Mkuu
The MoNA tunaomba gemu analysis
Bado watu hawafurahishwi na uchezaji wa Liverpool ila wakiangalia score board & table wanajikuta kutabasamu.
Thats football, kuna watu wanakwambia Madrid haileweki aina ya mpira wanaocheza, unaweza kuvaana nao vizuri ila wanaweza kupata goli from nowhere, pamoja na hayo imefanya wamekua giants kwa muda ndani na nje ya Hispania, ulaya na hadi duniani.
Al Ahly ya nchini Misri kwa miaka ya hivi karibuni wamekuwa na mfululizo wa matokeo mazuri ila ndani ya uwanja hawaoneshi soka la kuvutia lkn kwenye trophies wamo season in season out, hata moja la ndani watabeba, nadra sana kutoka kapa.
Ilikuwa hivyo kipi cha Sir Alex na utd yake. Na kinyume chake Mzee Wenger na soka lake lenye mvuto wa aina yake, ila kombe lake kubwa FA & Top Four, its a matter of Choice. Kwenye mpira performance ni ya wakati huo ila makombe ni ya muda wote. Ni sawa na ambao hatukumuona Pele, Maradona na wengine, ambao ni miongoni mwa magwiji wa soka, historia yao inaendana na mafanikio ndio maana inakuwa rahisi kutukuzwa kwenye mpira.
Leipzig vs Liverpool:
Mpira ulikuwa mzuri, hakuna kuogopana, njoo nikiupata nakuja, njoo mie nakusubiri nikiupata nakuja.
Kwenye muundo wa pressing 3-2-4-1 ndio ulitumika kuwakabili Leipzig, anaanza Nunez kufuata mpira ili kuwafanya Leipzig waanze mashambulizi kwenye third yao, baadae Macca anasogea mstari wa juu kuungana na Salah, Gakpo, Szobo wanatengeneza line ya watu wanne, nyuma yao Trent anasogea mbele kuungana na Gravern kwenye ile 2 na nyuma ni Vvd, Konate na Tsimi.
Leipzig hii ni kwa ajili ya kukaba spaces mapema zisiwafikie Haidara, Simon na Sesko ndio Silaha yao. Macca alicheza kwenye advance role zaidi ya tulivyozoea kumuona akicheza.
Thats how we try to grab all three points.
Kudos to Kelleher he had a good game 6 crucial saves superbly. Anapokea £10k per week. He deserves more MOTM.
Two offsides goal, with offside trick applied part of the game,
The problem with LFC apart from getting positive results, we are lacking killers upfront. Yaani inategemea na wameamkaje siku husika.
Nunez as ST na role ya kurudi chini kusaidia kuzuia, kidogo anaitendea haki kutoka game vs CFC
Slot anajaribu sana, ku manage wachezaji, mechi ni nyingi unawahitaji wachezaji wote wakiwa fit mpaka mwisho wa msimu.
Salah alinunua baada ya ile Sub lkn Slot alielewa utanuna but we need you coming matches we play as a team not individual, hizi individual zitakukutea humo humo kwenye team.
Gravern amekuwa top player ndani ya LFC, (ukiaminiwa aminika), Amekuwa tegemezi tayari. Its up to Jones aoneshe ukomavu wake.
Good defence with good defending abilities, wanaweza kukupa mataji but a well balance team inakupa muendelezo chanya.
Kati ya zile mechi ngumu mbili tayari with three points in the bag.
Chelsea[emoji736]
Leipzig [emoji736]
Arsenal…..[emoji2375]
Up reds
Up LiverpoolFc
Ynwa’