Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Nahodha wa zamani wa United, Gary Neville wakati mchezo ukiendelea alinukuliwa akisema: “Nimeiangalia United kwa miaka 42, sijawahi kuona timu mbovu kama hii ya sasa.”
Katika mchezo huo ilipofika dakika ya 7, mashabiki wa #ManUnited na Liverpool waliungana na kusimama kwa dakika moja kutuma salamu za rambirambi kwa Cristiano #Ronaldo wa Man United aliyefiwa na mtoto wake wa kiume wakati mpenzi wake akijifungua.
Kwa matokeo hayo sasa Liverpool anashika usukani wa Premier League akiwa na pointi 76 katika michezo 32, Man City ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 74 ikiwa na michezo 31.
Picha: Premier League