Wale wenzangu wa kule Marseyside,leo ndio kile kipute na watani wetu Everton kinapigwa.Katika mechi zetu mbili za mwisho kukutana na hawa jamaa tulitoka droo zote ikiwemo ile ya msimu uliopita ambayo ilamalizika kwa sare ya 2-2 na ile ya mzunguko wa kwanza ya sare ya 3-3.
Sina mashaka na kikosi changu najua tutafanikisha hili kwa maana huyu Tottenham anayetunyemelea leo anakipiga na Man City.
Kwa mtazamo wangu ningemuomba kocha amuanzishe Victor Moses badala ya Cissoko na kwa kipindi kirefu sijamuona beki wetu wa kulia Wisdom,nadhani angekuwa mbadala wa Johnson ambaye ni majeruhi.
Yote kwa yote nasema We will never walk alone mpaka kieleweke..Ushindi leo lazima,wenzangu wala msivunjike moyo,kama utaenda kubet leo basi nakwambia Liverpool ipe ushindi na kama ukiliwa njoo uchukue hela yako kwangu ila matumaini ya kuliwa yaweke pembeni labda Arsenal akuangushe.
"Nlikuwepo":bolt: