azamtv
Utaratibu wa jinsi ya kulipia na kupata kifurushi cha Azam Sports na chaneli zake kama Azam Sports HD pamoja na kubadili vifurushi kama unahitaji kifurushi kingine. Tunatoa tena maelekezo hapa, tafadhali yafuatilie kwa makini na utafanikiwa tu. Hii ni kwa wateja wa Tanzania tu.
Vifurushi vikuu vipo vinne (4) na Vya nyongeza ni viwili (2).
Vifurushi Vikuu ni; Azam Pure 12,000, Azam Plus 20,000, Azam Play 25,000 na Kihindi Pekee 16,000.
Vya Nyongeza ni; Azam Sports 15,000 na Kihindi cha nyongeza ni 6,000
Ili kupata Azam Sports HD, ni lazima uwe na kifurushi cha nyongeza cha Azam Sports cha shilingi 15,000. Kwa mfano kama una Azam Pure sasa hivi, jumla unatakiwa kulipia 27,000 (12,000 + 15,000 = 27,000 jumla). Ukiwa na Azam Plus (20,000 + 15,000 = 35,000 jumla). Ukiwa na Azam Play (25,000 + 15,000 = 40,000 jumla).
Ili kukipata kifurushi cha nyongeza cha Azam Sports, fuata utaratibu huu:
Kama hujafungiwa huduma na una kifurushi kikuu tayari;
1. Fanya malipo ya shilingi 15,000 na kisha piga namba *150*50*5#
2. Chagua namba 3, Sajili Huduma Mpya.
3. Ingiza namba ya smartcard.
4. Chagua namba 6, Azam Sports Add on 15,000
5. Baada ya hapo subiri dakika 5-20 utapata chaneli.
Kama umefungiwa kifurushi chako na unataka Azam Sports HD pia;
1. KABLA ya kufanya malipo, piga namba *150*50*5# kwanza.
2. Chagua namba 3, Sajili Huduma Mpya.
3. Ingiza namba ya smartcard.
4. Chagua namba 6, Azam Sports Add on 15,000
5. fanya malipo ya jumla ya kifurushi chako kikuu na cha Azam Sports HD pia. Kwa mfano lipia jumla ya shilingi 27,000 kama ulikuwa una kifurushi kilichofungiwa cha Azam Pure na unataka cha Azam Sports pia. Yaani 12,000 + 15,000 = 27,000. Vile vile fanya kujumlisha ulichonacho sasa kama ni tofauti na Azam Pure.
6. Baada ya hapo subiri dakika 5-20 utapata chaneli.
Kama umefungiwa na unataka kubadili kifurushi cha sasa na kuongeza cha Azam Sports pia;
1. KABLA ya kufanya malipo, piga namba *150*50*5# kwanza.
2. Chagua namba 2, Badilisha Kifurushi
3. Ingiza namba ya smartcard
4. Chagua kifurushi
5. piga namba *150*50*5# tena
6. Chagua namba 3. Sajili Huduma Mpya
7. Ingiza namba ya smartcard
8. Chagua namba 6 Azam Sports Add on 15,000
9. Fanya malipo ya jumla ya kifurushi chako kikuu na cha Azam Sports HD pia. Kwa mfano lipia jumla ya shilingi 27,000 kama ulikuwa una kifurushi kilichofungiwa cha Azam Pure na unataka cha Azam Sports pia. Yaani 12,000 + 15,000 = 27,000. Vile vile fanya kujumlisha ulichonacho sasa kama ni tofauti na Azam Pure
10. Baada ya hapo subiri dakika 5-20 utapata chaneli
Kama ulishalipia lakini unataka kubadili kifurushi kikuu, fanya hivi;
1. Unaruhusiwa kubadili kifurushi kikuu ndani ya siku mbili baada ya malipo kwa kuongezea tu malipo yako. Kama zimepita siku mbili, LAZIMA ulipie upya kifurushi hicho.
2. Kisha Piga *150*50*5#
3. Chagua namba 2, Badilisha Kifurushi
4. Ingiza namba ya smartcard
5. Chagua kifurushi
6. Baada ya hapo subiri dakika 5-20 utapata chaneli.