Liverpool FC (The Reds) | Special Thread


Brother, kuna levels and classes kwenye mpira.

Output za Trent/Salah/Virgil/Alisson, huwezi kuziweka kwenye mrija mmoja na zile za kina Diaz Aisee, utakuwa una-fail.

World class players are rare, mfano at City, world class players ni watatu tu (Rodri, Haaland, KDB), at Arsenal, i'd say Saliba, Magalhäes & Saka, at Chelsea kuna potential suitors ambao wanaweza ku-enter hiyo sphere in few years (Caicedo & Palmer), Spurs had Son but he's done, so hawana a world beater now, there are no world class players at Utd, Spurs, Chelsea etc.

At LFC, tumebahatika, tuna Salah, Virgil, Trent & Alisson.

WC players, ni unique players, Gakpo.& Diaz are doing so good this season, and i'm so happy, especially for Gakpo, but output yao bado ni ndogo sana uki-compare na ile ya Mane (WC player), na huwezi kulaumu because ni ceiling yao, Diaz & Gakpo wakiondoka LFC, kuna 5-10 players kwenye PL midtable teams can replace them, na usione gap yeyote, mfano, Mbeumo ni right profile ya kum-replace Salah, kama Salah akiondoka leo, Spearmann lazima atashauri Club imuangalie Mbeumo, ni right profile, but atakupa namba za Salah? NO, but Mbeumo atakupa numbers za Diaz & Gakpo, tena na zaidi.

Kwamba, Trent akipewa 300k, Diaz & Gakpo wata-ask for the same amount? kwa kipi my brother? kwa outputs zipi? maana mpira ni outputs, Edwards ana kina Gakpo zaidi ya 100 kwenye his laptop, uje umwambie akupe 200-300k? kaka? kweli?

Chiesa kwa bahati mbaya anapata kadhia ya majeruhi, lakini numbers zake ni hizo hizo za kina Diaz, na tumemnunua kwa 10m tu.

Trent, anacheza LFC, so tunamchukulia poa, na tunajifariji kwasababu ya kinachoendelea, but ile ni generational TALENT, uliza scout yeyote, hakuna Profile kama ile kwenye market, HAKUNA, au unadhani Fro Perez anahangaika bure? kila siku yupo UK anahangaika na Trent tu, acha mzaha. kama angekuwa ana mkataba at LFC now, bei yake isingekuwa chini ya £100m yule, Aisee ni Trent tunamuongelea hapa.

Wakati tunavunja record ya kumnunua Virgil, dunia ilitucheka, sahiv profile ya Virgil unaipata wapi? profile ya Alisson unaipata wapi? Au kwa kuwa wanacheza LFC, tunaona ni kawaida. maana ni kawaida kwa LFC fans kuamka asubuhi na kuanza kuwatukana hawa players wakiwa na bad games, na ni kawaida, maana wote tunakuwa na emotions,.kuanzia kwa kina Trent mpaka kina Salah, but hizi ni unique profiles, very unique profiles.

Wakati, tunamnunua Szobo kipindi kile, nilisema kuwa tumepata a rare profile, bahati mbaya Szobo haku-hit the ground running, so kuna watu walikuwa wanamsema kila siku humu, (kawaida ya LFC fans), but now ile profile unaipata wapi? nipe kazi ya kukuletea kina Alexis, nitaenda France/Italy/South America, na nitakuletea kina Alexis wa kutosha, but siwezi kukuletea Szobo, but we take him for granted, God forbid akiwa na bad game, but Szobo ndiyo funguo ya Slot kwenye big games.

Trent, has earned anachokitaka, if you cant give your WC player 300k.p/w, utampa nani sasa? kila siku tutakuwa tunasingizia wage structure? we are a big club, kama huwezi ku-offer wachezaji wako wakubwa big wages, kuna big guns wenzako watafanya hivyo.

If we got a DM in the summer, Ryan angekuwa ana-rotate na kina Szobo/Curtis, kama Slot aki-abandon hitaji la kununua a DM kwasababu ya uwezo wa Grav pale kati na kuamua kuendelea nae (no problem at all), the best he can ask in his new contract ni 120-30k, akienda juu ya hapo, simu zitalia kwa wadau, tutaingia chimbo.

Curtis? c'mon man.

Alexis, i'm 100% sure, Madrid/Barca wakija, he will force a move, but ni repleciable.

Mission ya Club kwasasa, ni kuhakikisha, our big 4 wanabaki, for 2-3 years, huku kukiwa na iniative za kutafuta warithi kwa nguvu zote na kwa kutulia, though output zitakuwa hazifanani, but tutahitaji ufanano wa profiles, maana tukihitaji same profiles with close/same output ili ku-replace our big 4, itahitajika pesa nyingi sana.

Mfano, if you want to replace Virgil, utatakiwa u-replace his Leadership, Aerial & ground dominance, Agression & Speed, body size, passing Vision & ability, space & 1v1 defending, in-game management, etc, kwa UK, vichache na vya muhimu utavipata kwa Saliba, but Arsenal watakuuzia? na hata wakitaka kuuza, utatoa £100m? so it will take time, to replace these players, hence tunahitaji wawepo.
 
MosDef Asante kwa taarifa Mkuu hivi ni kweli ...Michael edwards Ana uhuru wa kufanya kazi yake haswa kwenye hizi issue za mikataba? And if not kwanini alikubali tena kurudi Liverpool to work with the same owners? Au na yeye anatekeleza falsafa zao

Edwards ni mfanyakazi wa FSG, kwa mwamvuli wa LFC.

His MAIN job & wajibu, ni ku-protect interests za his owners & not LFC.

Kazi yake ni ku-initiate best possible deals for FSG.

