Ikiwezekana hata january aende tu kwenye timu kubwa ambayo atakuwa na uhakika wa kunyanyua kombe, ni aibu kwa mtu kama yeye aliyecheza kwa kiwango cha juu kwa muda mrefu kustaafu bila league title hata moja. Kwa Liver hata akae miaka mingine mitano hawezi kubeba. Kama anataka mafanikio ya Fasta aende La liga au BL (Ingawa La Liga na yenyewe kwa sasa haieleweki eleweki) , ila kama nia yake ni pesa nadhani ataenda zake US. Au mwisho wa siku akubali yaishe tu astaafu zake kama Jamie. Kama atabaki EPL mtu wa kwanza kumuulizia SG atakuwa ni Mourinho, jamaa anaoneka huwa anamkubali sana SG. Ila asilogwe kuhamia timu nyingine ya EPL.