Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Ndio ndio.
Arne Slot ni aina ya kocha anayeishi na wachezaji wake kama watoto wake, hivyo hutumia njia ya mazungumzo ya upendo kuwaelewesha vijana wake.
Lakini sio kwamba player akizingua hawezi kumkoromea.

Manyanza.

Kuna kitu kinaitwa, "Dressing Room Politics", ni kitu ambacho kipo enzi na enzi lakini katika modern football, kimekuwa ni kikubwa sana.

Dressing Room, siyo tu Coaches & players, but ni the whole managament, na kwa bahati mbaya katika modern football, wachezaji ndiyo wana-hold the key, wachezaji ndiyo wana power, player-power ni kubwa sana kwasasa katika football.

Hence, unahitaji coach ambae anajua au ana uwezo wa kuishi/ku-limit influential aspect ya nguvu ya mchezaji katika dressing room. kila coach ana njia yake ya ku-demand authority kwenye dressing room, pamoja na ukubwa wake, Klopp used ile approach ya "father to son & brother to brother" tactic ili kulinda/kuepusha mental/ego problems kwenye dressing room, while mwezake Pep anatumia approach ya "I have seen it all" tactic, kwamba i made Messi, utaniambia nini? Pep approach ni same na ya Mourinho, kwamba "I have Seen it all", won CL with Porto, got CHELSEA back to LIFE with countless big trophies, utaniambia nini? hizi approaches ni tofauti na zile za kina Klopp/Carlo/Wenger etc, na zote zina hasara na faida, approach ya kina Klopp hasara yake ni kuwa eventually you get so attached na players (sentimentalism), faida yake ni kuwa players wanakuwa ready to die for you on the pitch, approach ya kina Pep hasara yake ni consistent bust-ups na wachezaji, faida yake ni kuwa players hawa-relax/kuwa katika comfort zone. BUT approaches zote zinafanya kazi kwa namna yake.

Sasa, Slot ambaye ni upcoming & bado ni very young coach, unataka atumie approach ipi? ya kina Pep? kwa CV ipi?

Then kuna tofauti kati ya kuwa Ruthless na Mkoromaji, kuwa ruthless ni kuwa hutaki players wawe comfortable na pia unafanya kile unachohisi ni sawa bila kujali feelings za mchezaji LAKINI kutoathiri his progress au urge ya kujitoa kwaajili yako uwanjani, alichofanya Slot kwa Quansah ile game ya kwanza, ni kumuonesha kuwa kama unataka kuwa katika team yake you need to work on your weaknesses, na ndiyo maana baada ya game alitenga muda wa kuongea na Quansah na kumuelekeza kwanini alimtoa na kitu gani anahitaji kutoka kwake, Manyanza, Slot kamrithi Quansah kutoka kwa Klopp (WC coach), kwenye mind ya Quansah anaamini kuwa kama aliweza kupata nafasi na kuaminiwa na Klopp basi ana uwezo wa kucheza chini ya kocha yeyote yule, hiyo ndiyo mindset ya hawa watoto wote kwenye big clubs, kama Slot angemkoromea Quansah siku ile kuwa "kwanini unapoteza duels?? kwanini unakuwa mzembe?" angepoteza dressing room siku ya kwanza tu, maana senior players wangeaza ku-question atitude ya Slot, na ni kitu dangerous, kwasababu anachofanya Slot kwasasa ni ku-earn TRUST ya senior players, ku-prove kwanza kuwa my coaching abilities can win you trophies.

Nakupa mfano mdogo sana wa "dressing room politics", unamuona Gundogan, a treble winner, certified world class player, won everything at City, EVERYTHING, he joins Barcelona, get to play katika one of the most terrible Barcelona sides in recent years, the Barcelona side was so young, ungefikiri kuwa the kids and even other senior players who havent won anything big kwenye their careers, BAR Lewa ambaye naye moja ya World Class player and senior aliyekuwepo at the club, but you know what happened? kwenye ile game dhidi ya PSG last season, Araujo alifanya mistake ambayo ili-cost his team big time, na baada ya game Gundogan akaongelea ile mistake, si kwa ubaya, bali alikuwa anatoa his 2 cents kuhusu state ya game kwa ujumla, but guess what? The whole dressing room turned on him, and guess what again? juzi kaondoka Barcelona, ni Ter Stegen tu, ambaye alimpa mkono wa kwaheri, angalia tofauti ya Gundogan na Cancelo walivyoondoka Barcelona, sasa unaona shida ya kuwa na vitoto kwenye dressing room, kina Araujo wana kipi cha kutamba mbele ya Gundogan? but shida iliyopo hapa ni kuwa Gundogan kawakuta hawa wachezaji at Barcelona, wamekuwa pamoja kwa muda mrefu sana, ndiyo maana unaona kina Lewa hawataki shida na hawa wachezaji, ni sawa na LFC, Trent/Salah/Robertson/VVD/Alli/Kostas/Gomez/Curtis wapo LFC pamoja si chini ya miaka 6-7, then ongeza cream ya kina Konate/Jota/Diaz/Nunez/Alexis/Szobo etc, na ukiachana na hawa seniors kuna kids kama kina Quansah/Harvey/Bradley etc, sasa kocha mpya unaingia hapa na kuanza kukoromea hawa watu, unatafuta shida mkuu, shida ya hatari sana. ETH kaenda Utd, pressure ya kufundisha big club got to him, akaanza kuvimbia players, na approaches za kina Pep, mpaka sasa ameshindwa kuikarabati dressing room yake, ndiyo maana anasign sana his old players au players anaowajua closely, sasa unataka iwe hivyo at LFC?