Hana "say" kwenye financial operations zozote za Club, just like any other employee.
 
Acha ujuaji
 

Binafsi…

Naamini Trent atakuwa replaceable aisee, regardless of the number he has kwenye Club, but sijaona timu ikishake kwa kumkosa RB, ila kwa CB, MF’s na Attacker.
Yes he is a world class, he has good number as a RB, i agree.

Kwa anavyopanga Slot timu yake, you can see ni rare kutegemea his RB’s ku produce offensive numbers (assists,Goals,Key passes), na hapa ndio ubora wa Trent ulipo.

Kama RB atalipwa more the £300k in a near future, offensive players wata demand £ 400k under LFC itazidi kuwa ngumu. Bado naamini ni rahisi kuziba nafasi ya Trent kuliko Salah & Vvd.

I will still stand with FSG kwa hili kama Trent anahitaji more than £300k per week.
For RB??

Ynwa’
 
Huyo jamaa yenu kama kweli yupo anfield basi ya gongolamboto
 
LIVERPOOL vs MANCHESTER UNITED
Jumapili kunakazi, haitakua lelemama kihivo kama tunavyoaminishwa

United kweli imeoza ila inabaki kuwa ni United dhidi ya Liverpool inayoutaka ubingwa.

Ni siku ambayo Slot inabidi atuonyeshe sisi tunaomuamini kuwa ni kocha wa malengo.

Ni mechi ya tahadhari ukizingatia misimu karibu yote under JK hatukuwahi kuwafunga worst united either Anfield or OT tunapokuwa serious tittle contenders.

JK ni kweli ana namba nzuri against united lakini je zilitusaidia kubeba chochote? Jibu ni NO.

Arne Slot anakazi ya kujibu hicho kitendawili.

Ill take 1-0 mradi tuu ziwe ni 3pts
 
Game rahisi sana hii. Game ina nagoli mengi tu hii. United kwa forwardline yao sioni wakifungua backline yetu.
 

Brother.

Sidhani kama kuna reports zinasema kuwa Trent wants more than 300k. unless unataka kuingia kwenye PR trap ya FSG, i mean, nimekuwa nikiona this movie since 2011, so FSG PRs hazijawahi kunisumbua (personally).

Defender mwenye Goals contribution zaidi ya 110, tena at just 26 years old (with 20+ goals and more than 85 assists), huwezi kusema ni just RB, utakuwa unaongea kama siyo mtu wa mpira.

How many offensive players wana-post hizo numbers? una attacking MFs kwenye team yako ambao hawana hizo numbers na hatujui kama wanaweza kuzifikia, but tuna RB anatupa hizo numbers consistently brother, he's not just an RB, weka emotions pembeni.

Mkuu, small details kwenye mpira ina-matter sana, how can you watch Slot's offensive structure, na kushindwa kung'amua kuwa ameitengeneza offensive structure yake yote around Trent? kwenye offensive structure ya Slot, ni mchezaji gani ambaye amepewa extra-time/shot ya kuwa na nafasi ya kuchezea mpira/screen the pitch & face the play? ukiachana na enhancement ya 1v1 defending, nani yupo tasked na ku-minimize attacking threats & counters from middle & wide areas? ukiangalia structure (even, diagrams ambazo zipo kwenye hii threads), wakati Ryan/Alexis/Szobo/Curtis/Robbo, wapo kwenye defensive/offensive actions, Trent anakuwa wapi? ile space anayotengenezewa ni ya sababu gani? na kwa hilo tu ame-impact games ngapi kwa his one/first-touch long/shot pass?

Ukimuambia Slot amuondoe Trent now, Shape yake yote inabadilika, he will have to change kabisa set up ya MF, angebadilisha kabisa set-up ya front 3, Gakpo/Diaz wasingekuwa wana-attack the post consistently, Salah asingekuwa na uwezo wa ku-charge kwenye box kila akipata mpira, maana offensive starting point ingekuwa limited sana kwasababu kunakuwa hakuna one-way channels za passes kati ya Trent na Salah, Klopp tried to invert Trent, but Slot ame-tweak zaidi, na kutumia his one/first-touch action to dictate and open up our attacking traps.

Against West Ham, Trent had 93 touches, more than any LFC player on the pitch, and game yote ile ilikuwa dictated na Trent, kairudie ile game, uone role ya Trent kwenye offensive set-up ya Slot na base ya hiyo set-up ni nani.
 

3-4 goals minmum.

Hakuna team ya kuisumbua LFC pale, hizo gimmicks za kuwa game yetu dhidi ya Utd huwa haitabiriki, hazina maana yeyote kwa Utd hii ya sasa.
 
Even Bradley is better than him
 
People are actually mad at Trent, because Madrid wants him, LFC fans huwa wanachekesha sana.

Salah & Virgil had to cry kwenye media kuhusu mikataba mipya, na bado watu wanatafuta good words for FSG, au Trent nae alitakiwa alie kama kina Virgil kwenye media, ndiyo tuone kuwa anajali?

FSG walikuwa wapi mpaka hawa wachezaji wote wamebakiza 6 months tu kwenye mikataba yao? how can you blame players for this?
 
This was Alisson back in August, amebakiza 2 years in his deal, mwakani atakuwa kabakiza mwaka mmoja, then itabaki miezi 6, then tutaanza kupata hit-pieces, and fans will turn against him, FSG watabaki na Mamar, a 50k p/w GK.
 
Szobo anatumika kama punda now, itafika kipindi, nae atadai kile anachoona anastahili kutokana na kazi anayofanya uwanjani, nae ataanza kuwekewa longo longo.

atauzwa, tutatafuta a new Szobo, na kuanza kumpa time ya ku-adopt, then tutakuwa tunajiuliza why hatuna sustained development.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…