Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Leo hata siwapongezi kwa ushindi, bali natupa wote wapenda mpira, wapenda utu na wapenda amani, pole kwa uhuni uliomkuta Luis Diaz na tuombe hao wapumbavu waliowateka wazazi wake wakamatwe na waadhibiwe vilivyo.
Dunia ina matukio usiyotegemea kabisa, dogo anatoka kwenye familia maskini katumia kipaji vyema na kuwainua familia yake na sasa haya yamemkuta.
Colombia wana uhuni huu sana wa ransom yaaani kule ni jambo la kawaida sana.

Tunashukuru kwa kujali ndugu.

YNWA
 
Bobby hivi wewe huwa hupendi kucheka?
Nimekutag kule utd pita kule ucheke kidogo bwana.
Uzi ukiugusa tu unachekesha hatari πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜πŸ˜
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ Kucheka unaongeza siku za kuishi so they say.. Aaa natulia humu humu mpaka kuache kummidisa dogo Nunez wa watu sijui alikufanya aje... Kwa hio ikija ofa ya Salah na Nunez kutoka Uarabuni tuchukue ya Nunez na Salah ibakieπŸ™ƒπŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚


YNWA
 
Anakosa mengi sana tu , he thrives under chaotic situations na so far anazidi kujiamini na kua clinical amebakisha pandogo sana akuzime mdomo wako kabisa watch out buddy... Nunez alikotoka alikua anakipiga kwa mafanikio makubwa sole striker lakini huku mara apangwe LW mara CS nk lakini kote wala hana malalamiko.. Kilichobaki kwake sasa ni Domy acheze behind the front line na sio kuleee anakocheza sasa na magoli yatakua mengi sana kwa kua Domy atamtupia pasi murwa sana

Hata Jota nae anarejea taratibu taratibu tu tutaelewana.. Uzuri pale mbele kwa sasa pamesheheni kazi kazi Diaz, Nunez, Salah, Gapko, Jota wote hao wanauwezo wa kubadili matokeo muda wowote.

YNWA
 
Mpunga labda tuchukue Summer huko iwapo tu Salah ataforce kuondoka.

Lakini kama hajaforce asiondoke kwasababu sisi mashabiki ndiyo raha yetu yeye kufuga Migoli mengi cuz hata akiuzwa hizo hela hatutofaidika nazo sisi mashabiki bali zitaenda Mfukoni kwa Mzee Henry.
 
Au waje wafungwe Ukonga ili wakabebe Zege kwenye ujenzi wa Mwendo kasi pale Banana mpaka Gomz.
Jela za Ulaya upuuzi mtupu
Wanafunga jitu linanenepeana,wanalala pazuri kama hotelini..chakula kizuri.


Hawa waletwe wakafanye usafi barabara ya mwendokasi Magomeni-Mbagala.

Wakimaliza tunawatupia mashamba ya chai Ushirika Tukuyu huko wakachume chai.
 
Hata akilazimisha kuondoka tusikubali[emoji23][emoji23][emoji23]

Kwa kweli Mimi sioni faida nitakayopata endapo Salah ataondoka.
 
Salah hana mpinzani kwenye 1st Eleven
Hao wengine watagombania..
Ila kwa kweli pale mbele ni burudani.


Sawa Bobby..nasubiri wewe na mdogo wako mfunge bakuli langu[emoji23]
 
Twende bwana Man Utd ukaongeze siku za kuishi.


Wewe umeshikilia LFC tu pekeyake,kwani umekuwa mfungwa?[emoji38]
 
Raha jipe mwenyewe maisha ndio haya haya... Unakata mti unapanda mti.

YNWA
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kata mti panda mti
Reforestation[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Na kalivyo kahandsome halafu kanajua mpira..nimeishia kukamezea mate.
 
Dah jamani[emoji3064]
Wamuache Diaz wetu.


Ila Mungu yupo,
Wabaya watajulikana.
 
πŸ˜‚ πŸ˜‚ Ingekua mashabiki tuna chetu mfukoni ingekua raha sana... Nahisi kama vile upande wa Salah hii dili wanaitaka kwa sababu ni ngumu sana kuelewa kwa nini siku za mwisho dirisha la summer waarabu walizidisha sana spidi kumhitaji dogo.. Klopp atakua kazini na ma scouts kusaka mbadala wake endapo dogo atafosi kuodoka.

Kwa huuu moto alionao sasa amekua complete player design fulani kama Bobby anafunga na uchoyo amepunguza.. Liverpool wakomae hakuna kuuza mpaka June 2024 hukoo...

YNWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…