Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

LADDER499.png
 
“Most goal scoring encounter”

Arsenal vs Liverpool.

Kwa wakamaria tip muhimu. Ukiona tu Arsenal vs Liverpool / Liverpool vs Arsenal weka zako mzigo first team to score Arsenal, weka Arsenal will score within 1st 15 mins, unachukua mpunga wako vizuri.


Kwenye football ukiutaka ubingwa, hakikisha wale mnaofukuzana kwenye ubingwa unawafunga na kama hauwezi basi hakikisha hawapati alama zote kutoka kwako. It is what had happened yesterday Arsenal vs Liverpool.

Arteta alijua aah, Slot ujanja wako unaanzia hapo katikati you have no natural DM let me ask you some questions, akaongeza bodies kwenye central zone wakati LFC ina wawili kati (Gravern & Macca) Arsenal ilikuwa na (Rice, Merino na Trossard), huyu Trossard kazi yake ni kupokea mipira na kuiwaisha haraka iwezekanavyo kwa Saka & Martinelli. Arsenal wakafanya Highline and high pressing (narrow high pressing).

Where did Arsenal won first half? Switch OFF ya Robbo, Macca, Diaz and Trent. Hawa jamaa walikuwa na siku mbaya sana kazini, kama sio ubora wa Konate at the back, may be yangeongeleka mengine by now.


Arteta vs Slot ilikuwa kama Slot vs Maresca.

Ni kama timu zilibadili jersey tu hivi ila kuanzia miundo na mbinu za timu zilifanana karibu 80% ila Arteta aka mjanja. Ili uweze kumuwin mpinzani wako kwanza;
1. Hakikisha unajipanga vizuri kwa mbinu zako
2. Ndani ya mbinu zako jaribu kuwaza mpinzani wako atakujaje kwa aina mbinu zako akiona umembana huku atatokea huku, sasa hapo kwenye kutokea pia upawaze (hauna passion na ukocha hautoboi haitaki uvivu).

Arteta aliitazama mechi ya LFC & CFC akajua nikiwabana kati lazima watataka kutokea kwa Long balls, na long balls target ni nani, Salah na Diaz. Akamwambia Timber sikia yule Salah tembea nae popote atakapoenda, Partey kaa na Diaz, ilikua Zonal and Man marking game kwa Arsenal.

LFC tried building from the back mambo hayaendi, wakaanza long balls huko pia kuna pin imepigwa. I think angekua Jota atleast ingeongeza kitu kwenye kuwin long balls ana combo nzuri akiwa front, Nunez hard work tried alot, as ST and False 9 role imeanza kumuingia, last two and half games anapata kitu kizuri na anatoa mchango mzuri sana both kwenye attack and defense.

Arsenal enjoyed first half kwa sababu four LFC players had bad days in the office. Macca, Robbo, Diaz and Trent. Haikuhitaji degree kuona Subs hizi ni muhimu sana tena mapema sana.

SECOND HALF:-

Kama ilivyoonekana kuna wachezaji ni abiria uwanjani, Slot noticed it na akachukua maamuzi ya haraka (this is what a coach should do). Fanya changes where it due, ASAP.

Diaz off Gakpo on
Robbo off Tsimikas on
Macca off Szobo on

And the rest are Joyous to LFC fans ater the final whistle. Jones akashuka chini kupiga na Gravern, Szobo as 10 Gakpo as wide attack.

Kwenye Football after tactics applied unahitaji wachezaji wakupe 100% work rate mmoja akiwa abiria kuna kuzidiwa tayari hapo its better muwe pungufu na mindset iwe hivyo mpo 10 men.

Hapa ikawa walioingia wanatoa work rate kubwa sana ishu ilibaki kwa Trent pekee but that didn’t bother us we had BEAST, Monster mentality (Mr. Ibou, Ibrahima Konate), this man under Slot amekuwa roho ya defense aisee. Feel sorry to Quansah alikuwa na opportunity game vs Ipswich but that horrible 45 mins zimetosha kumsugulisha bench. Anachokifanya Ibou ategemee tu Mickey mouse Cups, or injury or suspension hivi hivi tukutane next season hiyo.

Outstanding performance from Mr. Ibou.


After Subs Slot akawaambie hey punguza long balls sasa tunaenda nao toe to toe with ball control, ila kwa asilimia kubwa target RHS kwa Arsenal. Sasa huku tunaenda kuongeza energy, Gakpo Tsimi and Jones wakafanya ambush ya upande wa kule wa Partey ili kuzuia asipande wala kuingia kati kuongeza energy kwenye MF’s, Gakpo fresh leg, Tsimi fresh leg. Kwenye 4-2-4 wide pressing, building from the back, slightly long balls ikaingizwa.

