Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Tatizo City anazengea zengea behind, akishinda kiporo chake ni point 2

Gundu letu tena tukiongozaga ligi tuu game inayofuata inakua ni "trick" game , kama hapa ni Newcastle

Hii ligi mwanga utaonekana vizuri march
 
title race

Arsenal na Liverpool ni wafukuza upepo tu !

City anafunga busta zote round ya pili, hapa ndo anapokuwa serious, pia ana depth,,,,

Msisahau Kdb yupo anapasha huko bado kidogo mtamuona kwa ground !!!!!!
Wachache wenye akili watakuelewa
 
title race

Arsenal na Liverpool ni wafukuza upepo tu !

City anafunga busta zote round ya pili, hapa ndo anapokuwa serious, pia ana depth,,,,

Msisahau Kdb yupo anapasha huko bado kidogo mtamuona kwa ground !!!!!!
Pasha tu
Na sisi tupo tunapasha
Thiago yupo anapasha pia.

Na kileleni tupo.
 

Offside inaanza kuhesabiwa pale mchezaji au wachezaji wa timu pinzani anapozidi/wanapozidi wachezaji wa ndani wa timu pinzani. Wachezaji wa ndani ni wale wasiotumia mikono kuucheza mpira uwapo ndani ya uwanja yaani kuanzia beki namba 2,3,4,5 viungo 6,8, 10 mawinga wawili 7&11 strika 9 (2,3,4,5,6,7,8,9,10 na 11). Hii ndio iliyozoeleka kwa wengi.

Sasa offside ina vipengele vyake ambavyo inategemea na tafsiri ya refa na sasa hivi VAR ndio kabisaaa huelewi consistency ya offside. Ila kwa sheria za sasa offside ni ukizidi sehemu yoyote ya kiungo cha mwili kwenye eneo la mpinzani.

Sasa hii hapa ndio inachanganya wengi, na inategemea busara na IQ za mwamuzi. Mchezaji wa timu pinzani akizidi hata mwili wote kisha mchezaji wa timu yake akapiga mpira na mchezaji yule akaingilia (interfere) lile lile tukio mathalani kuukimbilia mpira kuukwepa mpira au mpira kuugusa na kusababisha kumpoteza golikipa kwa namna moja au nyingine hii inakuwa offside. Mf wa matukio haya ndio kama goli la Gakpo mechi vs Butnley.

Lakini sasa hapa inategemea na uwezo wa mwamuzi wa kutafasiri matukio hayo. Ndio maana kwa tukio hili hili ni offside mwchi nyingine sio offside.

Kuna offside nyingine hutokea ikiwa mchezaji wa timu pinzani yupo mbele ya golikipa halafu nyuma ya golikipa kuna mchezaji wa ndani. Kwa mf. Alison katika piga nikupige akawa mbele kiasi ila ndani ya box hapo halafu nyuma akawa Saka halafu nyuma ya Saka akawa TAA ikitokea mpira ukapigwa kwa Saka na akafunga hii itatafsiriwa offside pia.

Kama haujaelewa uliza.
 

Gomez ana stats nzur as LB kuliko RB (fanny thing) he is Right footer kwenye nafasi hiyo wachache wana mudu kama Lord Milner.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…