3084227
Kwa kuanza, gari itakua ICE tu, ikiwa na engine ya 1.5T na 8 gear automatic transmissions.

View attachment 3084229
Gari itakuja na level 2 driving assistance, ikiwa na lane keeping assistance, parking assist nk.

Hii model unaweza kua haujaisikia, lakini ni moja ya best selling SUV huko China. Mfano mwaka jana zaidi ya gari 250,000 ziliuzwa na takwimu zinasema hadi sasa ni namba 4 best selling SUV ya 2024.
hatari sana
 
BYD Xia MPV

BYD wamezindua Multi-purpose Vehicle inayoitwa Xia, ambayo ina urefu wa mita 5, seat 7, kwa kuanzia $43,000/=
images (2).jpeg

Hii ni Plugin Hybrid itayotoka mwakani 2025 kwahiyo wameibania kuisemea vitu vingi.
byd-xia-2024.jpg

Ata picha za ndani hawajatoa kabisa.
images (3).jpeg

Kwahiyo tusubiri tu mwakani.
 
Volkswagen Passat Pro
VW wamezindua Passat Pro!
2025-volkswagen-passat-pro-launch-price-sedan-2-1068x601.jpg

Hii ni kwaajili ya wateja wa China, inakuja na 2.0L 4-cylinder engine, inayotoa 217 hp na ina 7-speed automatic transmission.

2025-volkswagen-passat-pro-launch-price-sedan-8-1068x601.jpg
2025-volkswagen-passat-pro-launch-price-sedan-6-1068x738.jpg

Kwa ndani ina screen tatu (moja 15 inch infotainment touchscreen, pili 10 inch instrumental cluster na ya tatu 11 inch kwaajili ya abiria), na augmented reality HUD.

2025-volkswagen-passat-pro-launch-price-sedan-4-1068x738.jpg

Ndani pia kuna spika 16 za Harman Kardon audio system, na seat unaweza adjust electrically na zina vents, heating, na massaging function.
2025-volkswagen-passat-pro-launch-price-sedan-5-1068x738.jpg

Bei bado hawajasema kwa sasa.
 
Volkswagen Passat Pro
VW wamezindua Passat Pro!
View attachment 3084317
Hii ni kwaajili ya wateja wa China, inakuja na 2.0L 4-cylinder engine, inayotoa 217 hp na ina 7-speed automatic transmission.

View attachment 3084318View attachment 3084319

Kwa ndani ina screen tatu (moja 15 inch infotainment touchscreen, pili 10 inch instrumental cluster na ya tatu 11 inch kwaajili ya abiria), na augmented reality HUD.

View attachment 3084320
Ndani pia kuna spika 16 za Harman Kardon audio system, na seat unaweza adjust electrically na zina vents, heating, na massaging function.
View attachment 3084321

Bei bado hawajasema kwa sasa.
Hii mutuka si haba. Ina ground clearance mzuri...
 
Rox 01
Rox Automobile wazindua All terrain REEV SUV iitwayo Rox 01.
66d55d49a3108f29a8b62fad.png

Ina engine ya 1.5L ambayo itatumika kama extender (generator) na battery la 58.4 kWh battery.

Kwa full charge, battery litakupeleka kilometa 306, na wakati tank la lita 70 ukijaza wese + battery utaweza kwenda jumla ya kilometa 1300+!

post26089_8.jpg

Pia, kuna 2.2 kW external power V2L (vehicle to load) system unaweza kuwasha vitu kama jagi, coffee maker, cookers hizi, friji dogo etc.
post26089_1.jpg

Hii ni gari ni kwaajili ya watu wa camping na road trip, kwani ina seat arrangement ya 2+2+3 au 2+2+2 kutegemeana na unavyoweka vitu.
post26089_3.jpg
 
BYD Seal 06 GT
Mchina anazidi kufanya mabalaa, sasa katuletea hatchback Seal 06 GT kwa $22,000/= tu!
pixelcut-export-1-9.jpeg

Hii gari itakua based na concept walioitangaza mwezi wa nne kwenye Shanghai Auto Show (Ocean M), ila hii ni more sportier na iko na advanced tech.
Weixin-Image_20240830230430.jpg

Kwa ndani, ina screen mbili moja inch 15 na instrumental cluster ya inch 10, pia virtually kuna HUD yenye 12 inch!