Hapo ndipo rythym ikaanza kupatikana, possess through the MF, timu ikaanza build up from the back with less long balls.

Arsenal didn’t change anything kwa sababu mbinu zilikuwa upande wao how can you change what work for you?

Arsenal stayed compact well organized. Trent is Trent anaweza kupotea asionekane but his only one pass can change everything, ndicho kilitokea jana one long pass to Nunez ikabadili kila kitu, thats how World class player act. Dawa ya highline ni kucheza na spaces to behind the lines na hii ni super long balls.

Makeshift defense ya Arsenal ilirahisisha kazi sana, i’m sure Arsenal wangetimia wangetuuliza maswali magumu zaidi.

Kelleher instructed to play long balls kwa Salah & Diaz but were not super super balls, plus kuna muda as a player una opt some moments kutumia your natural football brain.

Kuna mudaa Vvd, Konate wanatanua ili kuomba mpira kwa Kelleher still sticked with long balls.

Gini vs among famous LFC comeback Barcelona, alikuwa instructed na Klopp acheze defensively, jamaa aka opt hiyo instruction akacheza attacking wise and got two goals, thats what expected to kelleher first half. Hapo ilipaswa tumtumie Trent & Vvd wenye quality passes. Ukimtumia Keeper pekee yake kwenye long balls maana yake opponents bado wapo kwenye patterns zao effectively, hapo mnapaswa mfanye 1-2-1-2 passes kuwaondoa kwenye zones wachezaje, bila hivyo long balls zote zitadondokea kwao na ndicho kilitokea.

Aggressiveness vs Calmness
Experienced coach and vs Inexperienced coach and experienced players

Arteta yupp Arsenal msimu wa tano sasa na wachezaji wa sasa anao atleast one & half season but Slot ana miezi minne tu mpaka sasa, but he tries alot.

Tunakosa huduma ya natural DMF my hope we should go back to Zubi, or Ederson, we need natural DMF.

N.B

Arteta aache uhuni afundishe mpira kuna muda Arsenal ina sound like child, wastage of time ya kipuuzi hivi, they need to be professional. Kwa mtindo wake huo marefee watawafundisha inavyotakiwa kufanywa.

Its time to say goodbye to Robbo, he is our legend yes but with him hatutapata tunachokitaka, since last season alionekana ku struggle sana, this season anaonesha dalili zile zile za last season.

Arsenal & Liverpool conceded from set pieces
Arsenal & Liverpool conceded avoidable goals.


Goli la kwanza la Arsenal Robbo could have done otherwise na kuwin ule mpira kwa mchezaji mzoefu kama yeye hakupaswa kusimama na mchezaji kwa left foot kwa umbali ule, even ndani ya box angelijua he his fellow lest footer angefanya otherwise easy goal conceded.

Goli la mwisho la mechi Kiwior alifanya run iliyotoa mwanya kwa Salah ku opt akae wapi mpira ufike, kama angekuwa Gabriel eneo lile naamini asingefuata move ya Nunez, angaendelea kukimbia na Salah tu.

Fair draw.

Up reds
Up Liverpool

Ynwa’
 
We just need fullbacks reinforcement

Mrembo wa kulia atamzeesha sana Ibu, yeye yuko husy kushambulia na kujilamba lips . Na kule kwa beberu ndio kabisaaaa kuna Charlie champlin na picha wake (vituko
Naona tetesi kwamba kuna uwezekano wa kufanya reinforcement back line January kwa upande wa kulia. Ishu ni huu mkataba wa Trent aidha wampe anachotaka ama wasonge mbele.. Muda utasema.

YNWA
 
Naona tetesi kwamba kuna uwezekano wa kufanya reinforcement back line January kwa upande wa kulia. Ishu ni huu mkataba wa Trent aidha wampe anachotaka ama wasonge mbele.. Muda utasema.

YNWA

Ule u scouser alionao ndio utambeba, halafu timu inafanya vizuri, naona itamshawishi kudemand high na zaidi akiwa na msimu mzuri individually ndio itadengua bila £350k hata kubali, ila twahitaji DM kama tunahitaji huduma yake. Hivi hivi watamzeesha Mr. Ibu mapema

Ynwa
 
Back
Top Bottom