Liverpool FC (The Reds) | Special Thread


11. The Kop

Ni jina lililotoka na vita vya Boer (Borr war) pale south Africa 1900, ambapo wanajeshi wa kiingereza walipigana ili kupata hilltop kwa jina la spioen Kop (Spioen means Spy and Kop means hill).

Wanajeshi 300 walipoteza maisha na wengi walitokea Liverpool, hivyo manusura wakaamua kutumia neno hilo Kop pale Anfield kwa ajili ya kuwaenzi wanajeshi wao. New stand ikaitwa The Kop End. Hapa hukaa mashabiki wenye hamasa na uchangamfu wenye ulevi wa mpira ni kushangilia mwanzo wa mchezo hadi mwisho wa mchezo non stop. Hawa jamaa hawakuwa wanakaa hii THE KOP END hapakuwa na siti, ila baada ya sheria ile kupita 1994 ya lazima mashabiki wakae kwenye siti, ndipo pakatengenezwa viti.

Ynwa’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…