Avatr 07
Kampuni kutoka China, Avatr wameshatambulisha SUV yao ya Avatr 07, wanayosema itakua kati aya $35,000 hadi $50,000 kwa bei.
Avatr 07 itakuja na model kuu mbili, moja ni full EV na nyingine ni range-extendend EV.
Kwa full EV nayo utachagua kati ya RWD ambayo itakua na motor moja au AWD itakayokuja na motor mbili, na zitakua na range ya kilometa 650 kwa RWD na 610 kwa AWD.
Option ya pili ndio range extended EV.
Kwa kujikumbusha, REEV ni gari la umeme ambalo pia lina engine, mara nyingi inakua engine ndogo mfano cc 1500 au hadi cc900.
Lakini, tofauti na hybrid ambayo engine na battery zote zinatumika kuendesha magurudumu, hizi range extender kidogo zipo tofauti.
Hiyo engine haijaunganishwa na wala haifanyi kazi yoyote kuendesha gari, ila yenyewe inafanya kazi kama genereta. Kwamba, battery likiisha chaji, yenyewe itawaka na kuichaji battery ikijaa au ikifika kiwango flani iyo engine inazima. Nadhani kidogo umenipata.
Tuendelee na REEV..
Hii itakuja na 1.5L engine na utachagua tena RWD au AWD, na ina range hadi ya 1200+
Kuhusu design, hawa jamaa wanajua sana. Kuna watu jukwaani mlilamika kwamba hamtanunua Avatr 12 tulioidiscuss wiki iliopita kwasababu taa zake ndogo sana. Na hii pia, taa ova mstari.
Kuna double-layer LED daytime running lights ambayo ni style yao ya kujitambulisha pale mbele kama kawaida.
Ndani kuna cockpit yenye four-screen setup (ndio walivyosema kwenye presentation), moja ikiwa ni inch 35 4K, na mbili inch 6 ni side mirrors screen (ikumbukwe hatuna vioo nje ni camera), na moja ni Huawei intelligent control screen.
Kuhusu technology, wao wanatumia Taihang Intelligent Control Chasis ni mpya so hatuna pa kuifananisha napo, wana dual wishbone independent suspension, smart air spring, nk.
Pia Huawei wamewapa baadhi ya technology kwenye self driving, kuna LiDAR, parking assist, na collision avoidance system.