Slot akimkoromea Trent, Trent ataleta mentality zile zile za young players wote wa kwenye hizi big clubs, kwanza unanikoromea kama nani? kwa CV ipi? i have been coached by Klopp my whole life, i have won everything, i'm a scouser and worshipped by every single scouser in the City, na sasa kila siku Perez anapiga simu kwa my agent, wewe nani unanikoromea? na hapa ndiyo unakuta kwenye WhatsApp groups wanaanza kuulizana huyu kocha vipi? and if you think wachezaji wako hawa hawajam-discuss Slot kwenye group lao soon tu alivyotangazwa, then you're wrong. these players are human beings too and they gossip all the time, words ni kuwa Robertson ndiyo big gossiper (hakimpiti kitu).

So, njiq ya Slot kufanikiwa at LFC ni ku-manage dressing room dynamics, kukoromea kwa lugha nyepesi ni ku-instigate Bust-ups, na kwenye mpira mpaka zitokee bust-ups inamaana ni kitu kikubwa sana kimeenda WRONG, which sikioni at LFC.
 

Ladder 49.

Kifupi ni kuwa SINA excitement, yeyote na signing ya Chiesa, ni kuwa siwezi kucomplain kwa Club ku-grab a good opportunity ya kusign a talented player kwa cut price.

Chiesa na Melo, situations ni tofauti, Chiesa anakuja LFC akiwa na good amount of minutes kwenye his tank, huku akiwa ametoka kucheza a good amount of football, and its not a PANIC buy. because LW/RW positions zilikuwa ni least of our needs.

Mchezaji kufanikiwa katika Club mpya, haya ni matakwa ya Mungu (my personal belief), Chiesa signing can go all wrong, but ni kawaida kwenye football, shit happens, na kama ikitokea kwa Chiesa wont complain, hasa kutokana na his price, but siwezi kuwaza now kuwa atafail bali nawaza kuhusu mchango wake positive atakaotoa kwa Club.
 
Bajcetic to RB Salzburg season Loan

Nat phillips to Derby Count season Loan

Ben Doak to Middlesbrough season Loan

Marcelo Pitaluga to Livingstone Season Loan

Sijajua kwa nini Nat Philips hauzwi na the guy he is 27 yrs old. Ilikuja ofa ya 4M kutoka Trabzaspor ya Turkey ikachomolewa.
Kwa umri huu haujapata bado nafasi kwenye kikosi cha kwanza ni nadra sana kuingia kwenye timu. Nat anapokea 65k/pw 5k/pe less than Konate, while kuna kina Diaz wanapokea 55k/pw, Jones 15k/pw, Kelleher 10k/pe though are the contractual issues but they need to fix these things.
 
Man am really shocked bro why on earth are we signing GK or LW and leaving the DM empty to the extent sending Bajetic and probably Morton on loan.

Nerds sijui wana beti Manchester City bingwa ama maana this is ridiculous at the highest level

YNWA

Captain.

Juzi hapa nadhani ulimuona ndugu yako Ian Graham wakati anazunguka ku-market his baseless book, (ambacho sidhani kama angepata hata maneno ya kuandika bila Klopp), kwenye interviews zake zote alikuwa anam-sneak attack Klopp sana.

Hawa watu (Edwards/Graham & Later Ward) walikuwepo at LFC kabla ya Klopp & DID NOTHING, WON NOTHING, they were NOBODIES, unakumbuka kina Edwards walivyokuwa memes of LFC social media platforms kipindi kile? Klopp came in a CHANGED everything, aliamua kufanya nao kazi, when the world was laughing at them, unakumbuka the same LFC fans walikuwa wanapiga kelele FSG waajiri DOFs? majina yakiwa ni Zorc & Monchi? unakumbuka FSG walivyomu-approach LVG for the DOF role? Klopp refused to work with LVG, he chose Edwards ambaye at that time he was just a data/computer nerd (kama mimi tu) and still very young, na unakumbuka blunders za awali za Edwards? mpaka akawa meme kwenye world football? but Klopp na his approch ya "father to son/brother to brother" decides to stick na Edwards, mpaka tunakuja kukamilisha first major signing chini ya Klopp (Mane) alikuwa kishaharibu few deals (kama Hughes tu now), but hakukatiwa tamaa, but now Klopp anakuwa sneak-dissed, na funny thing is kuna watu wanaamini.

It was klopp who told the Data/scout department to look at Mane/Matip/VVD/Fabinho & Gini. unakumbuka fiasco ya Blackpool? Klopp alivyobambwa na VVD kwenye mgahawa akifanya tapping-up? unakumbuka ishu ya Robertson? Alikuwa relegated na Hull City walikuwa wameruhusu goals si chini ya 80, jina lake lilivyoletwa na Scouts, kina Graham walimkataa, it was Klopp who said I WANT HIM, look at Roberston now.

Kina Edwards walivyoondoka LFC, wakajua tuta-struggle kwenye signings, wakisahau kuwa it was Klopp who made these signings possible, Klopp went on and signed Konate, Jota, Diaz, Szobo, Gravenberch, Alexis, Gakpo, Nunez etc, Wachezaji ambao Slot mwenyewe anasema ni hard sana kutafuta upgrades kwenye market.

Then Klopp signed Nyoni (Slot loves him so much), Klopp signed VDB & Fabio ambao leo hii kina Edwards wamepata pleasure ya kuwauza kwa BIG MARGINS, Klopp kakuza kids ambao leo hii wametolewa kwa BIG MARGINS. now Bradley, Quansah na Harvey ni first squad players, kina Eswards wanapata kiburi cha kukataa bids kubwa za Kelleher (who made Kelleher?) the club thinks he's worth ยฃ30-45m, again who made HIM?

Transfer window imekuwa ni DISASTER, na aliyekuwa anabeba LAWAMA zote za FSG na management, hayupo.

Can you blame FSG for this window? i hate FSG but ni big NO.

Club ilifanikiwa ku-accumulate ยฃ71m kwa kuuza youngsters tu, na ingeweza kufika ยฃ100M kasoro kama wangekubali bid ya jioni ya Forest kwa Kelleher, bids za Nat, Gomez, Endo & Kostas.

ยฃ71m gets you DM yeyote ambaye alikuwa kwenye market this season, kuanzia Zubi (ยฃ51m) mpaka kina Varela (ยฃ55m), na CHIESA (ยฃ12M). but after Klopp kupata a stop gap (Endo) last season, nerds walitakiwa kujua umuhimu wa DM, na nina uhakika Klopp aliacha list ya his desired DMs aliokuwa anasubiria wawe available, na funny thing is, hii window ndiyo ambayo Zubimendi alionesha indications za kutaka kuondoka Sociedad, utakumbuka kuwa we tried last summer and he was not interested, TW hii umepata nafasi, mchezaji kakupa go-ahead ya kuongea na his Club, then unaanza ku-negotiate a BUY-OUT clause, kweli? tena kwa installments 4, huyu ni mchezaji ambaye ameshazikataa Barcelona/Arsenal/Bayern etc, what is LFC? umepewa chance itumie, Zubi aliongea mpaka na Slot, Slot masikini akamtolea foot-map yake yote na jinsi gani atakavyomtumia, then unaenda kuharibu deal.

Na, kinachoumiza, Slot asked for a DM and CB, but aliomba sana kupata DM, maana aliona kwa style yake atahitaji muda sana na Endo, ambaye pia kibaya zaidi umri umeenda, sasa Kocha anakuja, hakupi mzigo, na anataka tu 1-2 players, unashindwa kumpa, then baadae yanaanza mambo yale yale kuwa hakuna DM wa ku-elevate team, for Gods sake, our natural DM ni Endo, unashindwaje kutafuta an upgrade on Endo kwa miezi mitatu?na unajiita transfer guru?

We missed the boat on Tchou in 2022, but then in 2023 we tried on Caicedo & Lavia na ku-fail, then asked for Zubimendi na hakukuwa na majibu mazuri, FSG refused to sunction deal ya Palhinha, Guimaraes had RC ya ยฃ100m, so we had to settle for a stop gap, (Endo) who did so well in my opinion, now anakuwa new gaffer, anaomba umpe tu DM, just a single DM, unaangalia list aliyoacha Klopp unakutana na Zubimendi, unamuuliza Slot anakwambia anafaa sana kwa his style, unauliza kwa his agent, agent ana-communicate na his Player, wanakuomba uende Spain, unafika Spain, mnafanya a good meeting, mchezaji anakubali kuja LFC, unatoka kwenye meeting ukiwa umepata tu a verbal YES, unaamua ku-brief medias about the deal, then unarudi kwa waajiri, (baada ya kuambiwa na agent kuwa buy-out ya player ni ยฃ51m) unaenda kuanza kutela ujanja wa kizamani kutaka ku-negotiate a buy-out, kwa kuwa tu player kakupa YES ya mdomo.