Weixin-Image_20240830225001.jpg

Itakuja na single au dual motors, wakati hii dual motors itakupa 0-100kph kwa sekunde 5 tu.
Weixin-Image_20240830230429.jpg

Battery utachagua kati ya 60 kWh itakayokupa 505km au 72 kWh itayokupa 605km.
1758afbdb3b79d03566bd50f72555c4.jpg

Hii bei ni sawa na Subaru Imprezza ikiwa 0 km. Kwa mwenendo huu, bado kujitoa muhanga tu.
 
BYD Seal 06 GT
Mchina anazidi kufanya mabalaa, sasa katuletea hatchback Seal 06 GT kwa $22,000/= tu!
View attachment 3085242
Hii gari itakua based na concept walioitangaza mwezi wa nne kwenye Shanghai Auto Show (Ocean M), ila hii ni more sportier na iko na advanced tech.
View attachment 3085244
Kwa ndani, ina screen mbili moja inch 15 na instrumental cluster ya inch 10, pia virtually kuna HUD yenye 12 inch!

View attachment 3085247
Itakuja na single au dual motors, wakati hii dual motors itakupa 0-100kph kwa sekunde 5 tu.
View attachment 3085248
Battery utachagua kati ya 60 kWh itakayokupa 505km au 72 kWh itayokupa 605km.
View attachment 3085249
Hii bei ni sawa na Subaru Imprezza ikiwa 0 km. Kwa mwenendo huu, bado kujitoa muhanga tu.
Humo ndani mashallah, imenakishiwa vyema...
 
Nio EP9 (Electrical Performance 9)

Nio wameintroduce (tena) coùpe ila ni track only, sio legal kuendesha barabara zetu hizi.
Nio_EP9 (1).jpg

Hii ni track day sport car, ikiwa na two seat na very low ground clearance, na milango inayofunguka juu.
66d6aa91a3108f29a8b64555.jpeg

Hii gari jmetengenezwa na Nio wakishirikiana na Department ya Racing ya Nio Formula E (hii ni kama formula 1 racing Ila ya magari ya umeme). Ni kagari kaajabu kidogo, kana motor 4 kila tyre, kana gearbox 4 kila tyre, kanaenda Kilometa 427 full charge na kanatoa total of 1300hp.

NIO_EP9_rear_(cropped).jpg

Hiki kidude kwa nyuma kina spoilers ambazo unaweza adjust katika settings mbalimbali na inaweza tengeza downwards force hadi ya 2500 kg ikiwa katika 240kph, almost sawa na F1 car, so possibly kukata kota at 3.0Gs!

NIO_EP9,_Oslo_(2024).jpg

Bei yake ni almost Tsh Bil 8.9 okay hii ni track day only car. So wananunua racing teams kubwa.
 
Dongfeng Aeolus L7 EV
Wachina wametoa Dongfeng Aeolus L7 EV SUV itayoanza kwa $17,000/= tu!
Shanhai-L6_1724618767541-scaled.jpeg

Itakuja na motor moja yenye 160kW, na battery la 310 km litakalofikisha kilometa 518 likijaa, na unaweza kuchaji kutoka 30 hadi 80 kwa dakika 28 tu!

3.jpg

Kwa ndani, wajamaa wanakuja na black and orange, na kuna 10 inch screen ya dereva na katikati kuna 14 inch screen, na steering ya kibabe yenye shepu ya D.
image-4.png

Wachina wanaendelea kutoa vitu.
 
Back
Top Bottom