Sasa, imagine kama kwenye deal ya Zubi, Slot angekuwa na power ya maamuzi? ingekuwa tu, ni pay the RC, ni kama Klopp alivyowaambia FSG, pay RC ya Szobo hakuna room ya kunegotiate, FSG mpaka wakatumia third party (mkopo) kulipa ile RC (nahisi John Henry hakulala week hii, atakuwa aliumia sana), now umeuza youngsters ambao hawahitaji hata kuwa replaced, una ยฃ71m, why cant you pay the RC? unaenda kumsajili Mamar, wa nini? who needs a keeper now? mtu mwenyewe unayemsajili kuja kucheza ni mpaka Alli aondoke 2026 (Well, i think Alli will leave), ยฃ29m for a keeper, for what?

Mtu yeyote ambaye ata-spin hii transfer window kuwa ni positive, siyo LFC fan.

Slot amekuwa let down, but i believe in his coaching, kwa side ya pili, he has inherited one of the best squads in the league, na naamini players wata-show up for him. he deserves it.
 
If he can unlock the Beast Nunez we have ride to enjoy... Captain Chaos will be on ๐Ÿ”ฅ ๐Ÿ”ฅ ๐Ÿ”ฅ ๐Ÿ”ฅ ๐Ÿ”ฅ ๐Ÿ”ฅ.

Still positive mate if this bald gaffer get proper backing all shall be well.

YNWA

Man, i really really hope ataget the best out of Nunez.

if it goes all wrong, i can see Nunez at Atletico Madrid or Napoli next season, Chelsea are always in his ears, and he was discussed at Arsenal recently, but i dont think we will do business with them.
 
Issue ya DM liverpool imekua kama kipind flan cha Arsene Wenger na kusajil striker.

Ivi pale anfield hakuna ULTRAS?

Deal ya Tchou ilivyo-collapse, ilitu-cost sana, but then kama Caicedo deal ingeenda poa, tungekuwa na DM now, sidhani kama tungekuwa tunafurahia uwepo wa Lavia, maana sidhani hata kama ange-feature last season, so tushukuru deal yake ili-fail.

Tchou, caicedo & now Zubi ni big misses. but naamini kama Cheick (Crystal Palace) asingepata ACL, we wouldve tried.

We have Grav/Endo & Morton now at 6, ngoje tuone january.
 
Hatutakuja kuwa a seriuos club again. NON AMBITIOUS.

We will be alright.

Let Slot coach hii team.

He got let down by the nerds, na najua mambo yakianza kuwa magumu atakuwa subject ya abuses na lawama. but he's a very good coach, na naamini in the long run atafanikiwa sana at LFC.

It takes a coach with a lion heart kurithi mikoba ya Klopp, amekubali challenge, na naamini ata-deliver.

With or without the nerds.
 
Mapema mno kusema kwakweli, Klop amenifundisha ku BELIEVE, ametuondoa kuleeee........... #Doubters to Believers#

Edwards ame-fail this transfer window.

Mzigo umebaki kwa Slot, na najua ata-deliver kwa ukubwa sana tu, but a 6 angefanya kazi yake kuwa nyepesi sana.

Bado tuna kikosi kizuri sana, top three in the league kwa ubora, spine ya Allison-VVD-Trent-Salah bado inafanya tuwe one of the best teams/squads in europe.

I TRUST slot, but sitaki kumpa pressure kwasasa, tukibeba some trophies itakuwa safi sana, but tukishindwa this is his bedding season, so i wont complain, he's our gaffer now, na namuombea sana BARAKA.

He deserves it.
 

Nat earns ยฃ65k per/week mkuu, hakuna Club yeyote ile duniani inaweza kumpa huo mkataba na wages.

He will run down his contract next year, huwa anakataa offers za permanent sales kila transfer window, but next year, ndiyo utakuwa mwisho wake at LFC.

Na ni kaka yako Edwards ndiyo alimpa huu mkataba.

Nat is a millionaire.
 
FULL SQUAD.

GKs
Alli
Kelleher
Jaros

DEFENDERS
VVD
Konate
Gomez
Quansah
Trent
Bradley
Robertson
Kostas

MIDFIELDERS
Alexis
Szobo
Gravenberch
Endo
Curtis
Harvey
(Morton & Nyoni) & James too.

ATTACKERS
Salah
Diaz
Jota
Nunez
Gakpo
Chiesa
 
Hahaha

JF ni chaka ya kujificha ndugu yangu, so tunajificha ficha sana.

Am just a young kid, ndugu yangu.
Taja rika lako nijue kama mwanangu au mdogo wangu๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Ila upo vizuri sana aisee
Maandishi yako umepaka nini yanavutia kusema๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